.

Monday, May 9, 2011

ALIYEDAI KUBAKWA LIBYA, AFIKA TUNISIA

Eman al-Obeidi, ambaye aliingia ghafla kwenye hoteli moja mjini Tripoli iliyokuwa imejaa waandishi wa habari wa kigeni na kudai kubakwa na wafuasi wa kanali Muammar Gaddafi, amekimbia na kuelekea Tunisia.
 
Bi Obeidi aliliambia shirika la habari la CNN alivuka mpaka siku ya Alhamis, akisaidiwa na maafisa wa kijeshi walioasi.
Alisema aliondoka Tripoli kwa gari akiwa amefunikwa kichwa huku jicho moja tu likibaki wazi.
Mwezi Machi, aliwaambia waandishi wa habari alishikiliwa kwa siku mbili na kubakwa na askari 15 wanaomtii kiongozi wa Libya.
Tukio hilo lilipata umaarufu mkubwa tangu ghasia kuanza nchini humo, lakini kumekuwa na ripoti nyingine nyingi za ubakaji kama silaha ya vita kulingana na waangalizi.
Picha za kuondolewa kwa nguvu kwa Bi Obeidi kutoka hoteli ya Rixos na maafisa wa usalama wa Libya zilionyeshwa Machi 26 na kushuhudiwa na ulimwengu mzima.
Serikali ya Libya imekana kuwa mwanamke huyo alibakwa, na wanaodaiwa kumshambulia wamefungua kesi kwa madai ya kuwakashifu.
Kulingana na CNN Bi Obeidi ameripotiwa kupelekwa ubalozi wa Ufaransa mjini Tunis mwishoni mwa juma.

"JAMANI SIOI MAPEMA KAMA MNAVYONADHANI".

Chris Brown kuptia mtandao Twitter alizima uvumi uliokua umezagaa kuwa alimuomba mpenzi wake waoane wakati wa sikuu za Easter...


CHRIS BROWN AKIWA NA 'DEM WAKE' KARRAUCHE TRAN

Chis Brown inasemekana kuwa alimuambia dem wake Karrauche Tran kupitia kwenye simu kuwa anamuomba waowane lakini hakuwa na pete kwa wakati huo na mdada huyo kukubali,lakini Chris Brown akafunguka kuwa yeye ni mdogo sana kujihusisha na hizo issue za kuoa kwa sasa coz ndio kwanza ana miaka 21 tu!

MUTHARIKA: NILIOGA MATUSI KUTOKA KWA BALOZI WA UINGEREZA

Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, ameeleza sababu ya kumfukuza balozi wa Uingereza mwezi uliopita.
 
Katika taarifa yake ya mwanzo kuhusu ugomvi huo, Rais Mutharika alisema Balozi Fergus Cochrane-Dyet alimtusi, na hayuko tayari kukubali hayo, eti kwa sababu Malawi inapata msaada wake mkubwa kabisa kutoka Ukngereza, kushinda nchi nyengine.
Magazeti yalichapisha barua iliyofichuliwa, ambamo Balozi Cochrane-Dyet alimuelezea Rais Mutharika kuwa anaongoza kimabavu, na hakubali kukosolewa.
Uingereza ilimtaka balozi wa Malawi aondoke London, kujibu kufukuzwa kwa Bwana Cochrane-Dyet kutoka Malawi.

MBABE WA MUAMED ALLY AFARIK DUNIA.

Bingwa wa zamani wa uzito juu mkongwe Sir Henry Cooper, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76 nyumbani kwa mwanawe Oxted, Surrey.

Bingwa huyo wa Uingereza, Jumuia ya Madola na Ulaya, alipigana mara 55 na anakumbukwa sana katika pambano lake la mwaka 1963 alipomsukumia konde lililomuangusha chini Muhammad Ali - wakati huo akiitwa Cassius Clay.
Katika taarifa yake, Ali alisema amempoteza "rafiki yake wa zamani", akimuita, "mpiganaji hodari na muungwana".
Cooper aliyezaliwa London, aliwahi kushinda tuzo ya Mwanamichezo Bora wa mwaka mara mbili, alitunukiwa cheo cha Sir mwaka 2000.
Pamoja na mabondia wengine hodari wa Uingereza akiwemo Frank Bruno, Tommy Farr na Lennox Lewis, Cooper anaaminika ni bondia hodari Uingereza kuwahi kumpata katika uzito wa juu.
Baada ya kucheza ngumi za ridhaa ikiwemo michezo ya Olympiki ya Helsinki mwaka 1952 akiwa na umri wa miaka18, Henry na pacha wake George, aliyefariki dunia mwaka jana, wote waliamua kujiunga na ngumi za kulipwa wakiwa na umri wa miaka 20 mwaka 1954.
Aliendelea kucheza kwa mafanikio katika ngumi za kulipwa, lakini hakuwahi kushinda taji la dunia hadi alipostaafu akiwa na umri wa miaka 36, mwaka 1971 baada ya kutwangwa na Joe Bugner mwaka mmoja baadae baada ya kutangazwa na BBC kuwa ameshinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka mara mbili, mwaka 1967 na 1970.
Cooper, atakumbukwa sana kutokana na mapambano yake mawili na Ali miaka ya 1960.
Alimuangusha chini kwa konde zito la kushoto lililopewa jina la jina 'Enry's 'Ammer - ukiwa ni umaarufu wa konde lake la kushoto - lakini Ali baadae akashinda pambano hilo lisilokuwa la ubingwa mwaka 1963 katika uwanja wa Wembley.
Ali baadae alizungumza kupitia televisheni ya Uingereza kwamba Cooper "alinipiga ngumi kali hadi wazee wangu Afrika nao wamepata habari".
Akielezea juu ya kifo cha Cooper, Muhammad Ali amesema, "ameishiwa maneno ya kusema" kutokana na kifo cha rafiki yake.
"Henry kila wakati alikuwa na sura ya kutabasamu kwangu; ni tabasamu ya unyeyekevu na upendo", alisema Ali. "Ilikuwa ni jambo jema kuwa karibu na Henry. Nimempoteza rafiki yangu wa zamani. Alikuwa ni bondia hodari na muungwana."

"TUPENI UBINGWA WETU JAMANI"

Manchester United inahitaji pointi moja kutangazwa bingwa wa ligi kuu ya England, baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya Chelsea kwa mabao 2-1.
Magoli ya Havier Hernandez katika dakika ya kwanza na bao la kichwa la Nemanja Vidic yaliipa ushindi muhimu kwa Manchester United kusogelea ubingwa.
Goli pekee la Chelsea lilifungwa na Frank Lampard.
United walitawala zaidi kipindi cha kwanza, huku Chelsea wakipigana kufa na kupona katika kipindi cha pili.
Man United itakutana na Blackburn Jumamosi ijayo.

BABA HAJI ATOA TALAKA BILA KIFICHO.

Haji Adam au Baba Haji a.k.a "Peoples Choice"  wa pili kushoto waliokaa, nguli wa kiwanda cha filamu bongo, tarehe 7/5/2011 ametoa rasmi talaka kwa mzazi mwenziye baada ya kutoelewana kwa kipindi kirefu. Akiongea kwa jazba mzazi mwenziye huyo aliyezaa naye mtoto mmoja na Haji, alilamika kua hapati matunzo mazuri kutoka kwa mumewe huyo kwa kipindi kirefu sasa. Kwa upande wa Baba Haji yeye alisema si kweli maneno ya mzazi mwenziye kwani amekua akimhudumia kama mke halali kabisa wa ndoa kama diani yake inavyoamuru.
 Hata hivyo pamoja na kupewa talaka hiyo, mzazi huyo alisema sakata halitaishia hapo kwani atafanya kila mbinu kumchafua mzazi mwenziye huyo kwenye vyombo vya habari ili kumshikisha adabu.
 Baba Haji naye akajibu hatojali hata alienda wapi kwani ameshatoa talaka ametoa, anachoangalia sasahivi ni masomo yake.