.

Thursday, August 18, 2011

KAA TAYARI KWA DEVIL'S KINGDOM............!!!!!!!


Filamu ya Devil's Kingdom ya nguli wa filamu nchini Steven Kanumba ambayo inakadiriwa kutumia mamilioni ya fedha katika utengenezaji wake na ikiwashirikisha nyota wakali wa filamu wa hapa nyumbani na pia kuwa filamu pekee iliyoweza kumleta msanii kutoka nje ya nchi inatarajiwa kutoka hivi karibuni kaa tayari.

Baadhi ya washiriki wa filamu hiyo wakati wa upigaji picha

Gwiji huyo ametumia fedha hizo ikiwa ni pamoja na ujio wa Super Star Ramsey Noah kutoka nchini Nigeria kwa ajili ya kuja kurekodi filamu hiyo ya aina yake na kuweka historia kwa kampuni yake kuonyesha nia zaidi ya kuipeleka mbele sanaa hiyo ya filamu kwa kuwashirikisha nyota wakali kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwakutanisha na wasanii wa hapa nyumbani kupitia kazi zao na kupata uzoefu kutoka kwa wasanii hao.
Ramsey Noah na Steven Kanumba

FAST AND FURIOS 6 KUTOKA 2013.........!!!!!!


Vin Diesel

Movie kali inayotikisa ya series ya mwigizaji wa filamu za kibabe, Vin Diesel inayokwenda kwa jina la Fast and Furious 6 imepangwa kuachiwa mwaka 2013.

Filamu iliyotokisa ya Fast 5

Filamu hiyo inayohusu uhalifu wa genge moja la kutengeneza fedha imetengenezwa chini ya mtayarishaji maarufu Justin Lin inatarajiwa kuwa tishio zaidi ya zile zile zilizopita.

Mtayarishaji wa Fast and Furios Justin Lin

Movie ya mwisho kutoka ya hivi karibuni ya Fast Five imeonyesha mafanikio kwa kuuza jumla ya nakala dola milioni 600 duniani kote.

Baadhi ya utamu wa vipande vya movie ya Fast Five.........




''BEYONCE KAMA MICHAEL JACKSON''............!!!!!!

Beyonce akiwa on stage

Rapa Shawn Carter''Jay Z'' amemwagia sifa mkewe mwanadada Beyonce Knowles kuwa anamuona kama Michael Jackson wa pilia liyebaki duniani.

Beyonce na Jay Z

Jay Z amesema katika chombo kimoja cha habari nchini Marekani kuwa ufanyakazi kazi wa nguvu wa mke wake ndio unaoumpa shoo nyingi na kuwafanya baadhi ya watu kufikiria kuwa anafanya kazi kwa mashine ambapo amesema uwezo huo ameuona wakati anamsindikiza kufanya onyesho la kutangaza albamu yake ya nne.

Mfalme wa Pop Michael Jackson enzi za uhai wake akifanya shoo

Jay Z anasema anamuona mkew kama Michel Jackson wa pili aliyebaki duniani baada ya kwanza kufariki akiwa na miaka 50.

YANGA ILIVYOLIWA 'DAKU' NA SIMBA............!!!!BAO 2-0......

Kibao kikionyesha 2 bila Live!!!!!

Mabao mawili kutoka kwa wachezaji Haruna Moshi ‘Boban’ na Felix Sunzu yalitosha kuinyamazishaa Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa jana usiku katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufanya Simba iibuke na ushindi wa mabao 2-0.

Timu ya soka ya Simba kabla ya mechi kuanza
Simba na Yanga zikimenyana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Mchezaji wa Simba Uhuru Selemani akinyanyua juu ngao ya hisani mara baada ya kukabidhiwa rasmi katika mchezo huo.
Mashabiki wa Simba wakishangilia Game jana ilikuwa raha tupu
Wachezaji wa Simba wakishangilia kutoka kulia ni Emmanuel Okwi, Victor Costa, Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Juma K. Juma.

ASKARI WAFANYA NGONO KITUONI.............!!!!

Jeshi la Afrika Kusini limeingia kwenye kashfa baada ya Askari wawili toka nchini humo kujulikana kuwa walifanya mapenzi wakiwa kazini tena na uniform za kazi.
Shuka chini ushuhudie tukio by tukio........

Kwa hisani ya www.chiniyacarpet.blogspot.com....unaweza kutembea kila siku kwa habari za burudani ambazo hazijachakachuliwa mahali popote.....