.

Tuesday, July 19, 2011

NJAA SOMALIA INAZIDI KUTISHIA............


Hali ya njaa katika nchi ya Somalia inazidi kuwa mbaya na Umoja wa mataifa umelenga kutangaza kuwa sehemu kadhaa nchini humo zinakabaliwa na janga la kimataifa kufuatia hali hiyo.


Maelfu ya familia yapo katika hali mbaya ya uhitaji wa chakula na maji na wanatembea mwendo mrefu kutoka nchini Somalia mpaka katika makambi ya wakimbizi ya Dadaab huko  mashariki mwa Kenya.






Hali ya ukame iliyolikumba eneo hilo haijawahi kuonekana kwa zaidi ya miaka 60 na umoja wa mataifa umeielezea hali hiyo kuwa ni eneo la dharura kwa binadamu.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema kuwa mashirika ya kutoa misaada yanahitaji kupata hakikisho zaidi kutoka makundi ya wapiganaji kabla kupeleka misaada nchini humo.

AISHA MADINDA HUYOOO KWA CHOKI.....



Aliyekuwa mnenguaji mahiri wa bendi ya African Stars wana wa kutwanga na kupepeta Aisha Madinda amehamia rasmi bendi ya Extra Bongo kwa Mzee wa farasi Ally Choki na kuungana na mwalimu wa madansa Super Nyamwela kusongesha mzigo katika bendi hiyo inayokuja kwa kasi ya ajabu katika muziki wa Dansi Tanzania.





Kuna habari kuwa aliyekuwa mshindi wa kimwana manywele wa twanga pepeta kwa mwaka 2011 amechukua nafasi yake kwenye bendi hiyo kutokana na umahiri wake wa kudance.

HONGERA DIDA WA ''G''...........!!!!!!!!!!!!


Mtangazaji maarufu wa kipindi cha ‘Mitikisiko ya Pwani’ cha kituo cha radio cha Times FM Khadija Shaib ‘Dida wa G’ amefunga ndoa tena na mwanamume wake kipenzi aitwaye Gervas Mbwiga ambapo sherehe hizo zilifanyika  ukumbi wa New Msasani Club jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu kibao kutoka pande mbalimbali za jiji.






Picha kwa hisani ya Globalpublishers

MWANDISHI WA HABARI UINGEREZA AKUTWA AMEKUFA

Mwandishi wa zamani wa gazeti maarufu duniani la News Of The World (NOTW) Sean Hoare ambaye alivujisha kashfa iliyoliyolikumba gazeti hilo kujihusisha kunasa simu za watu mbali mbali amekutwa amekufa nyumbani kwake nchini Uingereza.

Polisi nchini imesema mwili wa Hoare ulikutwa nyumbani kwake huko Watford siku ya Jumatatu asubuhi baada ya wasiwasi kuibuka kwa kutofahamu alipo na msemaji wa polisi wa kituo cha Hertfordshire amesema kifo hicho kinachukuliwa kama hakieleweki.

Hoare alidai katika makala yake kupitia gazeti la New York Times kuwa Andy Coulson ambaye kwa sasa ni msaidizi wa waziri mkuu wa Uingereza alimshawishi kunasa mawasiliano ya simu.

JENNIFER LOPEZ NA MARC ANTHONY WAJARIBU KUNUSURU NDOA YAO



Baada ya kutangaza kutengana wanandoa Jennifer Lopez na Marc Anthony wamekenda kufanyiwa ushauri nasaha wakihaha kujaribu kunusuru ndoa yao.

Wanandoa hao ambao walitangaza kutengana siku ya Ijuma lakini watu wao wa karibu wamesema kuwa wamekuwa na msuaguano wa muda mrefu.



Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinasema kuwa Jennifer amejitahidi kwa uwezo wake kuifanya ndoa hiyo idumu kwa kwenda katika vituo mbalimbali vya ushauri nasaha na alikuwa mvumilivu na mwenye mapenzi na kufanya chochote alichioambiwana mumewe lakini sasa amechoshwa.

50 CENT KUSAIDIA WENYE SHIDA



Rapa 50 Cent ana nia ya kutumia nafasi yake pamoja na ushawishi alionao katika jamii kuwasaidia wenye shida na tayari ameshajiwekea lengo la kuwalisha waafrika bilioni moja.

Mkali huyo wa muziki warap ulimwenguni alibadili maisha yake kutoka uuzaji wa dawa za kulevya Jijini New York na kuwa miongoni mwa wasanii wakali wa hip hop na kupata pesa nyingi tangu mwaka 2003.


Na sasa nyota huyo wa muziki wa hip hop anataka kugawana na wenye shida kipato chake kwa kutilia mkazo ndoto yake ya kuwasaidia watu wenye njaa barani Afrika.

LADY GAGA AKABILIWA NA WAHALIFU WA MTANDAO


Nyota wa muziki nwa mwanamapinduzi wa mitindo ambaye haishiwi vituko Lady gaga amewaita polisi baada ya wahalifu wa mtandao ''maharamia'' kuishambulia tovuti yake binafsi na kuiba taarifa za mashabiki wake.

Tovuti hiyo ya Gaga imevamiwa na maharamia hao wa mtandao ambao wamechukua taarifa za siri za mashabiki zikiwemo majina yao na anuani za barua pepe zao.

Wawakilishi wa Lady Gaga wamesema wahalifu wameiba taarifa zilizokuwepo kwenye database ya tovuti zikiwemo za majina yote mawili ya baadhi ya mashabiki wa msanii huyo.