.

Sunday, May 15, 2011

ARUKA GHOROFANI NA KUPOTEZA MAISHA.

Bingwa wa Olympiki katika mbio za masafa marefu za Marathon Mkenya Samuel Wanjiru ameaga dunia.
Duru za polisi zinasema, Wanjiru alikumbana na mauti baada ya kuruka kutoka kwa chumba chake cha ghorofa moja katika eneo la Nyahururu, mkoa wa Kati wa Kenya.
Idara ya polisi imethibitisha kifo hicho na kusema kwamba uchunguzi umeanzishwa ili kubainisha sababu za kifo hicho.
Mwanariadha huyo alishinda medali ya dhahabu katika mbio za olimpiki mwaka wa 2008 mjini Beijing, kwa kuweka muda wa 2:06:32. na kuandikisha rekodi ya kuwa mkenya wa kwanza kushinda mbio za marathon kwa upande wa wanaume .
Wanjiru pia alikuwa bingwa wa ulimwengu katika misururu ya mbio za marathon, maarufu kama world marathon majors kuanzia mwaka wa 2008 hadi mwaka wa 2010.
Wanjiru pia aliweka rekodi ya mbio za kilomita 21 kwa kuandikisha muda wa dakika 58:33.
Mwezi Decemba mwaka uliopita wanjiru alifikishwa mahakama, kwa mashtaka ya kutishia kumuua mkewe, kumjeruhi mlinzi wake wa nyumbani na pia kumiliki bunduki aina ya AK-47 bila idhini ya serikali.
Mapema mwaka huu Wanjiru alihusika kwenye ajali mbaya ya barabarani katika barabara ya kutoka Nairobi kuelekea Nyahururu, hatua iliyomfanya kujiondoa kutoka kwa mbio za London Marathon

JENGO GHALI KULIKO YOTE DUNIANI

Mukesh Ambani, ni tajiri bilionea kuliko wote nchini India, na pia ni tajiri wa nne kwa thamani katika levo za dunia. Ambani amejijengea jumba la kuishi lenye thamani za Dola Bilioni za Kimarekani.
 Jumba hili lina ghorofa 27 ambazo ukizizungukia zote kwa siku moja basi unamaliza mahitaji yako karibu yote bila kutoka nje ya mjengo huo. Mukesh amesema kwamba hili ni jumba la kuishi yeye, mkewe kipenzi, na watoto wao watatu (Hapa lazima mwafrika apige kelele).

Katika jumba hili kuna sehemu maalum kwa ajili ya kufanyia mazoezi na kutunza afya kwa ujumla, mahala pa kuchezea dansi penye ukubwa kama wa klabu zetu tunazozifahamu hapa nyumbani, madimbwi kadhaa ya kuogelea (swimming pool), ukumbi wa kutazamia senema unaoweza kubeba watu 50 kwa wakati mmoja, vyumba kibao vya wageni (mwafrika sijui ataendelea kulalama kwenye hili?), na mwisho kabisa ni varanda zenye ukubwa wa kucheza sarakasi kabisa.

Ukitaka kufika nyumbani kwa bwana Mukesh, unaweza kutumia usafiri wa aina mbalimbali. Kama unajua wazi kwamba foleni za India zitakufanya uwe unasonya njia nzima basi unaweza kuchukua helikopta, pale nyumbani kwa bwana Mukesh kuna viwanja vitatu kwa ajili ya usafiri huo. Kama namna gani vipi umenunua gari mpya na unataka kwenda nayo kumlingishia bwana Mukesh usitie shaka, ana uwanja wa kuegesha magari 160 kwa wakati mmoja.

Ukishuka kwenye gari au kipepeo (helikopta) chako kuna lifti tisa zinakusubiri wewe uende kokote katika ghorofa hizi 27, kwa hiyo dada zangu msitie shaka, komeleeni michuchumio ile ile ya mwaka.

MJUE TAJIRI MKUBWA DUNIANI.

Carlos Slim, tajiri mkubwa kabisa duniani, kwa mara nyingine tena ameendelea kutete kiti chake cha mtu mwenye mavumba zaidi ya binadamu mwingine yeyote hapa duniani. Carlos ni mtu wa Mexico na ni mmiliki wa makampuni yanayojihusisha na huduma za mawasiliano.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes ni kwamba Slim kwa mara nyingine amempiga bao mwenyekiti wa kampuni la Microsoft, Bill Gates, ambaye ndiye alikuwa tajiri mkubwa kwa kitambo kirefu kabla ya kubwagwa na Slim miaka michache iliyopita.
Jarida la Forbes linasama kwa takwimu zao inaonekana Slim amejiongezea utajiri wake kwa karibu asilimia 40 zaidi. Thamani ya utajiri wake imeongezeka toka dolari bilioni 20.5 hadi dolari bilioni 74, huku akimwacha Gates katika nafasi ya pili akiwa na dolari bilioni 56 mchagoni.
Forbes wanendelea kutwambia kwamba mwaka huu kumekuwa na ongezeko la idadi ya mabilionea wapya 200. Sita kati ya mabilionea hawa ni wawekezaji katika hisa za kampuni la Facebook, akiwamo mwanzilishi wa kampuni hilo, Mark Zukcerberg.
Dustin Moskovitz ndiye bilionea mdogo kuliko wote duniani, akiwa na umri wa miaka 26 tu, na ni mwekezaji katika hisa za kampuni la Facebook.
Mwanzilishi wa kampuni la  Ikea, Ingvar Kamprad, ndio bilionea aliyepoteza fedha nyingi kwa mwaka huu. Forbes wameshudia utajiri wake ukiporomoka toka dolari bilioni 17 kibindoni hadi bilioni 6 mchagoni.
Inasemekana utajiri wa pamoja wa mabilionea wote hawa umefikia dolari trilioni 4.5, wamevunja rekodi.
Ifuatayo ni ordha ya mabilionea hawa wa dunia:

KUACHA KUMBUKUMBU NI MUHIMU.

Gari la Bob Marley.

Pichani ni gari aina ya Land Rover ambayo ni moja kati ya kumbukumbu za vifaa vya nguli wa muziki wa Reggae Duniani hayati Bob Marley gari hili limehifadhiwa kwa wale wanaotembelea kuona na kujua histori ya Hayati Bob Marley huko Kingston Jamaica.

SIMBA YAITOA TP MAZEMBE.


Katika taarifa iliyotolewa muda mfupi baada ya uamuzi wa Kamati ya Maandalizi ya Caf kwa mashindano ya vilabu, klabu hiyo ya Congo imesisitiza haijavunja sheria kwa kumchezesha Janvier Besala Bokungu, ambaye klabu ya soka ya Simba ya Tanzania imemshutumu alivunja mkataba wake na klabu ya Esperance na kujiunga na Mazembe, hali iliyomfanya asistahili kucheza katika michuano ya Caf.
“Uongozi wa Mazembe unauona uamuzi wa Caf haukubaliki ndio maana haraka tutakata rufaa kutokana na uamuzi huo. Meneja wetu Mkuu Frederick Kitenge kwa sasa yupo Cairo akiangalia vipengele vyote vya kupata haki kwa klabu yetu,” Taarifa hiyo ya Caf imesomeka katika mtandao rasmi wa Corbeaux.
Iwapo rufaa ya Mazembe itagonga mwamba, watakosa nafasi ya kutetea ubingwa wao na pengine kuweka rekodi ya kuwa mabingwa wa vilabu barani Afrika kwa mwaka wa tatu mfululizo, ambapo klabu hiyo imesema ndio lengo lao kuu msimu huu.
Katika hali nyingine, Chama cha taifa cha kandanda cha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kimetupilia mbali maombi ya Mazembe ya kutaka kuahirishwa mechi yake ya mwishoni mwa wiki dhidi ya DCMP, kwa sababu mabingwa hao wana ziara ya mazoezi nchini Brazil.
DCMP itadai pointi zote tatu iwapo Mazembe haitatokea uwanjani siku ya Jumapili. Kuna mashaka kama timu hiyo itasafiri kuelekea Marekani Kusini ili ikabiliane na DCMP.

"LIKE A FATHER LIKE A SON.

 
Prince Mtambalike mwenye T.shirt nyekundu akifuatilia kwa makini maelezo toka director wake Single Mtambalike, Richie Richie a.k.a Denzel Washington ambaye ni baba yake mzazi. Prince ambaye ameshiriki kwenye filamu iitwayo "MTAANI KWETU" Prince aliyecheza kama Muhamed ameonesha uwezo wa hali ya juu  kiasi cha kuwafuahisha wote waliokua nao Location. Richie akizungumza na safuu hii amesema filamu hiyo itakua moto wa kuotea mbali maana mbali na yeye mwenyewe kuiongoza, pia amechegeza. Richie ameeleza kipaji cha mwanaye ni kikubwa mno kiasi cha kuwatahadharisha wale wote walio kwenye tasnia hii wajipange."kwa kweli mwanangu amenionesha kipaji cha hali ya juu mimi mwenyewe sikutegemea."

KIMWANA MANYWELE NA DHAMIRA ISIYOELEWEKA.

Kimwana Manywele Husna Iddy (Sajent) mshindi wa mwaka 2007, mwenye top ya njano akiwa na vimwana wa manywele katika mazoezi yao katika kambbi yao ya ASET iliyoko Kinondoni.,
Swali ni kwamba je ni lazma hawa vimwana wawe wanajua kukataviuno? mimi nilidhani hayo maswala kukat viuno wangewaachia bendi zenyewe zitafute mnenguaji bora wa kike. Tutamtafuta muandaaji wa shindano hili ili atupe dhumuni la shindano hili.


Husna (Sajent) akiwa na Kasim (Super K) wakiwa wanatoa maelekezo ya jinsi ya kucheza style za Twanga Pepepta.

Akiwa nao katika mpinda mgongo style.