.

Saturday, July 30, 2011

HAPPY BIRTHDAY TO YOUU!!!!!!!.........


Leo tarehe 30 July 2011 ni siku ya kuzaliwa ya mmoja wa wamiliki wa blog hii Mamaa Salma Dacotha ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha ''Yaliyomo yamo'' kupitia Radio One stereo kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Alhamis saa 3 kamili asubuhi hadi saa 6 mchana ambapo anatimiza miaka kadhaa ya maisha yake.Blog hii inamtakia kila kheri katika maisha yake na kubariki kazi ya mikono yake siku zote akiwa na afya njema.

JAY Z ADAKWA AKICHAKACHUA............!!!!!


Rapa Jay Z hivi karibuni amedakwa katika mazingira ya mashaka ambayo yanamuonyesha kama anatoka nje ya ndoa yake na mke wake wa long tym Beyonce Knowles ambapo amenaswa katika hoteli moja akipata mlo wa usiku kwa staili ya wapendanao na mwanadada ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja.


Jay z hakuambatana na mke wake aliyekuwa katika sherehe maalum ya utambulisho wa albamu mpya ya aliyekuwa mmoja wa member wa kundi la Destiny Child Kelly Rowland.

KUNANI JLO NA P DIDDY......!!!!???


Kuna habari kuwa baada ya kuachana na mume wake Marc Anthony nyota wa muziki Jennifer Lopez amerudiana na ex wake yani mpenzi wa zama ni Sean Diddy Combs''Diddy'' na chanzo cha habari kinaripoti kuwa nyota hao walitwa wakipata Dinner pamoja NYC julai 27 mwaka huu.


Chanzo hicho kinadai Jlo alianza kujisogeza karibu kwa P Diddy baada ya ndoa yake na Marc Anthony kuanza kuyumba lakini pia ripoti za hivi karibuni zinadai Jlo alianza kuwa na mahusino na kijana mtanashati ambaye ameshiriki kama mpenzi wake katika Video ya wimbo wa ''Im Into You''.