.

Sunday, July 31, 2011

SALMA'S BIRTHDAY PARTY@NYUMBANI LOUNGE..........!!!!!!!!!

Picha hapo chini zinajieleza jinsi mambo yalivyokuwa Hot Hot katika siku ya kuzaliwa ya Mtangazaji mahiri wa kituo cha Radio One Stereo party iliyofanyika Nyumbani Lounge na kuhudhuriwa na marafiki zake kwa mwaliko maalum......



Shoping ilianzia Kiki's Fashion







Champeign ilifunguliwa na bosi mwenyewe Deogratius Rweyunga......

Cheerssss.........!!!!

Wadadaz

Mahalatito Salma Dacotha an'Hanifa Hamidu marafiki wa kweli........




Salma akipokea zawadi yake ya Laptop kutoka kwa mtu wake wa karibu....

Lady Hanifa na Skyner


Kiatuzzzz cha Ukweee!!!!


Mr & Mrs Kimwaga nao waliwakilisha.....

Saturday, July 30, 2011

HAPPY BIRTHDAY TO YOUU!!!!!!!.........


Leo tarehe 30 July 2011 ni siku ya kuzaliwa ya mmoja wa wamiliki wa blog hii Mamaa Salma Dacotha ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha ''Yaliyomo yamo'' kupitia Radio One stereo kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Alhamis saa 3 kamili asubuhi hadi saa 6 mchana ambapo anatimiza miaka kadhaa ya maisha yake.Blog hii inamtakia kila kheri katika maisha yake na kubariki kazi ya mikono yake siku zote akiwa na afya njema.

JAY Z ADAKWA AKICHAKACHUA............!!!!!


Rapa Jay Z hivi karibuni amedakwa katika mazingira ya mashaka ambayo yanamuonyesha kama anatoka nje ya ndoa yake na mke wake wa long tym Beyonce Knowles ambapo amenaswa katika hoteli moja akipata mlo wa usiku kwa staili ya wapendanao na mwanadada ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja.


Jay z hakuambatana na mke wake aliyekuwa katika sherehe maalum ya utambulisho wa albamu mpya ya aliyekuwa mmoja wa member wa kundi la Destiny Child Kelly Rowland.

KUNANI JLO NA P DIDDY......!!!!???


Kuna habari kuwa baada ya kuachana na mume wake Marc Anthony nyota wa muziki Jennifer Lopez amerudiana na ex wake yani mpenzi wa zama ni Sean Diddy Combs''Diddy'' na chanzo cha habari kinaripoti kuwa nyota hao walitwa wakipata Dinner pamoja NYC julai 27 mwaka huu.


Chanzo hicho kinadai Jlo alianza kujisogeza karibu kwa P Diddy baada ya ndoa yake na Marc Anthony kuanza kuyumba lakini pia ripoti za hivi karibuni zinadai Jlo alianza kuwa na mahusino na kijana mtanashati ambaye ameshiriki kama mpenzi wake katika Video ya wimbo wa ''Im Into You''.

Thursday, July 28, 2011

NICKI MINAJ APIGWA FAINI


Rapa wa kike wa Marekani Nicki Minaj amepigwa faini baada ya kuimba mashairi yenye lugha chafu jukwaani wakati akitumbuiza nchini Jamaica mwishoni mwa wiki.


Mwanamuziki huyo aliwasilishiwa hati ya kuvunja sheria za nchi hiyo baada ya kutumbuiza katika ukumbi wa Reggae Sumfest huko Montego Bay.ambapo alipigwa faini ya dola elfu moja za Jamaica ambazo ni sawa na dola 12 za Marekani kutokana na fedha za nchi hiyo kutokuwa na thamani.

JAY DEE MWANAMUZIKI ANAEHESHIMIKA KWA MATENDO YAKE............


Ijumaa iliyopita tarehe 22 July 2011 bendi inayoongozwa na mwanadada mahiri na anaheshimika nchini Tanzania Judith Wambura wengi tunamfahamu kama Lady Jay Dee ilitimiza miaka 6 tangu kuanzishwa kwake na kudhihirisha furaha na kuthamini mchango wawanaomzunguka Jay Dee aliamua kutoa tuzo wafanyakazi wake ikiwemo tuzo ya mfanyakazi bora,mfanyakazi mwenye nidhamu,mfanyakazi aliyeudumu n bendi kwa muda mrefu n.k vile aliweza kutoa tuzo kwa mashabiki wake ikiwemo best female na male suporter.





Hakika Jaydee atabaki kuwa mwanamuziki anayeheshimika siku zote nchini Tanzania kutokana na kujua anachokifanya katika kazi yake ya muziki ikiwemo kubuni vitu mbalimbali ambavyo vitaendelea kumuweka katika gemu muda mrefu kama hivi karibuni tulivyoona akizundua maji yake ya kunywa ya Jay Dee Pure Drinking water na kufanya vitu vingi katika jamii.

Blog Hii inamtakia kila la kheri Judith Wambura Mbibo ''Lady Jay Dee'' katika kila analofanya Mungu ataendelea kubariki kazi ya mikono yako kila siku endelea kuwa mfano wa kuigwa kila siku kwa wanamuziki wa sasa na wa baadae.....

BECKHAM AWEKA MAJINA YA WATOTO WAKE KWENYE VIATU..........


Nyota wa soka ulimwenguni David Bekham anazidi kudhihirisha mapenzi makubwa aliyonayo kwa kids wake kwa kuamua kuanika majina yao kwenye viatu vyake vya kusakatia kabumbu.


Beckham aliweka majina na watoto wake ambao ni Brooklin,Cruz,Romeo pamoja na Harper seven..

BIG BROTHER GRAND FINALE!!!!!!!!!.................

Shindano la Big Brother ambalo lilianza Mei 1 mwaka huu linafikia tamati yake Jumapili wiki hii huku washiriki saba wakiwa bado ndani jumba hilo kugombea kitita cha 200 000 ambapo kwa mwa huu kutakuwa na washjindi wawili ambao watanyakua kitita hicho kila mmoja.














Washiriki waliobaki ni pamoja na Hanni wa Ethiopia,wawakilishi wa Nigeria Vina na Karen,Luclay ambaye anatoka Afrika Kusini,Lomwe wa Malawi,Wendal wa Zimbabwe pamoja na Sharon O ambaye ni mwakilishi pekee aliyebaki kutoka Afrika Mashariki wa nchini Uganda.



Katika fainali hizo wasanii mbalimbali watatoa burudani ambapo Tanzania inawakilishwa na mwanamuziki wa miondoko ya Crunk C PWAA,Fally Ipupa kutoka DRC,WizKid na Mo’Cheddah kutoka Naija Nigeria,Professor na Speedy kutoka Afrika kusini.

Kaa tayari Jumapili hii kuona nani atabahatika baada ya mchakamchaka wa siku 91 zenye furaha,majonzi,mabishano,mivutano,mahusiano na kila aina ya vituko vilivyofanyika ndani ya BIG BROTHER AMPLIFIED 2011 ambayo Tanzania iliwakilishwa vyema vya wanadada Bhoke Egina pamoja na Lotus Kyamba.


WABUNGE CHADEMA WATOLEWA BUNGENI.................


Wabunge watatu wa Chadema leo wametolewa nje ya bunge baada ya kuvunja kanuni za bunge kwa kuwasha vipaza sauti (MIC) na kuongea bila mpangilio.



Wabunge hao mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu,Godbless Lema wa Arusha mjini na Mchungaji Peter Msigwa mbunge wa Iringa Mjini walitoka nje ya bunge wakisindikizwa na askari wa bunge na naibu spika wa bunge Job Ndungai.