.

Thursday, June 9, 2011

"HAWA NDIYO WANAOPOTEZA FEDHA KWENYE TIMU ZETU HAPA NCHINI"

Ugumu wa maisha umewafanya vijana kubunu biashar zilizo halali na zisizo halali. Ukipita maeneo ya Kariakoo na Karume utaona kuna jezi za timu mbalimbali za hapa nchini na nje ya nchi yetu zikiwa zimetandazwa chini, swali ni je! wenye timu zao kama Simba, Azam Fc, Yanga na nyingine nyingi zimetoa vibali kwa vijana hawa kuuza jezi hizi?

"BAJETI IMEWAKUMBUKA WATU HAWA?"

Wapo vijana ambao maisha yao hutegemea zaidi foleni ya jijin Dar-es-salaam kama anavyoonekana kijana huyu kwenye picha kijana huyu alipokua akiuza samaki maeneo ya Mikocheni, ambapo anasema kwa eneo la Mikocheni wangejengewa eneo la kuuzia samaki wao.