.

Thursday, August 4, 2011

LADY GAGA,TIMBERLAKE WAKALI WA KUTUPIA...........!!!!!


Lady Gaga

Wanamuziki Justin Timberlake na Lady Gaga wameshika nafasi ya kwanza katika chaguo la jarida Vanity 2011 kwa kuwa wasanii namba moja wa kimataifa wanaovaa viwalo vikali kali duniani.Waimbaji hao wamechagulia ikiwa ni sehemu ya mikakati ya jarida hilo ya kumsaka msanii wa kimataifa anaetinga viwalo vikali vya mitindo mbalimbali duniani.


Justine Timberlake


Justine Timberlake akiwa jukwaani
Washindi wengine wanaokubalika kwa kuvaa mavazi mazuri ni pamoja na Johnny Depp, muigizaji Carey Mulligan, Nyota wa "The King's Speech" Colin Firth, mshindi wa Oscar Tilda Swinton pamoja na muigizaji wa "The Social Network's" Armie Hammer.

Johny Depp

OPRAH KUPEWA TUZO YA HESHIMA...........


Opray Winfrey
Malkia wa vipindi vya TV vya mahojiano Oprah Winfrey pamoja na muigizaji James Earl Jones watapatiwa tuzo za heshima katika sherehe za utoaji tuzo za Oscar za mwaka huu.Winfrey ambaye  aliyewahi kutwaa tuzo ya Oscar ya muigizaji bora msaidizi mwaka 1985 kupitia filamu ya ''The Colour Purple'', atapewa tuzo ya Jean Hersholt Humanitarian kutokana na kujitolea kwake mno kutoa misaada.

James Earl Jones
Jones pamoja na msanii Dick Smith watapatiwa tuzo maalum kutokana na kufanya vyema katika kazi zao za uigizaji filamu.

HAPPY BIRTHDAY YOUU...BARACK OBAMA....!!!!!

Rais Barrack Hussein Obama

Leo tarehe 04 Aug 2011 ni siku ya kuzaliwa kwa rais wa 44 wa Marekani Barrack Hussein Obama ambaye anatimiza miaka 50.


Rais Obama akiwa na mkewe Michelle Ohama

Barack Obama alizaliwa mwaka 1961 sawa na taifa la Tanzania ambapo alifunga ndoa na Michelle Robinson October 3,1992 na kufanikiwakupata mtoto wa kwanza Malia Ann mnmo wa July 4,1998 na baadaye Natasha ambaye aliyezaliwa June 10,2001.



Rais Obama na watoto wake Malia na Natasha pamoja na mkewe Michelle katika nyakati za furaha.