| Shughuli ilianza pale Vimwana Manywele na Twanga Pepeta, wakijitambulisha kwa mashabiki na majaji kwa kuingia stejini na vazi la asili. |
| Wakionesha umahiri wao katika kunengua na vazi la asili. |
| Hakuna cha bure duniani ni lazima jasho likutoke mtoto wa kike. |
| "Hapo sasa hapo sasa" zungusha nyonga mwananguu. |
| Mratibu wa Kimwana Manywele na Twanga Pepeta, Maimatha wa Jesse baaada ya kupagawa na kuwasogelea Vimwana na kuwatunza. |
| "Kweli kazi ni ngumu" baada ya kumaliza ngwe ya kwanza wakatoka kwaajili ya kuingia ngwe nyingine. |
| Safari ya mmoja mmoja kuonesha umahiri wake ikaanza ili kusaka nafasi ya kwenda fainali. |
| Chief Judge, Methew Kiongozi aliye kulia akifuatilia kwa umakini mkubwa mpambano ukiendelea katika Club Suncirro. |
| Twanga Pepeta nao walito ushirikiano wa kutosha katika kutoa show ya nguvu. |
| Ukawadia ule mda wa kuvuna ulichopanda kipindi chote wakiwa kambini. Chief Judge akisoma waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali. |
| "Kiukweli siamini kama nimepita!!!" |
| Hawa ndiyo kumi bora wakipongezana baada ya kutangazwa kuwa ndiyo wataingia kwenye fainali itakayofanyika tarehe 17/6/2011, pale Ubungo Plaza. |
| Wakiwa kwenye picha ya pamoja, wakiwa na na wadau mbali mbali. |
| Hawa ndiyo kumi bora waliamua kutoa show ya shukrani kwa kufanikiwa kupita kuelekea fainali. |
| Sajent akitoa shukrani kwa walihudhuria. |



















