.

Thursday, August 11, 2011

WANAWAKE WANAOVUTA SIGARA HATARINI KULIKO WAUME.........


Utafiti mpya umeonyesha kwamba wanawake wenye tabia ya kuvuta sigara wako katika hatari ya kupata maradhi ya moyo zaidi kuliko wanaume wenye tabia hiyo.

Utafiti ulioendeshwa miongoni mwa zaidi ya watu milioni mbili umepata wanawake wako kwenye hatari ya maradhi ya moyo kwa asili mia 25 wakati wanapotumia tumbako.


Sababu za matokeo haya hazijatolowa japo watafiti kutoka Marekani wamesema wanawake wako kwenye hatari kubwa ya kuvuta kemikali zenye simu kutoka kwa sigara ikilinganishwa na wanaume.

STRANGE ADDICTIONS.......!!!!!!!!!!!

Adele amekuwa akila sponji za makochi kwa miaka 20 sasa akiwa amejisikia kuwa na mawazo anajiliwaza kwa kula makochi.

Lauren awali alikuwa addicted kunywa pombe na dawa za kulevya lakini sasa amekuwa addicted kufanya mazoezi kupita kiasi ambapo anafanya mazoezi kwa hadi saa 6 kwa siku.

Kesha amekiri kuwa anakula nusu ya pakiti la toilet paper kila siku mahali popote anapotembelea kwenye  gari movie.

Lori amekuwa addicted kulala na blow dryer tangu akiwa na umri wa miaka 8 inagawa anasikia kuungua na sauti kubwa lakin yuko tayari kuhatarisha maisha yake

Huyu yeye anakula sabuni.

Huyu anakula Glasi anaitwa Josh

HOT LIST YA WANAMUZIKI MATAJIRI WA HIP HOP................!!!!!!!

Forbes magazine's hip hop rich list imetoka na rapper Jay Z anaongoza kwenye Top 20 ya Hip hop Artist....


1. JAY Z - $37 MILLION


2. P DIDDY - $35 MILLION


3. KANYE WEST - $ 16 MILLION


4. LIL WAYNE - $ 15 MILLION


5. BIRDMAN - $15 MILLION


6. DR. DRE - $14 MILLION


7. SNOOP DOGG - $14 MILLION


8. EMINEM - $14 MILLION


9. AKON -$13 MILLION

10. LUDACRIS - $12 MILLION

BEHIND THE SCENE YA KIPINDI CHA MAMBO YOYO.......@ITV....

Baadhi ya maandalizi ambayo huwa yanafanywa kabla ya kuanza Kipindi cha mambo Yoyo kinachorushwa na Kituo cha ITV Jumapili saa kumi na moja kasoro dakika tano jioni.

Hizi picha za kipindi cha Jumapili hii na msanii atakaekuwepo tafadhali usikose kutazama.

Setting ya Camera

Msanii wa wiki akifanyiwa Make up

Mtangazaji wa kipindi Lady Hanifa akifanya Make Up kujiweka Smart mbele ya Camera

MAMA ALIYEKUTWA AMEKUFA BAADA YA KUPOTEA.........

Mama mmoja mkazi wa maeneo ya Tegeta jijini Dar es salaam ambaye alijifungua watoto wawili mapacha Arafa na Arafat na kwa bahati mbaya akaugua kichaa cha mimba na baadae kupotea bila kujulikana mahali alipo kwa juhudi za ndugu na jamaa za kumtafuta zikashindikana lakini jana mwili wake ukaonekana maeneo ya Tegeta akiwa amekufa na mwili wake kuwa kwenye hali mbaya.


Mashuhuda wakiwa eneo la tukio



Maiti ya mama huyo ikiwa imelala chini.
Watu wakimiminika kukimbilia eneo la tukio jana