.

Monday, June 6, 2011

"AISEE BABAANGU....CHESMA NA MKE WANGU USICHESE NA KASIAANGU"

Mr. Asenga ni shoe shiner maarufu jijini Dar-es-salaam anayefanyakazi ndani ya Bar ya Mango Garden Kinondoni, na yuko kwa mda mrefu sasa na yeye kama yeye ajidai kwa kukaa mda mrefu eneo hilo la biashara yake hiyo na kuendesha maisha yake ya kila siku. katika ofisi yake ana kandambili zisizopungua 20 kwaajili ya wateja wake wanapofika eneo hilo la biashara.




"Biashara ni hasubuhi atii jioni kwa mama Manka kujipongeza." Mr. Asenga akihesabu mkwanja baada ya kumaliza kazi ya mteja wake. Licha ya kua na kandambili zaidi ya 20, Asenga anasema kuna wakati wateja wake wengine hukosa ndala maana zote zinakua tayari zina watu tayari hata hivyo amesema otabidi atafute kijana wa kumsaiadia kazi ili na yeye awe BOSS.

MTANASHATI WA DUNIA AJIFUNZA U-BAA MEDI.

Kijana Kamal Ibrahim, ambaye ni mshindi wa Mr World 2011, katika tafrija iliyofanyika Chikago nchini marekani, kwenye tafrija hiyo jamaa alionekana akiwahudumia wageni waalikwa kana kwamba na yeye si mgeni mualikwa, lakini baadaye jamaa alisema anafanya hivyo kama kujifunza kutoa huduma za hotel ili aweze kuisaidia jamii yake ipasavyo. Katika tafrija hiyo pia alikuwepo mlimbende wa dunia Alexandria Mills 2010, na mlimbwende wa Afrika Emma Wareus ambapo kwa pamoja walijifunza mambo mbalimbali yahusuyo watoto na jamii kwa ujumla. Wabongo hapo vipi? Mkipata jina kidogo tu hamtaki kusalimia watu na magari yenu mnaweka tinted eti mnakwepa usumbufu kwa watoto nyooooooooooooo!!!!!!!

RIHANNA AITETEA VIDEO YAKE MPYA


Rihanna Mwanamuziki wa Marekani ameamua kuitetea video yake mpya ya "MAN DOWN" Kwa kile kilichoelezwa kua ndani ya video hiyo kuna vitendo ambavyo watoto wanaweza kujifunza mambo ya kigaidi Rihhana naye alifunguka na kusema kila mzazi anajukumu la kumlea mwanaye katika maadili mazuri ili asijiingize kwenye vitendo viovu na si video yake ndiyo itachochea uovu kuwepo.