.

Sunday, July 17, 2011

HAPPY BIRTHDAY MWAMBA WA AFRIKA KUSINI


Afrika Kusini leo tarehe 18 July 2011 inasherehekea siku ya kuzaliwa ya rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela ambaye anatimiza miaka 93.


Mandela anasherekea siku hiyo akiwa na afya nzuri huku taasisi yake ikiwa imetoa wito kwa kuwataka wananchi kufanya kazi za kujitolea kwa dakika 67 kwa siku hii ya leo kusherehekea miaka 67 aliyojitolea kupigania uhuru wa watu wa Afrika Kusini.

Nyota huyo ambaye ni mwamba aliyepigani uhuru wa taifa hilo na anayepingana na ubaguzi wa rangi anatarajia kutumia siku hii na familia yake katika kijiji alichokulia Mashariki mwa Cape ambapo watoto wa shule yenye watoto milioni 12.4 inatarajia kumuimbia mfululizo kumpongeza.


Tunamtakia maisha marefu zaidi yenye afya njema daima....Happy Birthday Nelson Mandela.........!!!!!!