.

Saturday, April 30, 2011

HALLLLAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

David Beckham na mkewe victoria

Malkia ELIZABETH II akiwasili Westminster Abbey
                 Sir  Elton John akiwasili na  Mume wake David furnish

Friday, April 29, 2011

PICHA ZAIDI KUHUSU HARUSI YA KIFALME
In this image taken from video, Britain's Prince ...
inawezekana kina dada wengi walikuwa wanamtamani lakn wapiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Prince William, Kate Middleton, Kate, Duchess ...
mambo ya Duke Of Cambridge
   
 .
Britain's Prince William kisses his wife Kate, ...
jamani jamani jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Kate Middleton, Michael Middleton, Pippa Middleton
Heshima lazima iwepooooooooooo
Britains Prince William and his wife Catherine, ...
Gari hii ilitumiwa pia na prince charles na mkewe marehemu princes diana mwaka 1981 ambao ni wazazi wa prince william wakati wa harusi yao,imetumiwa pia na prince william na mkewe cate
 

PWEZA IKER ATABIRI USHINDI MECHI YA MARUDIANO KATI YA MADRID NA BARCELONA

Pweza aliyepewa jina la Iker wa nchini Hispania ametabiri kuwa Real Madrid wataigaragaza Barcelona na hatimaye kufanikiwa kucheza fainali ya kombe la mabingwa wa ulaya.
Pweza huyo ambaye awali utabiri wake kwa mechi mbili za wababe hao wa Hispania ulikuwa wa kweli, ametabiri kwa mara nyingine kuwa Real Madrid watafanikiwa kuitoa Barcelona kwenye mechi za nusu fainali ya kombe la mabingwa ulaya.

Pweza huyo aliyepewa jina la Iker kwa heshima ya golikipa mkongwe wa Real Madrid, Iker Casillas alitabiri mechi mbili zilizopita za watani hao wa jadi ambapo ya kwanza walitoka sare ya 1-1 wakati mechi ya pili Madrid walishinda 1-0.

Pweza huyo mwenye uzito wa kilo 16 aliwekwa kwenye Aquarium kwenye mji wa Benalmadena uliopo kusini mwa Hispania ambapo alikimbilia kwenye sanduku lenye bendera ya Real Madrid na kuliacha sanduku lenye bendera ya Barcelona. Masanduku yote mawili yalikuwa na chakula kwaajili ya kumvutia Pweza huyo.

Madrid na Barcelona wanapambana kesho jumatano kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali itakayochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu wakati mechi ya marudiano itakuwa kwenye uwanja wa Barcelona, Nou Camp mnamo mei tatu.

Timu itakayofanikiwa kumtoa mwenzake itakutana na mshindi kati ya Manchester United ya Uingereza na Schalke 04 ya Ujerumani.

WAMJUA MTU MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI?

Junrey Balawing huenda akatangazwa mtu mfupi kuliko wote duniani mwezi juni mwaka huu atakapotimiza umri wa miaka 18 akiwa na urefu wa sentimita 56 tu. GONGA Life Style Pembeni Kushoto kwa habari zaidi.

YAWEZEKANA BABA KUMUOMBA MWANAYE MSAMAHAA?

Katika mazingira ambayo tunakulia sisi watanzania mara nyingi mama ndio anakuwa karibu na watoto zaidi kuliko baba. Ofcourse hii inaweza kubadilika kutegemea na familia husika. Ila kwa mtazamo wa ujumla naweza kusema hivi ndivo ilivyozoeleka. Sasa mara nyingi baba anakuwa mkali kwa watoto inafikia hatua mtoto akimuona baba amerudi kutoka kazini badala ya kufurahia ndio anasikitika. Anamsalimia then anatafuta sehemu ya kujificha. Well, hili si tatizo sana maana sometime inakuwa ni nature ya mtu kwamba anakuwa yupo hard kwa kila mtu hata kwa familia yake.

Sasa tatizo linakuja pale huyu baba ambaye hana ukaribu na wanae pale anapojikuta amemchapa mwanae kimakosa au kampiga kimakosa then kwa sababu yupo too superior anaona kuomba msamaha kwa mwanae ni udhaifu. Akijiangalia kwa jinsi anavyo behave then aseme samahani....anaona duh hii nitakuwa nimejishusha hadhi yangu. Anaamua kunyamaza tu na kuendelea na maisha kama kawaida.

Sasa ubaya wake ni kwamba mtoto nae anakulia katika mazingira kama hayo. Hajafundishwa kuomba msamaha na hajawahi kuombwa msamaha. Hali hii inakuwa inaendelea kutoka kizazi hadi kizazi. Mimi sidhani kama ni aibu au kujidhalilisha kama ukiamua kuomba msamaha pale unapofanya makosa hata ka wale waliokuzidi umri. Ndio inakuongezea heshima maana binadamu mara nyingi tunakumbukana kwa mabaya so watu wanapokuzungumzia pale ulipochemsha basi watasema pia kuwa uliomba msamaha. Mimi kwa mtazamo wangu nadhani ndio inaongeza utu wako mbele za watu.

Anyway point ya muhimu niliyotaka kuisema ni kwamba mara nyingi kuomba msamaha kwa mwanao inakauwa ni vigumu zaidi kama utatengeneza umbali kati yako na watoto wako. Ikishakuwa hivyo kama ukimfanyia makosa mwanao kuomba msamaha inakuwa ni kazi ngumu sana. Kuna familia moja naifahamu ambayo baba na mama huwa wanashindana kutengeneza ukaribu na watoto wao hali ilinivutia sana sio siri. Hope kwamba we can adopt some ways of living from other families. Hii haimaanishi kuwa upo dhaifu. Kwa sababu be sure kwamba zipo pia familia ambazo pia zina adopt some ways of life from you
.

"DINGI AKINISTUKIA SIJUI ITAKUAJE?"

NI KWELI MAENEO YETU YANANUKA?

"JAMANI TUSISUBIRI MVUA ZIKATIKE HALAFU TULALAMIKE NJAA"

UKIMUONA AKIWA ANAENDA OFISINI ANAJIHESHIMU SANA LAKINI!!!!!!!!!!!!!!!!!!



Hapa akiwa maeneo yake ya home


"SIJALALA NAKUSANYA NGUVU ZA KUKATA MAJANI"

  Bwana Frank akiwa amejipumzisha kabla ya kuanza kukata majani maeneo ya Ilala. Yawezekana kabisa jamaa amesahau ule msemo "USIFUGE WANYAMA MJINI" maana hawatapata malisho mazuri kama vijijni, huku mjini watakula lami.

"HUKU KWETU ZINA SOKO SANA TUPE FURSA TUJE TUWEKEZE NA KWAKO"


JK akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wamafunzi
wanaosoma katika vyuo mbali mbali nchini Misri baada ya kukutana na kuzungumza nao mjini Cairo.
JK alionesha kufurahiswa na juhudi zao walizo zionesha na kujitolea kompyuta 6 na amehadi kuwasidia zaidi hapo baadae, JK alitoa mchango mara tu baada ya kusomewa risala ya wanafunzi iliyosomwa na katibu mkuu wa unoja huo ND. Gharibu nasro, ndani ya risala hiyo waliomba serekali inayo ongozwa na JK kujenga kituo cha utamadu nchi humo na Raisi aliwahidi kulifanyia kazi.

Wednesday, April 27, 2011

LIL WAYNE: NITASTAAFU NIKIFIKISHA MIAKA 35

Rapper mkali kutoka nchini Marekani,Lil Wayne ambaye amekuwa katika game tangu akiwa na umri wa miaka 15 tayari ameanza kuzungumzia kustaafu mara atakapofikisha umri wa miaka 35. Lil Wayne ambaye miongoni mwa wafuasi wake kupitia label yake ya  Young Money ni pamoja na Rapper mkali mzaliwa wa Toronto,Canada na rapper machachari wa kike,Nicki Minaj, hivi sasa ana umri wa miaka 28. Kwa maana hiyo Rapper huyo ana miaka mingine 7 tu kusimama imara katika ulingo wa muziki.
Akizungumza na Angie Martinez wa Hot 97, Lil Wayne ambaye mashabiki wake hupenda kumwita “Weezy” alieleza kwamba atahakikisha anajituma kwa kadri ya uwezo wake ili kupumzika atakapotimiza miaka 35. “Hiki ndicho kinachotokea unapofanya kazi sana.Watu wanadhani kwamba unaposema unafanya kazi sana ni kwamba unafanya kazi masaa mawili ya ziadaHaya ni maisha yangu, “alisema. “Ndio maana kustaafu katika umri wa miaka 35 ni sawa sawia kabisa kwangu”
Wakati wasanii wenzake kadhaa waliwahi kutangaza kustaafu na kisha kurudi kwenye game ,kama vile Jay-Z, Lil Wayne anaweka bayana kwamba yeye hatanii anaposema hivyo. “Huu ni mpango madhubuti kabisa na nitautekeleza, ”
Alipoulizwa kama ana mpango wa kuendelea kupata watoto wengine, rapper huyo aliweka wazi kwamba hana mpango huo,”Hapana,nipo sawa kwa sasa.Nina watoto wanne na nadhani wananitosha kwa wakati huu”
Hivi sasa Lil Wayne yupo katika tour “I am Music II tour” pamoja na Nicki Minaj, Rick Ross na Travis Barker na anatarajiwa kuachia album yake mpya ya The Carter IV tarehe 16 Mei mwaka huu.

MAWAZIRI TANZANIA: UNAONAJE UTENDAJI WAO...SO FAR?

Msomaji mwenzetu mmoja hapo jana aliomba kuona picha ya Baraza la Mawaziri la sasa baada ya kuona picha ya Baraza la Kwanza la Mawaziri baada ya Muungano katika post iliyopo hapo chini inayomzungumzia Oscar Kambona na Wikipedia.
Kwa bahati mbaya,hatuna picha ya Baraza la Mawaziri lililopo madarakani hivi sasa wakiwa wamesimama au kuketi pamoja. Badala yake tunayo picha hii ambayo tuliitengeneza wenyewe ya Baraza la Mawaziri lililopo madarakani.Kuna fununu kwamba siku si nyingi,Rais Kikwete atafanya mabadiliko katika baraza la mawaziri lililopo.
Sasa badala ya kuweka tu picha na kusema “pichani ni Baraza la Mawaziri na kisha kutoka kushoto kwenda kulia ni yule na yule na yule’,nadhani ni wakati muafaka tukajiuliza,Je unaonaje utendaji wa Mawaziri hawa mpaka hivi sasa?Yupi ambaye unaona anafanya kazi yake ipasavyo na yupi analegalega au kutowajibika kabisa.

OSCAR KAMBONA: MAISHA YAKE KWA MUJIBU WA WIKIPEDIA

Mwaka juzi niliandika kidogo kuhusu umuhimu wa kuandika na kutunza historia zetu hususani mitandaoni katika zama hizi za maendeleo makubwa na ya kasi ya sayansi na tekinolojia.
Nakumbuka niliandika na kuomba wajuzi wa historia ya nchi yetu,kushiriki katika kuandika na kuitunza historia ya Mwanasiasa Mkongwe,Hayati Bibi Titi Mohammed kupitia mradi wa Wikipedia ambao leo hii unasifika na kuaminika kuwa chanzo cha maarifa mbalimbali.Kwa bahati mbaya,mpaka hivi leo ukurasa wa Bibi Titi Mohammed katika Wikipedia bado una mapungufu.Unahitaji kuendelezwa.Ni kweli kwamba hakuna anayejua kwamba Bibi Titi alizaliwa wapi na kwamba hata tarehe yake ya kuzaliwa haijulikani zaidi ya kwamba alizaliwa mwaka 1926?
Pamoja na utata ambao umekuwa ukijitokeza mara kadhaa kuhusu usahihi wa kinachoandikwa katika Wikipedia,hivi leo inasemekana kwamba wanafunzi wengi,hupata maarifa yao kupitia Wikipedia.
Utata unaojitokeza kuhusu usahihi au kinyume chake katika Wikipedia, unatokana na ukweli kwamba Wikipedia inaandikwa na kila mtu.Wewe na mimi.Kila mtu ana uhuru wa kujiunga na Wikipedia na kuchangia.
Hatari ya uhuru huo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa mtu au watu kuandika historia katika jinsi ambayo itakidhi mahitaji yao na hivyo kuandika habari potofu au za uongo.Hilo linaweza kufanyika kwa bahati mbaya au makusudi.
Kama hunipendi mimi Jeff Msangi,basi unaweza ukaingia katika Wikipedia na kuandika unachokitaka wewe mpaka hapo mwingine anayeijua historia yangu kwa jicho lingine,atakapoingia na kusahihisha.Kama mimi mwenyewe nipo hai pia naweza kuwaandikia Wikipedia na kutoa malalamiko yangu na wao watarekebisha.Kwa kawaida,mtu binafsi haruhusiwi kujiunga na Wikipedia na kuandika habari zake binafsi kwa minajili ya kujitangaza na mambo kama hayo.Historia yako inaandikwa na watu wengine.
Sikumbuki nilikuwa nawaza nini leo nilipoamua kujaribu kutafuta habari zinazomhusu Mwanasiasa mkongwe,Marehemu Oscar Kambona(13th August 1928-July 1997). Historia yake,kwa mujibu wa Wikipedia, imeandikwa vizuri na kwa umakini.Nasema kwa umakini kwa sababu imeandikwa kwa nia ya makusudi ya kuelezea maisha ya mwanasiasa huyo katika miale ya kumtaka msomaji kuelewa vizuri historia yake na kile kilichojiri mpaka akaja  kutoelewana na serikali ya awamu ya kwanza  na bila shaka Hayati Baba wa Taifa,Julius Kambarage Nyerere mwenyewe. Lakini kila kitu kilichoandikwa pale ni sahihi? Mtiririko ule wa matukio ndivyo ulivyokuwa? Ni kweli kwamba Kambona na Nyerere walishindwa kuelewana katika suala zima la siasa za Ujamaa na Azimio la Arusha peke yake? (Nyerere aliamini katika Ujamaa wakati Kambona aliamini katika Ubepari)

KIKWANGUA ANGA KINAKUJA TANZANIA


UJENZI USHAANZA HAPO KWA CHINI



TATU WAJIDANGANYA TABORA JAZZ BAND


Kheri iwe kwako msomaji.Natumaini hujambo na wiki hii haikuwa mbaya kwako.Kama ilikuwa na mikwaruzo,basi ni ile ambayo unaweza kuikabili.Kama ilikuwa ngumu sana,basi mwachie Muumba.Yeye anaweza.
Hii ni weekend ya katikati mwa mwezi. Hapa tunaweza kusema kama hesabu za mwanzo wa mwezi zilikwenda kombo,basi leo tanki la mafuta lipo chini ya mstari wa katikati.Usitie shaka,wenzako wakikupigia simu kwamba muongozane kwenda viwanjani,tia  kisingizio cha “dozi ya malaria”. Si unajua hakuna kitu kibaya kama kwenda mahali na kuanza kutumbua huku hesabu kali zikiendelea kichwani.Unaweza kabwa na mnofu wa nyama.Kile kicheko cha bar ya kona kinaota mbawa. Zile mbwembwe za “tuletee kama tulivyo na kisha mwambie jamaa wa jikoni aje” leo sio mahala pake.
Ushauri wangu;weekend hii tumia muda wako nyumbani.Cheza na wanao.Soma nao,cheka nao. Hilo likikushinda (yawezekana hujazoea au watoto wana ratiba zingine za birthday parties nk, basi jisomee.Kama unacho kitabu cha After  4:30 cha David G.Mailu kikamate uso. Kuwa makini,kilipigwa marufuku. Sishauri kukamata remote na kuanza kubadili channel. Ina raha gani kushinda kutwa  ukitazama wenzako wanafanya wanachokipenda na kulipwa ilhali wewe chali?! Aste aste,msaada kwenye tuta.Vyovyote vile iwavyo, usikate tamaa,ni life.Kuna leo na kuna kesho. Unaweza lala masikini ukaamka tajiri.Cheza karata zako vyema.Jitokeze mahali sahihi katika wakati sahihi au muafaka.
Leo katika Zilipendwa tunaelekea Tabora.Kule tunawakuta Tabora Jazz Band.Miaka mingi imeshapita tangu nitembelee mkoa wa Tabora. Leo hii sina hata kumbukumbu nzuri kwamba mara ya mwisho kufika pale ilikuwa lini.Pamoja na hayo, bado ninakumbuka kwamba niliupenda ule mji.Enzi zile,ulikuwa ni mji simple usio na mengi.Watu walijuana vyema.Nakumbuka Chuo cha Uhazili.Kilisifika kwa kutoa makatibu muhtasi wa “ukweli”.Mama zangu wadogo kadhaa wamesoma pale.Nakumbuka shule ya sekondari Uyui.Nilikwenda pale kumsalimia mjomba wangu alipokuwa anasoma pale. Nakumbuka Tabora Girls na Tabora Boys. Mpaka hivi leo nina ndugu wanaishi maeneo ya kule. Nakumbuka disco la pale.Mwana Isungu.Hospitali ya Kitete.Tabora,Tabora,Tabora…nitarudi.
Tukiachana na kumbukumbu yangu inayofifia kuhusu Tabora,Tabora Jazz Band wanao wimbo unaoitwa Tatu Wajidanganya. Kwamba Tatu anadhani kwa sababu anapendwa,basi anayo nguvu ya kumgombanisha jamaa na ndugu zake.Penzi likashinda undugu.Inawezekana?
Wimbo huu ni miongoni mwa zile nyimbo ambazo kwa namna fulani zilikuwa zinatupa kitambulisho cha muziki wa kitanzania ambao ulikuwa ni mchanganyiko mzuri sana wa Afro-Jazz au Afro-Cuban.Jaribu kusikiliza jinsi ala zilivyopangwa.Piga picha jinsi jamaa walivyokuwa jukwaani na zile bugaloo zao.Burudani ya kutosha.Basi burudika  na Tatu Wajidanganya na uwe na weekend njema

JAMANI MTUSAIDIE KUJENGA DARAJA HUKU KWETU

Wakazi wa Dar es Salaam wakivuka Mto Tegeta wakiwa wamebebana baada ya daraja linalounganisha Salasala Kilimahewa na kulangwa Goba kubomoka.

Tuesday, April 26, 2011

KATIBA MPYA TANZANIA

Uundwaji wa Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara na Majukumu yake 
Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara (“TLS”) ni Taasisi ya Wanasheria wa Tanzania Bara iliyoanzishwa kwa Sheria ya Chama cha Wanasheria cha Tanganyika, Sura ya 307 Toleo la 2002. Kwa mujibu wa Sheria hii, Chama kina, pamoja na mambo mengine, jukumu la kuisaidia Serikali katika mashauri yanayohusu utungaji wa sheria na utekelezaji na matumizi ya sheria, na pia kulinda na kusaidia umma katika masuala yote yanayohusika na kadhia za sheria.
Chama cha Wanasheria kinatoa taarifa hii kwa mujibu wa mamlaka mahsusi ya sheria.

Mazingira ya Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba, 2011
Tarehe 11 Machi, Muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba, 2011 (kwa kifupi “Muswada”) ulitangazwa katika Gazeti la Serikali la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Toleo Namba 1 Jarida Na.2. Chama kilipata nakala ya Muswada huo Jumanne, tarehe 30 Machi, na kilisambaza hizo taarifa kwa wanachama wake siku ya Alhamisi tarehe 31 Machi ili kupata maoni yao. Siku ya Jumamosi tarehe 2 Aprili, Chama cha Wakufunzi wa Chuo cha Dar es Salaam (UDASA) waliendesha mjadala wazi kuhusu Muswada, mjadala ambao uliripotiwa kwa mapana katika vyombo vya habari. Siku ya Jumanne, tarehe 5 Aprili, Chama chetu kilialikwa kupitia Kurugenzi ya Kamati za Bunge (“Kurugenzi”) kushiriki katika mjadala juu ya Muswada ambao ulipangwa kujadiliwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Bunge (kwa kifupi “Kamati”) tarehe 7 Aprili Dodoma, kama ilivyopangwa awali. Mnamo mwisho wa siku hiyo Chama chetu kiliulizia maendeleo kuhusu mijadala bayana, na kikahabarishwa kwamba sasa sehemu mpya tatu (3)zimetajwa kwa ajili ya mijadala bayana, yaani Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar; aidha taarifa tulizopata ni kwamba mijadala itafanyika tarehe 7 na 8 Aprili, na ikibidi tarehe 9 Aprili. Kutokana na uthibitisho huu,Chama chetu kikaahidi kushiriki kikao cha Dar es Salaam.
Jumanne tarehe 5 Aprili Muswada uliwakilishwa Bungeni kwa Hati ya Dharura isomwemara ya kwanza. Tarehe 7 Aprili, Rais wa Chama chetu aliipelekea Kamati - kwa maandishi - maoni na mapendekezo ya wanachama wa Chama cha TLS kuhusu Muswada. Tarehe 8 Aprili, Rais wa Chama cha TLS alitoa mapendekezo kwa mdomo.
Baada ya kushiriki katika mijadala ya umma, Chama kilitiisha mdahalo kuhusu Muswada kwa wanachama ili kuhakikisha mawazo ya wanachama wengi iwezekanavyo yanakusanywa kuthibitisha msimamo wa wengi katika Chama. 

Hoja na Maoni

UTANGULIZI
 
Kwa kuwa Chama cha TLS kimejizatiti kwa dhati kuimarisha na kuendeleza utawala wa sheria nchini Tanzania, kwa kujua kwamba sheria inapozingatiwa ipasavyo, utawala wa sheria huwalinda wananchi dhidi ya matumizi ya kibabe ya mamlaka ya Serikali; kwa kuwa tunaafiki dhana kwamba sheria zote lazima zitungwe kwa shabaha ya kuenzi Utawala wa Sheria, utawala bora na nyanja ya demokrasia ambayo imejengewa misingi imara katika falsafa ya haki ya nchi yetu na ambayo inashabihiana na viwango vya kimataifa na vyenye ubora maridhawa; kwa kuwa Chama kinaamini kwa dhati kwamba hatima na mchakato mzima kuhusu marejeo na utungaji wa Katiba mpya unapaswa kupata uhalali muafaka kwa njia ya ushirikishwaji wa wananchi; na kwa kusisitiza kwamba haki haitakiwi tu ifanyike, bali pia ionekane kwamba inafanyika, Chama kinaeleza msimamo wake mintarafu ya Muswada kama ifuatavyo: 

1. Kuhusu lugha ya Muswada: Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba Muswada utangazwe katika lugha ya Kiswahili, kwa kuzingatia dhana ya haki kupatikana (jambo ambalo linamaanisha mtu wa kawaida kupata nakala na uelewa) kwa Watanzania wote (wanaoishi vijijini na mijini, wananchi wa kawaida, wenye mapato ya kati na wa matabaka ya juu), ikiwa ni sambamba na lugha inayotambulika ya toleo rasmi la Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya
 Tanzania, 1977 (kwa kifupi “Katiba”); 
2. Kuhusu jina la Muswada: Chama kinashauri kwa dhati kwamba jina la Muswada lisomeke ‘Muswada wa Kutunga Katiba Mpya, 2011’ ili kuonyesha dhahiri nia ya wananchi (kwamba wanataka Katiba mpya, siyo marekebisho yake) katika mchakato mzima;
3. Kuhusu maelezo ya awali la Muswada: Chama kinapendekeza kwamba tamko la awali lirekebishwe na lioneshe wazi madhumuni: MUSWADA wa Sheria itakayoweka mfumo wa kutunga/kuweka Katiba mpya inayokidhi vigezo vinavyokubalika kimataifa vya demokrasia na utawala bora’; 
4. Kuhusu ukomo wa Katiba na utungaji wa rasimu ya Katiba mpya: Chama kinatoa tahadhari kwamba Katiba ya sasa haisemi lolote kuhusu ukomo wa Katiba na utungaji wa katiba mpya; kwa mujibu wa Ibara ya 98, ni utaratibu pekee unaotajwa wa kufanya marekebisho. 
Kutokuwepo kwa vipengele vya suala hili kutafanya michakato yoyote ya kuunda Katiba mpya kuwa batili.


Hivyo basi kama jambo la lazima, Chama kinapendekeza kwa dhati yafanywe marekebisho ya Katiba, kuwekwe vipengele vitakavyoruhusu utaratibu wa ukomo wa Katiba iliyopo na utungaji wa Katiba mpya. 
5. Kuhusu kifungu cha 5 cha Muswada - Uundwaji wa Tume: Chama kinashauri kwa dhati kwamba Tume iundwe moja kwa moja na Sheria hii. Lugha inayotumika katika Muswada inakasimu kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania mamlaka ya kuunda Tume ambapo Rais atakuwa na uhuru wa utendaji. Aidha Rais analazimika kuunda Tume hiyo baada ya tarehe 1 Juni 2011 (tarehe ambapo sheria hii itaanza kutumika), lakini hakuna kikomo kinachotajwa cha jukumu hili.
Ili kurekebisha kasoro hizi, kifungu hiki kisomeke, “Tume ya Katiba inaundwa kwa Sheria hii.”
6. Kuhusu kifungu cha 6 cha Muswada - Uteuzi wa wajumbe wa Tume: Chama kinatoa maoni na mapendekezo yafuatayo: 
  • Uwakilishi katika Tume: Muswada unapendekeza Tume iwe na uwakilishi wa Tanzania Bara na Visiwani kwa idadi sawa. Lakini kifungu hiki hakizingatii hata kidogo tofauti ya ukubwa wa idadi ya watu na kwamba Katiba ya Muungano inahusika na Zanzibar pale tu masuala ya Muungano yanapotajwa. Hivyo basi, ili kuhakikisha kuna uwiano stahikikatika Tume (yaani unaozingatia sura halisi ya mambo), idadi ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na kutoka Visiwani izingatie idadi ya watu.
  • Muundo wa Tume: Tume iwe Jopo la Wataalamu watakaoteuliwa kutoka mchanganyiko wa kada za taaluma, mashirika na jumuiya mbalimbali kwa kuzingatia jinsia, dini na ngazi za utaalamu. Aidha kif. 6(2)(e) kinampa Rais mamlaka ya kuteua kwa hiari yake wajumbe wa Tume wasiokuwa katika makundi ya watu waliotajwa katika fasili (a) hadi (d)- jambo ambalo linaweka mwanya wa matumizi mabaya ya madaraka.
7. Kuhusu Kifungu cha 8 cha Muswada - Hadidu za Rejea (kwa kifupi “hadidu”) za Tume: Kwa ajili ya uwazi na uwajibikaji, Chama kinapendekeza kwamba hadidu ziandikwe na chombo huru na ziidhinishwe na Bunge la Tanzania, badala ya Rais.
8. Kuhusu Kifungu cha 14 cha Muswada – Gharama za Tume: Muswada unadhihirisha dhamira ya Serikali kwamba matumizi ya Tume yatalipwa kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali. Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba kuwe na mfumo wazi, bayana na wa uwajibikaji katika kuidhinisha na kutoa taarifa za matumizi.
9. Kuhusu Kifungu cha 16 cha Muswada – Kutoa taarifa kwa Rais: Ili pawe na mfumo wazi na bayana, Chama kinapendekeza kwamba Taarifa ya Tume iweze kupatikana kwa umma, yaani wananchi waione na waruhusiwe kutoa maoni yao juu yake, hata kama taarifa inapelekwa kwa Rais.
10. Utekelezaji: Ili kuhakikisha kwamba Watanzania hawaachwi nje ya mchakato huu, Chama kinapendekeza kwa msisitizo kwamba shughuli ya Tume – kwa mtizamo wa kawaida – zifanyike mikoa yote 26 ya Tanzania, na siyo katika baadhi tu ya mikoa, kama msimamo ulivyojitokeza kwenye mijadala bayana iliyoendeshwa na Kamati ya Bunge.

11. Kuhusu vipengele visivyoruhusiwa kuguswa – Kifungu cha 9 (2) na 20 (1):
 
Muswada unafanya vipengele vya msingi vinavyohusu ibara za msingi za Katiba visiguswe. Kwa mfano, kif. 9 (2) kinataka mambo ya Muungano na suala la ofisi ya Rais, mambo yote mawili ambayo yaliyowekwa na Katiba, yasiguswe. Kif. 20 (1) kinakinzana na Ibara 26(2) ya Katiba ambayo inalinda haki ya mwananchi kupinga uhalali wa kikatiba wa sheria za nchi. Kuviacha vifungu vibaki pia ni kukiuka utekelezaji wa Utawala wa Sheria.
12. Kuhusu kasoro za uchapishaji zimebainika, lazima ziepukwe kwa uangalifu: Usahihi wa Muswada unategemea uandishi na rejea sahihi. Kwa mfano, kif. 19 kinatakiwa kurejea kif. 18 na siyo kif.19; na kif. 20 (3) kirejee kif. 20(2) na siyo kif. 20 (1). Athari ya hili la pili, kwa mfano, ni kumtwika tuhuma ya jinai mtu yeyote anayeamua kufungua shauri mahakamani kupinga Sheria hii – jambo ambalo ni kinyume na Katiba, na ni ukiukwaji wa haki na wajibu wa msingi.

13. Kuhusu Kifungu cha 21 cha Muswada - Kutangazwa Baraza la Kutunga Katiba: Muswada unatamka kwamba Rais ana mamlaka ya kuunda Baraza la Kutunga Katiba na kwamba anaweza kutamka Bunge lijigeuze kuwa Baraza la Kutunga Katiba.
 
Chama kinapendekeza kwamba Rais asiwe na mamlaka ya kuligeuza Bunge kuwa Baraza la Kutunga Katiba, na kwamba muundo wa Baraza uamuliwe na wananchi watakaoteuliwa kutoka kada mbalimbali (yaani taaluma na uzoefu, mashirika, taasisi za kidini na makundi mbalimbali).
14. Kuhusu Kifungu 26 cha Muswada – Kusimamia kura ya maoni (referendum): Inaonekana kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi si mahala pake kuratibu suala la uhalalishaji wa Katiba. Chama kinapendekeza kwamba taasisi za jamii, vyama vya siasa na watu binafsi na makundi mengine waruhusiwe kushiriki kwa uhuru uelimishaji wa umma kuhusu upigaji wa kura ya maoni.
Hatimaye Tume ya Katiba idhibiti uenendeshaji wa upigaji kura ya maoni.
15. Kuhusu sehemu ya VI – Uhalalishaji wa Katiba: Chama kinapendekeza kwamba mchakato wa uhalalishaji uendeshwe na Tume, siyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa kuwa imeundwa na Katiba.
Mpango wa Chama wa Hitimisho:

a) Chama kinashauri kwa dhati kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, aiondoe Hati ya Dharura iliyoambatanishwa na Muswada uliowasilishwa Bungeni. Kwa ushauri wa Chama Muswada ufuate utaratibu wa kawaida ili Wabunge na umma wote upate fursa ya kutosha kujadili na kutoa maoni kuhusu Muswada.
 
Hali halisi, Halmashauri ya Chama cha Wanasheria kimeamua kumtembelea Mtukufu Rais ili kumfikishia yeye binafsi ujumbe huu.

b) Chama kinaisihi Serikali isitafute kugundua upya gurudumu katika mchakato huu – kwa kadiri inavyowezekana, Serikali ijifunze kutoka uzoefu wa nchi nyingine, kama vile Kenya na Uganda.
 

c) Chama chetu kiko mbioni kuunda Kamati ya Katiba, ambayo- pamoja na mambo mengine- itaishauri Halmashauri yetu juu ya maendeleo ya mchakato unaoendeshwa na Serikali, itatoa msaada wa kitaalamu na utatoa mapendekezo stahiki kwa Halmashauri yetu, umma na vyombo vinavyohusika na mchakato wa kutunga Katiba.
 
Kama hapana budi, Halmashauri ya Chama itapanua majukumu ya Kamati hii ili iweze kuwa msemaji kwa niaba yake kuhusu mijadala, ambayo yaweza kuhitaji hatua zaidi.
Imewakilishwa kwa niaba ya Chama cha Mawakili Tanzania Bara
Francis K. Stolla
RAIS

CHADEMA: SUMAYE SIYO FISADI, HATUKUMTAJA KWENYE KATIKA LIST OF SHAME

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimetoa ufafanuzi juu ya orodha mpya ya ufisadi na mafisadi nchini, iliyosomwa juzi Mjini Tabora na Katibu Mkuu wa
chama hicho, ikiwa ni mwendelezo wa ile iliyotolewa mwaka 2007, Mwembeyanga, Dar es Salaam.

CHADEMA kimelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya taarifa ya baadhi ya vyombo vya habari jana kumnukuu Dkt. Slaa akisema kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Bw. Fredrick Sumaye ni mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi nchini, kwa mujibu katika orodha hiyo mpya.

TANZANIA NI NCHI TAJIRI INAYOONGOZWA NA WAPORAJI

HIVI HAPA HAWAKUMPA KA-PHD?

HUY MWANAFUNZI WA IFM NA WQENZAKE WANAHIJI KIKOMBE CHA BABU

Kwa nini dada zetu mnapenda picha za utupu? kwa kisingizio cha uhuru wa binadamu

HAYA NDIYO MAANDALIZI YA TAIFA LA KESHO


Hii ndiyo shule ya Karne ya 21.


PINDA AAGIZA UCHUNGUZI DHIDI YA MURO

SERIKALI imeagiza kufanyika uchunguzi wa kina dhidi ya tuhuma zinazomkabili Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro. Agizo hilo lilitolewa bungeni jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa hapo, akisema serikali itahakikisha hatua zote za uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo zinafuatwa na kulifanya liishe haraka. Waziri Mkuu alisema tukio hilo limekuwa  likiendeshwa katika hali ya tofauti kutokana na mtuhumiwa na vyombo vya dola kukimbilia kwenye vyombo vya habari kulizungumzia. Alisema hali hiyo inaweza kuleta hisia tofauti kwa jamii, hivyo kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndan.

Monday, April 25, 2011

Kiwanda cha kutengeneza samani.

YALIOJIFICHA NDANI YA GEREZA LA TIHAR LILILOPO KUSINI MWA ASIA




 Tihar Prisons, ambayo pia hujulikana kana Tihar Ashram, ni gereza kubwa Asia kusini. Lipo katika kijiji cha Tihar takribani kilomita 7 kutoka Chanakya Puri, magharibi mwa New Delhi, India. Inazungukwa na Hari Nagar.

 Gereza linatunzwa na taasisi ya marekebisho . dhumuni lake ni kubadili tabia za wafungwa kuwa raia wa kawaida katika jamii kwa kuwapa ujuzi, elimu na kufuata taratibu maalum. Bidhaa zote zinazotengenezwa ndani ya gereza hili hupewa jina la Tihar.

NICKI MINAJ NA RIHANA KUFANYA VIDEO YA WIMBO WA "FLY" PAMOJA

Wasanii maarufu katika tasnia ya muziki nchini Marekani Rihanna na Nicki Minajkufanya video kwa ajili ya track ya “Fly.”
Akizungumza na vyombo vya habari nchini Marekani Nicki alisema kuwa wanatengeneza video hiyo yeye pamoja na Rihanna weekend hii na kwamba watautumikia ulimwengu kwa njia nyingi tu na sii hiyo video watakayoitengeneza.
Minaj alikiri kuwa Rihanna ni Mwanamuziki wa kike ambaye anamfeel.
Nicki alisema kuwa angependa kushirikiana na wanamuziki wengine wa muziki mbalimbali  na kwamba huwa hasikilizi muziki wa aina moja tu na angependa watu wote wangesikiliza hivyo kama yeye.  “ninasikiliza miziki ya kila aina, ninasikiliza sana miziki ya injili” alisema Minaj.

UNAFAHAMU MAVAZI YA KUVAA NIGHT CLUB?

Kupendelea kutoka nyakati za usiku hasa siku za weekend ni njia moja wapo ya kupata good tym, kukutana na watu wapya na ku-hang out na marafiki. Watu wengi hupendelea hasa kwenda katika kumbi za starehe (night clubs). Si tu kwa kuwa unahitaji kuwa na marafiki bali pia kusikiliza muziki kwa sauti kubwa na kucheza kadiri moyo wao utakavyo. Hata hivyo, kwenda katika nyt clubs huzingatia uvaaji wa mavazi.

SIKIA NDOTO ZA MAPACHA HAWA WA NIGERIA


MAPACHA wanaotamba kwenye filamu za Nigeria, Chidinma na Chidiebere Aneke wanatamani kuolewa na wanaume mapacha na wazae mapacha kama wao. Wasanii hao wa kike wamesema:  'Tunatamani tukiolewa tuzae mapacha wa aina mbili, wawili wa kike na wawili wa kiume na tuishi kwa amani na waume zetu. Tunatamani pia kuolewa siku moja wote wawili, na ikiwezekana na wanaume ambao ni mapacha kama sisi. Lakini tuna imani Mungu atatuchagulia wanaume wanaotufaa. Hatutaki sana kujadili maisha yetu binafsi lakini kifupi ni kwamba tunaishi kwa raha sana na mambo mengine ni siri sana hatuwezi kuyasema'.

MHHHH!!!! USHER RAYMOND NA RIHANA WAZUA TETESI ZA KUA MWILI MMOJA


Usher Raymond

KUNA dalili za uhusiano wa kimapenzi kati ya wanamuziki Usher Raymond na Rihanna.

Ishara zilijionyesha wakati wa sherehe iliyoandaliwa na kampuni ya mavazi ya Armani huko Coachella, California.

Jarida la OK! linaripoti kuwa Usher aliomba kuandaliwa meza ya kukaa na Rihanna.

�Usher aliomba mapema kuandaliwa meza ya kukaa karibu na Rihanna,� mtu mmoja alikaririwa na jarida la OK!

�Rihanna ndiye alitangulia kwenye eneo la tukio akiwa na walinzi wake na kufuatiwa na Usher.�

Watu hao wawili inasemekana walikuwa bize wakicheza pamoja usiku wote wa shughuli.

Rafiki yao mmoja wa karibu amedai kuwa watu hao wamekuwa karibu katika siku za karibuni.

UNATAKA KUA NA NGOZI NYORORO YENYE KUWAKA? NISIKILIZE MIMI


KILA mtu anapenda kuwa na ngozi laini na ya kuvutia, kuna wengine wanafanikiwa kuwa na ngozi hizo lakini wengine wanashindwa kuwa na ngozi laini kama ya mtoto kutokana na kukosea baadhi ya mambo.

Makala ya leo inachambua hatua muhimu za kuhakikisha unakuwa na ngozi laini wakati wote.

Kitu cha kwanza cha kuzingatia ni kuhakikisha unanawa uso wako mara tatu kwa siku, hiyo itasaidia kutoa uchafu ambao unaweza kung'ang'ania na kufanya uso usiwe na mng'ao wa asili na husaidia kuzuia chunusi.

Kitu kingine ni kuhakikisha unanawa uso kwa sabuni ambayo inakwenda sawa na ngozi yako, kama ngozi yako ni ya mafuta hakikisha unatumia sabuni ambayo itakuacha ukiwa mkavu na kama ngozi yako ina ukavu, jioshe na sabuni itakayokufanya uwe na unyevu kiasi (sabuni hizo zinapatikana kwenye maduka ya vipodozi).

Vile vile mhusika anatakiwa kuwa na krimu mbili, yaani ile inayopaswa kupaka mchana na ya usiku. Ikumbukwe kuwa wakati wa usiku ngozi inatakiwa kupakwa krimu laini zaidi kuliko mchana.

Mhusika pia anatakiwa kusugua ngozi yake au kufanya 'scrub' mara mbili mpaka tatu kwa wiki, hiyo itasaidia kutoa uchafu ambao unaweza kujificha katika vinyweleo. Sasa basi kwa mfano mimi mwenyewe Binafsi nina masharti yangu ya kila siku ili kuiweka vizuri ngozi yangu na ndio maana wengi wakikutana LIVE na mimi wananiuliza 'Oooh BEN unatumia nini kwenye ngozi yako? Sasa kwa mfano mimi, kila nikiamka asubuhi lazma ninywe maji glass 2 kabla ya kupiga 'MSWAKI' na mara nyingi mie sinywagi 'CHAI' ila nahakikisha saa 4 ivi napata Juice au 'FRUITS' mchanganyiko tena 'ORIGINO' na sio ya BOX huku mwili wako ukiusindikizia na maji ya kunwa kila baada ya muda flani na pia yakupasa ujue una Ngozi ya aina gani ili utumie 'LOTION' au 'CREAM' ya aina gani yatakayokufaa zaidi mwilini. Alafu hakikisha kila mara unafanya mazoezi na mwili utoke JASHO jingi ili ngozi itoe uchafu kwenye 'VITUNDU! Na pia hakikisha kabla hujalala unakunywa tena Glass 2 za maji na pia ni marufuku kulala na 'MAKE UP' usoni na endapo utaaamka usiku kwenda 'MSALANI' kunywa tena 2, fululiza ivyo kwa wiki 2 utanipa majibu mwenyewe! Mimi ni mtaalamu wa ngozi maana nilishapitiaga 'KOZI' iyo ya wiki 2 iliyoandaliwa na kampuni ya 'VENUS' kwaiyo nina uwezo wa kukuangalia tu alafu ninakushauri utumie Vipodozi gani ili Ngozi yako iwe 'BOMBA' hata kama una 'MAPELE' kibao, TRUST ME!

KAZI NI KAZI.......


Moshi Hemba Mfaume

WASWAHILI husema, ‘kazi ni kazi, bora mkono uende kinywani’, hivi ndivyo ilivyo kwa Moshi Hemba Mfaume ambaye kwa miaka 32 amekuwa akichinja ng’ombe katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Ni kazi ambayo kwa jumla inawezekana imemwezesha kuwachinja ng’ombe 1,152,000 kwa muda wote wa kazi yake ile.

“Naipenda sana kazi yangu kwa kuwa ndio ambayo imenifanya nifike hapa nilipo kwa kuniwezesha kupata maendeleo yangu na familia yangu, japo sikuwahi kuwaza kama ningekuwa mchinjaji katika maisha yangu, lakini namshukuru mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuipata.”

Hiyo ni kauli yake mzee huyu mwenye umri wa miaka 61, mkazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam ambaye anakiri kuwa yeye ni mchinjaji mkongwe wa ng’ombe katika machinjio hayo ya serikali.

Hemba ambaye anasema kuwa ni mzaliwa wa Kisarawe, Pwani alipata elimu ya msingi katika Shule ya Kisarawe miaka ya ‘50 ambapo alishindwa kuendelea na masomo ya darasa la tano baada ya matokeo ya darasa la nne kutokuwa mazuri.

Anasema kuwa alianza kufanya biashara ya kuuza karanga, muhogo na bidhaa mbalimbali sokoni lengo lake likiwa ni kujikimu kwa kipato, jambo ambalo lilimsaidia kufanikiwa kuendesha maisha yake ya kila siku.

Kutokana na uwezo wake mkubwa katika kucheza soka, Hemba anasema kuwa mwaka 1972 alipata ajira katika karakana ya iliyokuwa Idara ya Ujenzi, Mawasiliano na Barabara (sasa Wizara ya Ujenzi) ambako alikuwa akifanya kazi ya ufundi wa kutengeneza magari ambayo aliifanya kwa takribani miaka minne.

Anasema kuwa akiwa katika karakana hiyo alikuwa akilipwa mshahara wa Sh240 kwa mwezi, kiasi ambacho anakiri kuwa kwa wakati huo kilitosha kwa mahitaji yake ya kila siku.


“Nilipata faraja sana baada ya kupata kazi katika karakana hiyo na niliongeza bidii katika soka kwa kuwa hicho ndicho kilikuwa kigezo cha kupata ajira mahala hapo.

“Kwa bahati mbaya, mwaka 1976 timu yetu ya Ujenzi ilivunjwa na hivyo kunikosesha kazi nikaondoka na kwenda kiwanda cha nguo cha Kilitex cha mjini Arusha ambako hata hivyo sikukaa kwa muda mrefu na hatimaye nikarejea Dar es Salaam,” anasimulia.

Anasema kuwa aliporejea Dar es Salaam alijiunga na kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill kilichoko Tegeta ambapo alikuwa akifanya kazi ya kukusanya saruji iliyomwagika, kazi za usafi na nyinginezo ambapo hata hivyo hakudumu nazo sana kwani aliamua kuachana na kazi hiyo na kutafuta kazi nyingine.

Anasema mwaka 1977 alilazimika kufanya kazi kwa kujitolea katika machinjio ya Vingunguti baada ya kuona maisha yanazidi kuwa magumu na alijitolea kwa kazi hiyo akipiga deki na kufanya usafi mwingine.

“Nilijitolea kwa miaka miwili katika machinjio haya wakati huo yakiwa chini ya Mwarabu aitwaye Salehe Dahari kabla ya serikali kuchukua vitega uchumi vyake mwaka 1979, kazi ilikuwa ngumu sana kama unavyojua kazi za watu wasio na elimu kubwa zina mateso yake,” anasema na kuongeza:

“Sikukata tamaa na nilijitolea kwa miaka miwili huku nikipata posho kidogo tu ambayo ndo ilinisukuma katika masiha yangu, lakini niliamini siku moja nitafanikiwa na maisha yangu yatakuwa mazuri kwa kuwa niliweka nia na kuipenda kazi yangu”

Hemba anasema kuwa mnamo mwaka 1979 baada ya serikali kuchukua vitegauchumi vyake ikiwamo machinjio hayo ya Vingunguti, yeye alifanikiwa kuwekwa katika ajira hasa kutokana na viongozi wake kubaini uwezo na uadilifu wake kazini.

Anasema kuwa aliwaheshimu sana wakuu wake wa kazi jambo ambalo hadi leo analifanya kwa kuwa alijua ni watu muhimu katika kufikia malengo yake katika maisha na kwamba ndio ambao walikuwa wakimshauri kwa mambo mbalimbali.

“Nilifurahi sana nilipopata kazi ya kuajiriwa kwa kuwa hicho ndicho kitu nilichokuwa nikikililia kwa siku nyingi, niliahidi kuendelea kuwa mwadilifu kazini kwa kuwaheshimu na kuwatii wakuu wangu wa kazi na kufuata sheria za kazi, hiyo ndio siri ya mafanikio yangu,” anasema

Anasema kuwa kazi ya kuchinja aliianza rasmi mwaka 1979 ambapo kwa kupewa mwongozo mzuri na Iddi Kondo Sewando alipata ujasiri wa kufanya kazi hiyo ya kuchinja ng’ombe kiasi ambacho aliwakuna watu wengi machinjioni hapo.

Anasema kuwa siku ya kwanza alipata tabu kidogo kwa kuwa alikuwa akikiona kitendo hicho cha kuchinja katika mawazo yake siku nzima na kumfanya ashtuke mara kwa mara kutokana na hisia hizo ambazo baada ya kuzoea kazi ziliondoka zenyewe kichwani mwake.

“Kama unavyojua ng’ombe ni kiumbe hai kwa hiyo unapomchinja hushtuka, siku ya kwanza hata mimi mwili ulisisimka, nilishtuka tena niliogopa, lakini kwa kuwa nilitaka kuwa na utendaji bora katika kazi yangu niliongeza ujasiri na hatimaye kuizoea kazi hiyo,” anasema

Anaongeza kuwa baaadye alibobea katika kazi hiyo na kwamba sasa anachinja ng’ombe kati ya 100 hadi 150 kwa usiku mmoja jambo ambalo kwake limekuwa ni la kawaida.

“Kila siku nachinja ng’ombe kati ya 100 hadi 150 na nimeizoea kazi hii sasa najua mbinu nyingi tu za kumchinja ng’ombe tena bila usumbufu na hivyo sio kitu cha kutisha tena kwangu,” anasema

Anasema kuwa alijawa na furaha ya ajabu baada ya kupata mshahara wake wa kwanza akiwa machinjioni hapo ambao ulikuwa ni Sh 380, pesa ambayo alikuwa hajawahi kuipata kama mshahara na hivyo pesa ilimwongezea bidii katika kazi yake hiyo.

Anasema anaipenda sana kazi yake ya uchinjaji kwa kuwa imemletea tija tofauti na kazi alizokuwa akizifanya kipindi cha nyuma na kwamba hali hiyo imemwezesha kujijenga kimaisha na kununua mahitaji muhimu ya familia.

Anasema kuwa kazi hiyo imemwezesha kujenga nyumba ya kuishi iliyoko Buguruni na kuwasomesha watoto wake wanne hadi kufikia kiwango cha elimu ya sekondari na vyuo, ambapo watoto wake wawili ni madereva wa magari wakati, mmoja mwalimu na mwingine ni nesi.

Anasema kuwa uadilifu wake kazini umemjengea heshima kubwa miongoni mwa wafanyakazi wenzake na wakuu wake wa kazi ikiwa ni pamoja na ndugu, jamaa na marafiki ambao wamekuwa wakimpongeza kwa kazi yake hiyo.

“Naishukuru familia na ndugu zangu kwa kuniunga mkono kwa kazi yangu hakuna aliyeonyesha kutoikubali pamoja na kwamba watu wengi wanaiona ni kazi ngumu na inayotia kinyaa lakini ndugu zangu wananipa faraja kwa kuwa wako nyuma yangu wakinipa nguvu ya kusonga mbele katika maisha” anasema

Anasema kuwa changamoto ambazo zinamkabili katika kazi yake ni pamoja na kupata shida ya macho kuona kutokana na madhara yanayotokana na kuona maji ya mimba ya za ng’ombe ambayo yanaathari kubwa katika macho.

Anasema pamoja na kutumia miwani maalumu ya macho lakini bado tatizo hilo ni kikwazo kwake kwa kuwa limemuathiri kwa kiasi kikubwa japo bado yupo imara katika kufanya kazi yake hiyo ya uchinjaji.

Aidha, anasema kuwa changamoto nyingine ni suala la kutopata usingizi wa kutosha hasa kwa kuwa kazi yao huwataka kuifanya kuanzia saa tano usiku hadi saa kumi za alfajiri na wakati mwingine kujikuta wakiendelea kufanya kazi za nyumbani wakati wa mchana.

Anasema zamani wakati akiishi katika nyumba za kupanga majirani zake walibaki na maswali na wengine kumhisi vibaya kuwa labda ni mwizi hasa kutokana na kufanya kazi usiku na mchana kulala huku familia yake ikikaangiza nyama kila siku.

“Changamoto nyingi ni za kawaida tu, lakini hili la madhara ya maji ya mamba za ng’ombe ndilo kubwa zaidi na inahitaji umakini zaidi vinginevyo unaweza kuishia kuwa kipofu hapo baadaye,” anasema

Hata hivyo, Hemba anawashauri vijana kujishughulisha na kuacha kusubiri kupata kazi kirahisi kama ambayo vijana wengi wamekuwa wakidhania na kukaa vijiweni kusubiri kupata kazi rahisirahisi na zenye mshahara mkubwa.

Anasema kuwa wakati anaanza yeye kazi alijitolea kwa miaka miwili na baadae kuajiriwa jamno ambalo hata vijana wa leo wanapaswa kuliiga kwa kuwa subira huvuta heri na huonyesha ukomavu na nia ya kazi husika.

“Vijana wanapaswa kutambua kuwa huu sio wakati wa kuzembea kusubiri kazi rahisi rahisi tena zenye mshahara mkubwa, mimi nilianza kuuza karanga, kufanya kazi kwenya mashirika kama kibarua na hatimaye sasa niko hapa machinjioni ni matunda ya uvumilivu wangu” anasema Hemba

Aidha Hemba anawashauri vijana ambao watapenda kufanya kazi ya uchinjaji wanaweza kufika katika machinjio hayo kwa kuwa kuna mafunzo mbalimbali huwa yanatolewa kwa vijana kwa ajili ya kuandaa wachinjaji wa kizazi kijacho.

“Baada ya kuifanya kazi hii kwa miaka 32 ninatarajia kustaafu kazi hii mwakani, kwa hiyo ni vizuri kupata vijana ambao wataendeleza fani hii na kuna mafunzo mengi yamekuwa yakiendeshwa na asasi mbalimbali za kiraia juu ya namna ya kuchinja kwa ubora zaidi kwa hiyo vijana wasisite kujitokeza ili kujifunza,” anamalizia.

SHIKAMOO BABU.

Mtoto Colins Mustafa, akimsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye tamasha la pasaka lilofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

KIBONGO BONGO HII IMEKAAJE?

  • Waandishi Habari wawili waliokuwa wamekamatwa nchini Uganda kutokana na kibonzo kilichochapishwa katika jarida lao wameachiliwa kwa dhamana, lakini wameamriwa kuripoti katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi, CID, ili kujieleza. Walifika huko siku ya Alhamisi lakini wamesema hakuna walichoambiwa bali kuamriwa kurudi tena siku ya Ijumaa.
  • Mhariri wa jarida la kila mwezi Summit Business Review, Mustapha Mugisa pamoja na mchapishaji wake Dk Samuel Sejjaka, inadaiwa walikuwa na nia ya kumkejeli kiongozi wa taifa.
  • Walikamatwa mapema wiki hii, na wakili wao, Murungi Godwin, alisema wateja wake wamekuwa wakiripoti katika kituo cha polisi, pasipo kuchelewa, na kilichofanyika Alhamisi, ni kama kuwaongezea dhamana.
  • "Waliachiliwa kwa dhamana, na kutakikana kuripoti jana, na tulipofika hapo, afisa aliyekuwa anasimamia kesi hiyo, alitueleza turipoti tena leo", alielezea Murungi.
  • Mhariri wa jarida hilo ambalo huchapishwa kwa Kiingereza, Mustapha Mugisa, alisema askari wapatao kumi waliingia afisini mwake, na kumuuliza ikiwa yeye ndiye mhariri wa jarida hilo, na alipothibitisha hayo, walimuelezea lilikuwa na kibonzo, na ilielekea jarida lilikuwa na nia mbaya ya kisiasa, na hivyo wakamkamata.

Saturday, April 23, 2011

KWELI YESU KRISTU ALITESEKA

Vijana wa Kanisa laKiinjili la Kilutheri Tanzani (KKKT) usharika wa Azaniac Frontmjini Dar es Salaam, wakiigiza sehemu ya mateso ya Yesu Kristu wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kanisani hapo.

Friday, April 22, 2011

MMMH HII NAYO IMEKAAJE JAMANI...


CHADEMA: Tutahoji utajiri wa Ridhiwan.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willbroad Slaa amesema chama chake kinajipanga kuhoji kile alichodai utajiri mkubwa wa ghafla wa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji na pia Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Dk Slaa alisema hayo jana katika Kijiji cha Ikungi, mkoani Singida alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara. Alisema anajua kuwa mjumbe huyo (jina tunalihifadhi kwa kuwa jitihada za kumpata kujibu tuhuma hizo hazikufanikiwa), licha ya umri wake mdogo hivi sasa ana fedha nyingi. Katika mkutano huo Dk Slaa alimtuhumu kuwa na utajiri uliopindukia ambao alisema haulingani na umri wake. Dk Slaa alisema chama chake kina shaka na wingi wa fedha alizonazo kijana huyo na kwamba atahakikisha kwamba kigogo huyo anaiambia Chadema na Watanzania alipozipata. Alisema kijana huyo alimaliza masomo yake muda mfupi uliopita, lakini tayari amekuwa bilionea akisisitiza kuwa chama chake kitahoji alipopata mabilioni hayo. "Ninajua kwamba ana fedha nyingi, lakini huyu alikuwa mtoto wa shule juzi tu. Leo amekuwa bilionea! Atatuambia amepata wapi hizo fedha, Chadema tutahoji ni wapi amezipata," alisema Dk Slaa. Dk Slaa pia alizungumzia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa kelele za wapinzani hazimnyimi usingizi na kusema watahakikisha halali. Mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alitoa kauli hiyo alipozungumzia ushindi wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akisema umeimarisha ngome ya upinzani bungeni. "Rais Kikwete alisema kelele za upinzani hazimnyimi usingizi, lakini kwa kumchagua Lissu mmeongeza nguvu ya upinzani na sasa hatalala," alisema na kuongeza: “Ujumbe wangu kwenu ni kwamba sasa mmemchagua mbunge jasiri anayeweza kumwambia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mbele ya Waziri Mkuu kuwa amekuwa mvivu kusoma.” Alisema kutokana na ujasiri huo wa Lissu sasa miswada mibovu haitapelekwa bungeni. Awali, akizungumza katika mkutano huo, Lissu alisema Halmashauri ya Wilaya ya Singida imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo akisema kuwa ni mara ya kwanza fedha hizo kutengwa huku akijigamba kwamba ni kutokana na wapinzani kubana mianya ya wizi.

NAONA KAMA VILE MANENO YA MZEE MSEKWA YANA UKWELI FLANI IVI...


Msekwa: Yafaa spika kuwa mwanasheria, Spika Makinda asema si lazima!




MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa amesema ni vigumu kwa mtu asiye na taaluma ya sheria kuliongoza Bunge akiwa Spika.Msekwa ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 2000 hadi 2005, aliyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), hivi karibuni akizungumzia utendaji wake akiwa na wadhifa huo. Pia alizungumzia miaka 50 ya Uhuru.

Katika mahojiano hayo, Msekwa alisema alilazimika kurudi shule, kusomea shahada ya sheria ili aweze kuliendesha vyema Bunge.

Kauli hiyo ya Msekwa imekuja wakati Bunge la sasa likishuhudia mivutano ya kisheria baina ya wabunge na Spika wa Bunge hilo la 10, Anne Makinda.

Katika mkutano wa tatu wa Bunge hilo uliomalizika Jumamosi ya wiki iliyopita, Mbunge wa Singida Kusini (Chadema), Tundu Lissu ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba alionekana kuipa wakati mgumu Serikali alipokuwa akipinga kifungu cha sheria kinachowaruhusu wanasiasa kuingilia uhuru wa mahakama.

Katika mvutano huo ambao pia ulimhusisha, Spika Makinda, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alimuunga mkono Lissu licha ya muswada huo kupitishwa.

Katika Bunge la 10 pia kumekuwepo malumbano yanayoashiria wabunge wengi kutozijua vyema Kanuni za Bunge na sheria mbalimbali hivyo kujikuta wakivutana wao kwa wao, wakati mwingine na Spika Makinda.

Hata hivyo, baadaye akizungumza na Mwananchi, Msekwa alirejea kauli hiyo akisema: "Bunge ni la kutunga sheria, kwa hiyo ni muhimu kwa Spika kuwa na taaluma ya sheria."

“Ni kweli walinihoji TBC, ilikuwa ni kuhusu miaka 50 ya Uhuru. Ndiyo lile ni Bunge la kutunga sheria, kwa hiyo ni muhimu kwa Spika kuwa na taaluma ya sheria.”

Msekwa ambaye aliwahi pia kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1962-1970, Katibu Msaidizi wa Bunge kati ya mwaka 1960-1962 na Spika wa Bunge kati ya mwaka 2000-2005 alisema suala la Spika kusoma sheria ni la uamuzi binafsi siyo lazima.

“Huwezi kulilinganisha Bunge la wakati wangu na Bunge la sasa. Ni kweli kazi za Bunge ni zilezile, lakini wabunge wa sasa ni wengine. Siyo lazima kwa Spika kusoma sheria, ni uamuzi wa mtu binafsi," alisema na kufafanua:

"Adam Sapi Mkwawa hakuwa mwanasheria, Chifu Mang’enya hakuwa mwanasheria. Hata mimi nilipoanza sikuwa mwanasheria, lakini baadaye niliona umuhimu wa kusoma sheria.”

Bunge aliloongoza Msekwa lilishuhudia mawaziri wakilazimika kujiuzulu kutokana na kashfa. Hao ni pamoja na Profesa Simon Mbilinyi, Dk Juma Ngasongwa na baadaye Idi Simba wote hao kutokana na nguvu ya Bunge.
Akizungumzia kauli hiyo ya Msemwa, Spika Makinda licha ya kukiri kutosomea sheria moja kwa moja, alisema uzoefu alioupata Bungeni tangu alipotoka shule ndiyo unaomwezesha kuliendesha kwa ufanisi.

“Nimekulia na kuzeekea bungeni, taaluma yangu ni uhasibu, lakini mimi ni kati ya wabunge wakongwe. Tangu nimetoka shule niko bungeni,” alisema.

Alipoulizwa iwapo ana mpango wa kusomea sheria ili kumudu vyema zaidi uendeshaji wa Bunge, Makinda alisema kuwa amesomea sheria katika taaluma yake ya uhasibu ambayo inamsaidia pia kuzielewa Kanuni za Bunge.

“Kwani mimi sijasoma sheria? Mimi ni ‘accountant by professional’, (mhasibu kitaaluma) na huko nimesomea sheria. Ni kweli sina ‘bachelor’ (shahada) ya sheria, lakini, nina uelewa wa sheria," alisema.
Makinda alijigamba: " Nimekuwa mbunge, 'chief whip' (mnadhimu) kwa muda wa miaka minane, nimekuwa mwenyekiti wa Bunge, yote hayo yamenipa uwezo.”

Kuhusu changamoto anazokabiliana nazo katika nafasi hiyo, Spika Makinda alisema kuwa hilo jambo la kawaida kwake, lakini akasema tatizo na jambo kubwa ni wabunge kutokuelewa kanuni.

Hata hivyo, alisema anajitahidi kuwafundisha Kanuni za Bunge ili waendane na mwenendo wake.

“Unajua kipindi hiki wabunge ndiyo wamekuja, wengi wao hawajui Kanuni za Bunge, wanafanya makosa na utundu mwingi. Lakini tutawafundisha kanuni, naamini, Bunge litakuwa ‘smart’ siku zijazo,” alisema na kuongeza:

“Kwa mfano, sasa kuna kitu kinachoitwa ‘adjoin motion’ ambapo mbunge anamtaarifu Spika pale anapokuwa akiahirisha Bunge kuwa ana hoja ya kulitaarifu Bunge, basi Mbunge anapewa dakika 15 za kujieleza. Yote hayo tutawafundisha na wengi wameshaleta maoni ya kufanya hivyo.”

Akizungumzia tukio la hivi karibuni ambalo Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje alitoa kauli iliyosababisha wabunge kurushiana maneno, Spika Makinda alisema kuwa tukio hilo lilikuwa ni kinyume cha Kanuni za Bunge.

“Kanuni zinakataza wabunge ku-shout hovyo (Kupayuka). Ile ilikuwa ni makosa. Unajua wabunge bado wanajifunza na tutafanya ‘amendments’ (marekebisho) ya kanuni ili kuwawezesha wabunge kuzoea Bunge. Kwa mfano, sasa kuna kitu kinaitwa “Committee of supply,” yaani wakati wa mbunge kutoa shilingi Bungeni. Hilo nalo tutawafundisha ili waelewe,” alisema.




Mmmh WAVIVU utawajua tu maana wengine tumesimama tunashangilia wao wamekaa haaa ahaaaa ila tunaonyesha umoja wetu, pichani kuanzia kushoto ni TINO, RAY, RICHIE RICHIE, CHIKOKA na STEVE NYERERE wakiufatilia kwa makini mchezo unavyoendelea...

STEVE NYERERE na MAINDA nao walikuwepo, na vimo vyao pia vinalingana daaah...

Nguli JAQ WOLPER akionyesha Ufundi uku SHILOLE akiwa tayari kutoa msaada...

Hayaa mechi ndio inaanza na MASANJA nae akageuka mpiga picha wa KUJITEGEMEA...

Timu zimejipanga tayari kwa ukaguzi then mechi ndio ianze...

Mawaidha lazma yawepo ili watu wafuate sheria atiii...

Mkongwe KATIE nae yupo kwenye Timu ya Bongo Movie queen 'KUWAHAMASISHA' vijana...

Hiki ndio kikosi kamili cha BONGO MOVIE QUEENS kinachojumuisha wacheza Filamu woote wa kike nchini ambacho weekend iliyopita ilifungwa kwa TAAABU na timu ya TTCL kwenye mechi kali iliyofanyika kwenye viwanja vya TTCL kijitonyama! Vijana wanazidi kuiva kimazoezi kilasiku saa moja asubuhi pale kwenye viwanja vya Leaderz Kinondoni...
Hapa wanaonekana kina MAYA, JAQ WOLPER, COLETTA na wengineo wakifanya mpango wa 'sala' kidogo kabla mechi haijaanza...
Sala ikiendelea...





Bendi ya FM ACADEMIA aka 'wazee wa ngwasuma' kama kawa walimwaga 'SEBENE' la nguvu jana Jumapili ndani ya ukumbi wa Msasani Club ulioko maeneo ya Morocco jijini Dar! Kwakweli jamaa wanajua muziki ni nini na kwenye kumwaga 'MAUNO' nadhani kila mdau wa muziki anwatambua hawa mabwana, ilikuwa 'HAATWARIII' jana! Pichani nikiwa na 'Rapa' namba moja wa Bendi hiyo KHALIJO MWANA KITOKOLOLO...

Katikati ni Rais wa Bendi hiyo ya FM NYOSHI EL SAADAT aka 'Sauti ya simba' akiwa na ROGEE MUZUNGU kulia, wakiimba kwa hisia jana...

Mkaanga 'CHIPS' akiwa kazini...

Wanenguaji nao hawakufanya AJIZI, na walileta 'Ladha' safi saanaaa...

Mwimbaji nguli PATCHO MWAMBA aka 'Tajiri' akiwa sambamba na mwimbaji mpya wa kike wa Bendi hiyo aitwae Mariam ndani ya Msasani Club jana Jumapili...

Huyu anaitwa B52, ni mpiga gita la 'Solo' mkongwe nchini ambaye kwa wale wanaomkumbuka mwanamama SAIDA KALORI alivyotamba na zile nyimbo zake kwenye Album ya 'chambua kama karanga' basi huyu bwana ndie mtunzi na mpigaji wa gita katika ile Album yooote na kumpaisha sana SAIDA KALORI, kwasasa yupo na FM ACADEMIA...

Huyu anaitwa Queen Suzy, ni mnenguaji 'HATARI' ila ni bingwa wa kuhama Bendi, na tabia hiyo imemsababishia 'uadui' mkubwa kila anakoenda na 'kibaya' zaidi huwa anatokaga FM ACADEMIA anahamia TWANGA PEPETA, alafu anaondoka TWANGA anarudi tena FM ACADEMIA looh! Sasa ameshahama mara na kurudi maranyingi sana na majuzi alitoroka TWANGA akaenda OMAN basi ile kurudi Bongo akaenda kutua FM moja kwa moja daah...

QUEEN SUZY akiwajibika Jukwaani jana Jumapili ndani ya Msasani Club...

Weeeweeeee chezeeaaaa....

Rapa namba moja wa FM ACADEMIA aka 'wazee wa ngwasuma' KALIDJO MWANA KITOKOLOLO aka 'KUKU' akirapu kwa hisia kali jana ndani ya Msasani Club maeneo ya Morocco...

Ni mwendo wa 'SHOWBIZE' tu weee...

Kwakweli madansa wa Fm Academia ni wakali sanaaa, jaribi kwenda kushuhudia uone...


HII NI HADITHI YA KWELI KWA WALE WOOOTE WANAOTAKA KWENDA LOLIONDO KWA 'BABU'...


Hii ni hadithi ya ndugu yangu mmoja aliyekwenda LOLIONDO majuzi. Anasimulia hivi, ni usiku wenye baridi kali, mvua inayoambatana na upepo inanyesha. Katika hali ya kawaida, baridi hii haivumiliki kwani nawaona kina baba wakiota moto katika jiko linalotumiwa na mama lishe.Natamani kuungana nao lakini nashindwa kwani jiko lenyewe ni dogo na idadi ya watu waliolizunguka ni kubwa. Lakini pia ugeni wangu katika eneo hilo unakuwa kikwazo cha shauku yangu ya kujiunga nao.Mbele yangu nawaona kina mama na watoto wao wengi kiasi, wakiwa wamelala barazani katika moja ya nyumba za wageni zilizopo katika eneo liitwalo Wasso.Wasso ni kitongoji maarufu katika eneo la Loliondo. Kitongoji hiki ni sehemu ya mji wa Loliondo na kwa mujibu wa wenyeji wa mji huu, Wasso ni mji mpya unaopanua ukubwa wa mji wa asili wa Loliondo.Eneo hili linachangamshwa na uwepo wa shughuli nyingi za kibiashara, nyumba za wageni na hata gulio kubwa ambalo hufanyika kila Jumamosi likiwavuta wafanyabiashara wengi kutoka nchini Kenya. Lakini usiku, halitamaniki kutokana na baridi kali.Katika baraza au kwenye veranda ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Sayi, ndipo walipolala kina mama hawa. Udadisi wangu unabaini kuwa hawa ni wenyeji wa maeneo ya Wilaya ya Ngorongoro na wako safarini kwenda Samunge kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila kunywa dawa.“Usiku umewakuta hapa hivyo lazima walale halafu kesho asubuhi na mapema, wanaamka kwenda kwa babu kunywa dawa," anasema mmoja wa wahudumu wa nyumba ya wageni aliyejitambulisha kwa jina moja la Fatma na kuongeza: “Hapa ni kawaida, tena leo wamepungua, huwa wanakuwa wengi hadi tunawatimua (kuwafukuza). ”Nilimwuliza Fatma kwamba watu hawa wanatumia usafiri gani kwenda Samunge? Jibu lake lilikuwa ni fupi tu kwamba “…..hawa wanatembea”. Umbali kutoka Wasso hadi Samunge ni karibu kilometa 70 lakini, kwa mujibu wa wenyeji, matumizi ya njia za mkato huwawezesha kupunguza umbali huo hadi kufikia kilometa zisizopungua 40.Kwa maana hiyo wenyeji wanasema hutumia muda wa kati ya saa tano hadi sita kufika Samunge na baada ya kupata kikombe cha babu huanza tena safari ya kutembea kurudi makwao. Ng’ambo ya barabara kutoka ilipo nyumba hii ya wageni ya Sayi, ipo nyumba nyingine ya kulala wageni iitwayo Selemani. Hivyo jibu la Fatma lilinipa wajibu wa kuvuka barabara ili kwenda kuona iwapo kuna watu wengine waliolala barazani.Hali niliyoikuta ni ileile. Kina mama kwa kina baba walikuwa wakihangaika kujisitiri kwa mashuka na makoti waliyokuwa nayo. Katika hali ya ubinadamu, nawahurumia lakini sina la kufanya kwani hata kama ningekuwa na fedha za kugharamia malazi yao, vyumba katika nyumba za wageni zilizopo Wasso zilikuwa zimejaa. Malazi kwa Babu Samunge Wakati fulani nikiwa Loliondo, nililazimika kulala katika Kijiji cha Samunge ambako Mchungaji Mwasapila anatoa dawa ya magonjwa sugu.Siku ya kwanza tulipoamua kwamba tutalala Samunge mimi na wenzangu, Mussa Juma na Fidelis Felix tuliazimia kutafuta sehemu ya kulala usiku ule. Wakati tukiwa katika harakati za kutafuta malazi, nilibaini kwamba watu wengi ambao wanasubiri zamu za kunywa dawa hawana mahali pa kulala. Wengi wamechukua mikeka mabusati na kuyatandika pembezoni mwa magari yao na kulala hapo. Wengine wamekuwa katika foleni, wakilala kwa ‘staili’ hii kwa muda wa siku sita au zaidi.Lakini hawa wana ahueni kwani wana uwezo wa kufanya hivyo. Kuna wengine ambao maisha yao ni magumu zaidi ya haya. Hawa wanalala kwenye magari hasa magari makubwa kama malori mengine yakiwa ni Fuso. Humo kuna watu ambao wako taabani. Hawa hawalioni jua kwani hawana uwezo wa kutoka nje. Kutwa, kucha wamo ndani ya magari yao wakisogea taratibu kuelekea kwa Mchungaji Mwasapila.Katika gari mojawapo aina ya Fuso lililokuwa likitokea mkoani Mara, kulikuwa na abiria wasiopungua 100, wakiwemo wazee, watoto na wagonjwa ambao walikuwa hawajiwezi. Lakini pamoja na adha hiyo, watu wote katika eneo hilo wanavumilia tabu hizo wakiwa na shauku kubwa ya kukutana na Mchungaji Mwasapila ili awape kikombe. Kambi za mahemaKatika kutafuta malazi, tuliingia katika eneo lenye mahema na kuanza kuulizia gharama za kukodi kwa usiku mmoja.Katika eneo la kwanza tulionyeshwa mahema ya aina tatu. Moja ni hema ambalo kulala kwa usiku mmoja gharama yake ilikuwa Sh60,000. Hema hili ni kubwa na lina magodoro mawili madogo ya shule (futi mbili na nusu kwa tano).Pia tukapelekwa kwenye hema lenye ukubwa wa kati ambalo lilikuwa na godoro moja dogo. Gharama yake ni Sh45,000.Hema la tatu lilikuwa dogo na gharama yake ni Sh35,000. Hema hilo lilikuwa na godoro moja ndani. Kwa kuangalia uwezo wetu kifedha, tulilazimika kutafuta eneo jingine na baada ya kuzunguka katika maeneo kadhaa, tulibahatika kupata hema kwa gharama ‘nafuu’ ya Sh25,000. Hema hilo kwa mujibu wa msimamizi wake, lilikuwa na uwezo wa kulaza watu watatu kwa wakati mmoja. Katika eneo lile kulikuwa na mahema yasiyopungua 20 na wakati tulipofika, saa 4.20 usiku, lilikuwa limebaki hema moja tu, ambalo ndilo tulilopewa na kulipa kiasi hicho cha fedha. Hema hili liligeuka kuwa makazi yetu ya muda kwani kila tulipofika kulala Samunge katika siku zote 14 tulizokaa Loliondo, tukiendelea na kazi zetu za kihabari, tulikuwa tukilitumia. Usiku wa taabuUsiku wa kwanza ulikuwa wa tabu kwetu kutokana na hema hilo kuwa na dogoro moja tu dogo. Ilibidi tuweke vichwa na sehemu ya viwiliwili vyetu kwenye godoro hili huku sehemu ya miili yetu ikibaki chini katika ‘sakafu’ ya hema hilo ambalo kwa jinsi lilivyotengenzwa ni kama suti kuanzia sakafu, kuta mpaka paa. Hatukuwa na shuka, blanketi, kanga wala kitenge kwa ajili yakujisitiri na baridi. Pamoja na kwamba Samunge si sehemu yenye baridi ya kutisha, lakini ulipofika usiku wa manane, tulilazimika kuyatafuta majaketi na makoti yetu.Baridi ilianza kuingia katika miili yetu kwa mbali. Kweli, ulikuwa ni usiku wa tabu na kila mmoja wetu alitamani kuche haraka ili tuweze kuondokana na adha hiyo. Haya yalithibitika asubuhi pale kila mmoja wetu alipokuwa akiusimulia ‘usiku wake’ ulivyokuwa. Ulifika wakati tukataka kuweka azimio la kutolala tena Samunge lakini, kwa jinsi mazingira yalivyokuwa, azimio hili halikutekelezeka kwani tulirejea kulala kijijini hapa mara tatu zaidi.Hali hii inanikumbusha usiku wa mvua na baridi kule Wasso ambako kina mama na watoto wao walikuwa wamelala barazani baada ya kukosa malazi. Nilijiuliza moyoni, ikiwa sisi ambao tumepata hema tunapata tabu kiasi hicho, hali ilikuwaje kwa wale waliolala nje bila hata ya kuwa na nguo ya kujisitiri?Pamoja na hali hii, watu bado walionekana kuwa na shauku kubwa ya kufika Samunge kupata kikombe kwa Mchungaji Mwasapila.Mwisho



KAENI MKAO WA KULA KUPATA BOONGE LA 'MOVIE' KATI YANGU NA AUNT EZEKIEL, PICHA ZINGINE BAADAE...


Hii ni 'SCENE' ya Ufukweni nikiwa na AUNT EZEKIEL ambayo pia tulifunika sana kwenye hii Movie yetu itakayotoka soon...

Mambo juu ya mambo, HAATWAARRIIIII....

Cameraman wangu huyu anaitwa AMANI, ni mkali sana na amefanya kazi kuubwa saana kushooot hii Movie daah...

Hii ni 'SCENE' ya nyumbani kwangu nikiwa na rafiki yangu STEVE SANDHU...

'MITEGO' kama hii lazma iwepo kwenye Movie ila ndio 'UNAVUMILIA' tu...

SCENE yangu na AUNT EZEKIEL ikiendelea, hii movie itakuwa 'BALAA' ikitoka daah......

Na hapa tukiwa na mwigizaji mwingine aitwae STEVE SANDHU ambaye nae 'AMENYONGA' sana kwenye Movie hii itakayotoka soon...

Hii ni 'SCENE' nyingine kati yangu na AUNT EZEKIEL ikiendelea, ni balaa nakwambia...

IJUE FILAMU ILIYOTENGENEZWA KWA 'GHARAMA' KUBWA ZAIDI DUNIANI...


Kwa taarifa yako hii ni Filamu ya 'AVATAR' ambayo ndio Filamu iliyotengenezwa kwa bei 'MBAYA' zaidi duniani mpaka sasa! Filamu hii ya 'AVATAR' imetengenezwa kwa gharama ya Dola millioni 500 sawa na Bilioni 740 za kibongo kutokana na vifaa vilivyotumika kuitengeneza Filamu hiyo na mfano ni 'Camera' zilizotumika kushoot Filamu hiyo zilitengenezwa maalum kwa ajili ya Filamu hiyo tuu! JAMES CAMEROON ndie alikuwa muongozaji wa Filamu hiyo iliyoshirikisha nyota kama vile SAM WORTHNGTON, ZOE SALDANA, STEOHEN LANG, MICHELLE RODRIGUEZ, JOEL MOORE, GIOVANNI RIBISI na SIGOURNEY WEAVER.