.

Tuesday, February 1, 2011

EEEEH MUNGU TUSAMEHE DHAMBI ZETU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 Ni tukio ambalo limeshitua na kusikitisha watu jana katika jiji la Dar es salam,Eneo la Mwananyamala  kwa kopa karibu na Makabuiri ya Mwnanyamala , walikutwa  watoto   wachanga 11 wamefukiwa katika shimo lenye urefu wa futi moja wakiwa wamevingirishwa katika shuka moja lenye nembo ya hospitali ya Mwananyamala.
Hili ndilo shimo ambalo ilifukiwa miili ya watoto wachanga waliokutwa wamefariki. Eneo hili lilitambuliwa na  bwana mmoja aliyejulikana kwa jina moja tu la thabit alipokuwa katika harakati za kutafuta eneo la kuchimba kwa ajili ya kutupia takataka. Ukweli inasikitisha sana. Mpaka sasa swala hili lipo katika mikono ya sheria  tutaendelea kukupa habari mambo yanavyoendelea.