.

Tuesday, February 22, 2011

TUNAOMBA RADHI

Wadau tunaomba radhi , muda mrefu  sasa hatujaweka vitu  ambavyo mnatamani kuvipata kupitia  Blog yetu. Tunawaaahidi wiki ijayo mtapata mambo mazuri. Tunaomba radhi wadau mambo yameingiliana.
                                          TUNAWAPENDA SANA

Monday, February 7, 2011

NANI MATAWI YA JUU KATIKA KIVAZI CHA JIONI

             Rihana katupia kitu cha pink,c unajua tena pink for ladies


                Haya sasa mama wa nick kanon naye .Mariah Carey
     Mrs Shawn Corey Carter (jay-z) katupia kitu cha gold na black,Beyonce
Mrs Marc Anthony ,Jeniffer lopez hapo vp............................... 

Saturday, February 5, 2011

EPUKA UCHAFU KATIKA MAPENZI

           Katika mapenzi epuka uchafu  kwani  unaweza kumkera mpenzi wako kwa kuwa mchafu , Jitaidi kila wakati kuwa msafi ili uwe kivutio kwa mpemzi wako na  hili liwe kwa pande zote mbili isiwe kwa mwanamke peke yake. Kumekuwa na hisia flani kuwa mwanamke ndie anatakiwa kuwa msafi muda wote hii ni dhana potofu kwani ata mwanaume anatakiwa kuwa msafi  kwa mpenzi wake .Tuangalie sehemu muhimu  katika mapenzi inakera kumuona mpenzi wako ananuka Mdomo, Jasho  na sehemu nyingine   ambazo zinakera sana pia kuwa mchafu wa mavazi  haipendezi.Jitahidi  kujiweka sawa katika usafi ili kumvutia mwenzio kwani atatamakukumbatia muda wote na kuwakaribu na wewe.Kwaleo tuishie hapa tukutane tena katika ukurasa wa mapenzi kuwekana sawa

Wednesday, February 2, 2011

HARUSI YA INNI EDO WA NIGERIA

                          Gari hili lilimbemba Inni Edo na mumewe siku ya harusi yao
INNI  EDO ni msanii wa filamu wa kike kutoka nchini Nigeria,Amezaliwa tar 19 april 1982.Alianza uigizaji mwaka 2000,hadi sasa ameshacheza filamu zaidi ya 50,na alimaliza chuo cha sanaa university of calabar.
                                                     Akiiingia ukumbini FULL KUJIAMINI
                                                       Mi mzuri jamani na nimependeza
                                                     Akimpa support mr kukata keki
                                                Shosti akiuza sura,sijui ya kwake lini
                                                   Mmmmmmmmmmm,kitu cha lace weag
                                                       Jamani colour mmeiona hiyo
                                                     Mashostito wakiuza nyago
                                      Jamani suala la mila pia lilichukua nafasi yake
                                            Mwanamke mume ,Mwanamke ndoaaaaaaaaaaaaaaa
                                                                Abega Abega........
                             Huku ndiko chimbuko la vilemba.Vilemba oyeeeeeeeeeeeeeeeeeee




UREMBO

Asilimia kubwa ya watu wazima na vijana wa sasa wamekuwa na muonekano wa weusi kwenye macho pasipo kujua sababu na namna ya kuuondoa.
Huu weusi wakati mwingine unakuwa katika mfumo wa macho kuvimba na husababishwa na vitu vifuatavyo.

Ukosefu wa usingizi, uchovu, msongo wa mawazo, ukosefu au upungufu wa lishe au wakati mwingine dalili ya kuwepo kwa ugonjwa.
Mtu anapokuwa na mafua makali pia macho huonekana meusi na kuwa yamevimba
Kwa watu wenye umri mkubwa mfano kuanzia miaka 40 na kuendelea wanaweza kukumbana na hii hali ikiwa ni ishara ya ngozi kuanza kuzeeka.

Kuepuka hali hii fanya yafuatayo:
 1-Kunywa maji kwa wingi, yani glasi 8 hadi 10 kwa siku kila siku.
 2-Hakikisha unaepuka njia au vitu vinavyofanya uchoshe macho kama vile kutumia kompyuta au kuangalia TV kwa muda mrefu.
3-Hakikisha huachi cream ya aina yoyote katika ngozi ya macho kwa muda mrefu, dakika kumi baada ya kupaka krimu usoni futa kuzunguka macho ili kuiondoa.
4-Unapolala tumia mto ili kunyanyua kiichwa na kuzuia maji maji ya mwili kujilimbikiza katika eneo linalozunguka macho wakati umelala.
TIba:
Weka slesi za viazi kwenye macho ukiwa umeyafunga na uiache kwa dakika 15-20. Au tumia tango la baridi kuweka kwenye macho au majani ya chai (tea bags) iliyokwisha tumika kwa dakika 20.

Paka mchanganyiko wa limao na juisi ya nyanya kwenye sehemu iliyoathirika kila siku mara mbili.

Kila jioni paka mafuta ya mzaituni.

Tuesday, February 1, 2011

EEEEH MUNGU TUSAMEHE DHAMBI ZETU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 Ni tukio ambalo limeshitua na kusikitisha watu jana katika jiji la Dar es salam,Eneo la Mwananyamala  kwa kopa karibu na Makabuiri ya Mwnanyamala , walikutwa  watoto   wachanga 11 wamefukiwa katika shimo lenye urefu wa futi moja wakiwa wamevingirishwa katika shuka moja lenye nembo ya hospitali ya Mwananyamala.
Hili ndilo shimo ambalo ilifukiwa miili ya watoto wachanga waliokutwa wamefariki. Eneo hili lilitambuliwa na  bwana mmoja aliyejulikana kwa jina moja tu la thabit alipokuwa katika harakati za kutafuta eneo la kuchimba kwa ajili ya kutupia takataka. Ukweli inasikitisha sana. Mpaka sasa swala hili lipo katika mikono ya sheria  tutaendelea kukupa habari mambo yanavyoendelea.