.

Tuesday, May 10, 2011

"MATAJIRI MJIANDAE KWA KIBANO.

WAZIRI Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe amesema katika Bajeti ijayo ya Serikali, atapendekeza matajiri wabanwe ili kupunguza makali ya maisha kwa Watanzania walio wengi ambao kwa sasa wanataabika kutokana na umaskini.

Alisema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mbarali, mjini Rujewa, akisisitiza kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kutatua matatizo ya ugumu wa maisha yanayowakabili Watanzania.
"Tofauti ya kipato Tanzania inakuzwa na sababu mbili, moja ni matajiri kuzidi kuwa matajiri na maskini kuendelea kuwa maskini, hivyo hatua za kisera zinapaswa kuchukuliwa kuwazuia maskini kuwa maskini zaidi kwa kuwapunguzia gharama za maisha," alisema Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema).
Alisema katika Bajeti ijayo, atapendekeza kuziba pengo la kodi kwa kupandisha kodi ya kampuni kufikia asilimia 35, kuuza hisa za serikali katika kampuni za Airtel, NBC na BP hivyo kupunguza misamaha ya kodi hadi kufikia asilimia moja ya pato la taifa
.

HUU SASA UBAGUZI WA RANGI.

Waziri wa michezo wa Ufaransa amemwondolea lawama kocha wa timu ya taifa ya soka nchini humo Laurent Blanc kuhusiana na ubaguzi wa rangi, baada ya kocha huyo kupendekeza kupunguza idadi ya wachezaji weusi katika timu ya taifa.
Waziri huyo, Chantal Jouanno amesema hakuna ushahidi kwamba Blanc alivunja sheria yoyote kwa kujadili kupunguza idadi ya wachezaji weusi na wale wenye asili ya Afrika Magharibi, wanaojumuishwa katika timu za vijana za Ufaransa.
Blanc amejitetea kwamba alieleweka vibaya.
Kocha huyo pamoja na makocha wengine wa timu za vijana walikuwa wanajadili jinsi ya kuwazuia kwenda kuchezea nchi zingine wachezaji wanaokuzwa nchini Ufaransa.
Bi Jouanno amesema hatma ya mkurugenzi mkuu wa mafunzo katika timu ya taifa Francois Blaquart ambaye alisimamishwa kazi kufuatia kujitokeza kwa habari hizo itaamuliwa na shirikisho la soka la Ufaransa (FFF).
Shirikisho hilo lilitazamiwa kutoa taarifa za uchunguzi wake Jumanne alasiri.
Mapendekezo hayo yamezua tafrani katika shirikisho la soka la Ufaransa, ikiwa bado haijapita mwaka tangu Laurent Blank alipoajiriwa kujenga upya timu ya taifa, baada ya matokeo mabaya kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka uliopita nchini Afrika Kusini.
Wavuti wa taarifa za uchunguzi wa kisiri- Mediapart, ulichapisha taarifa kudai Blaquart alipendekeza kupunguzwa kisiri idadi ya wachezaji weusi na wale wenye asili ya Afrika Magharibi hadi kubakia asilimia 30 kwenye baadhi ya vituo vya kutoa mafunzo kwa vijana chipukizi, kikiwemo kituo mashuhuri cha Clairefontaine.
Ilidaiwa Blanc alikubaliana na mpango huo ili kukuza zaidi wachezaji wenye ''utamaduni na histoaria'' ya Wafaransa.
Wakati wa Kombe la dunia wachezaji wapatao tisa katika timu za nchi zingine walikuwa ambao waliwahi kuichezea timu za taifa za vijana nchini Ufaransa.

HIZI NDOTO JAMANI! KILA MTU ATAOTA.

MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa ameoteshwa na Mungu kutoa dawa kwa njia ya kikombe kutibia wagonjwa wenye maradhi sugu.
Dawa hiyo amedai Mungu amemuotesha kutoa dawa ambayo ni maji ya kisima, bomba na haichanganywi na chochote zaidi ya maji hayo.

Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.

Awali imedaiwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya ukonda katika daladala na hivi karibuni ameibuka na kudai kuwa ameoteshwa.

Kufuatia taarifa hiyo watu wameanza kujitokeza nyumbani kwa kijana huyo kupata kikombe cha dawa hiyo huku akiwa ameshika msaahafu mkononi.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Temeke, wanafanya jitihada za kufanya mahojiano maalum na kijana huyo na taarifa itatolewa kwenye vyombo vya habari.

Kijana huyu ni wa saba kujitokeza na kudai wameoteshwa na Mungu na wengine wamejitokeza katika mkoa wa Mbeya, Moshi, Mbeya, Iringa, Tabora na Morogoro, Pwani wote wakidai kuoteshwa na Mungu kutoa tiba kwa njia ya kikombe.

HUYU NDIYO MTOTO WA KICHINA JAMANI.

Mtoto Lu Hao wa nchini China pamoja na kwamba ana umri wa miaka 3 ana uzito ambao ni mara tano zaidi ya uzito wa mtoto wa umri wake, ana jumla ya kilo 60. Lu Hao, mtoto wa miaka mitatu wa nchini China, alizaliwa akiwa na uzito usiozidi kilo 2.5 lakini hivi sasa ana uzito ambao ni sawa na uzito wa watoto watano wa umri wake wakiwekwa pamoja.

Uzito wa Lu Hao mbali ya kuwashangaza wazazi wake, umewashangaza pia madaktari wa nchini China ambao wameshindwa kujua nini kimemsibu mtoto huyo.

Wazazi wake wamejaribu kila njia ya tiba ya mtoto huyo bila mafanikio na majaribio ya kumlazimisha Lu Hao kula kiasi kidogo cha chakula yamefeli kutokana na mtoto Lu Hao kuangua kilio muda wote mpaka anapopewa chakula chake.

Katika mlo mmoja mtoto huyo huweza kufagia sahani kadhaa za wali na nyama.

"Inatubidi tumuache awe jinsi anavyotaka, tunapomnyima chakula huangua kilio bila kupumzika", alisema mama yake Lu Hao, Chen Yuan.

"Katika mlo mmoja, humaliza sahani tatu kubwa za wali", alisema baba wa mtoto huyo na kuongeza "Tusipompa chakula hufanya vurugu na kuangua kilio siku nzima".

Mtoto Lu Hao anapenda kuogelea lakini hapendi kutembea hali iliyowafanya wazazi wake wawe wanampeleka shule ya chekechea kwa pikipiki.

Wazazi wake wamemtengenezea sehemu ya mazoezi ambapo kila wanapomlazimisha kufanya mazoezi ndivyo anavyosikia njaa zaidi na kula sana na hivyo kuzidi kunenepa.

"JAMANI CONDOM ZIKO WAPI?


Huku Serikali ya Kenya ikiimarisha kampeni dhidi ya UKIMWI, mbinu moja imekuwa kuhamasisha jamii kuhusu kinga kwa kutumia mipira ya kufanyia mapenzi, CONDOM. Kinga hii imefanikiwa katika maeneo ya mijini.
Hata hivyo hali ni tofauti vijijini. Miongoni mwa jamii ya wafugaji, Condom imekuwa ni bidhaa nadra sana kupatikana, hali inayowafanya kutumia njia mbadala, baadhi zikiwa hatari kama alivyogundua Ng'endo Angela alipozuru eneo la Isiolo Mashariki mwa Kenya.

NOELLE AUZA BIKIRA YAKE KWA SHILINGI MILIONI 100.

Mwanafunzi mmoja wa kike wa nchini Ubelgiji mwenye umri wa miaka 21 ameinadi bikira yake na kufanikiwa kupata mteja aliyeinunua kwa takribani Tsh. Milioni 100.
  Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina moja la Noelle aliunadi mwili wake kwenye mnada wa tovuti ya Yantra ya mjini Amsterdam, Uholanzi ambayo inadili na kuwatafutia wanaume wanawake.

Noelle ambaye ni mwanafunzi anayeishi nchini Ubelgiji, aliamua kuinadi bikira yake nchini Uholanzi huku akificha sura yake ili wazazi wake na marafiki zake wasimgundue.

Baada ya miezi miwili ya mnada huo hatimaye mnada huo umeisha kwa Noelle kufanikiwa kuiuza bikira yake kwa euro 50,000 ambao ni zaidi ya Tsh. Miloni 105.

Noelle atatumia masaa 24 na mwanaume aliyeshinda mnada huo ambaye hajataka kujitambulisha.

Mwanaume huyo mbali ya kupata nafasi ya kuivunja bikira ya kimwana huyo atatakiwa kama sharti la mnada huo ampeleke Noelle kwenye mgahawa wowote ambao Noelle atauchagua.

Noelle anasema kuwa mshindi wa mnada huo atapewa cheti cha daktari kinachothibitisha kuwa Noelle ni bikira. Noelle alisisitiza kuwa tendo la ngono lazima lifanyike kwa kutumia kondomu.

Noelle alidai kuwa aliamua kuinadi bikira yake ili aweze kupata pesa za kujikimu kwenye masomo yake.

Noelle alijinadi kwenye mnada huo kwa kusema kuwa yeye ni mrembo mwenye macho ya hudhurungi, urefu wa mita 1.73, kiuno cha saizi 10 na matiti ya saizi B.

"Mimi ni msichana wa kawaida na wazazi wangu hawatafurahia wakisikia ninainadi bikira yangu", alisema Noelle.

Bei ya kuanzia kuweka dau katika mnada huo ilikuwa ni euro 5,000 (Tsh. Milioni 11).

Katika kuwadhirihishia watu kuwa yeye si kahaba, Noelle alidai kuwa atatoa asilimia tano ya pesa atakazozipata kwa mashirika ya hisani.

ANCELOTTI APATA MKOMBOZI.

Meneja msaidizi wa zamani wa Chelsea Ray Wilkins, amesema meneja wa Chelsea anayekabiliwa na chagizo kubwa la kuondolewa, Carlo Ancelotti hapaswi kutimuliwa mwishoni mwa msimu huu wa ligi.
 
Mustakabali wa Ancelotti unatokana na tetesi nyingi zinazoenea hivi sasa baada ya Chelsea kumaliza msimu mikono mitupu.
Lakini Wilkins aliiambia BBC Radio 5: "Sidhani kama klabu inahitaji mabadiliko ya haraka... lakini kwa hakika wachezaji wapya ndio wanahitajika kuongeza nguvu katika kikosi kilichopo.
"Mabadiliko ya jumla, kwa kuanzia kwa kocha, itakuwa ni makosa makubwa."
Chelsea inajiandaa kumaliza msimu bila kombe lolote baada ya kuchapwa na Manchester United siku ya Jumapili, wakiwa na matumaini ya kumaliza nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya England.
United pia iliiondoa Chelsea katika mashindano ya ligi kuwania Ubingwa wa Ulaya mwezi wa Aprili.
Meneja wa zamani wa Chelsea Guus Hiddink, aliyeiongoza klabu hiyo kuchukua kombe la FA mwaka 2009, amekuwa akitajwa-tajwa huenda akarejea Stamford Bridge, ingawa kocha huyo Mrusi inaarifiwa hapendelei kazi hiyo.
Waholazi wawili Marco van Basten na Frank Rijkaard pia wametajwa kuwa nao wanaweza wakapewa kazi ya kuinoa Chelsea msimu ujao, pamoja na Andre Villas-Boas, aliyeiwezesha Porto kufika hatua ya fainali ya Europa msimu huu.
Mwengine anayehusishwa kupewa kazi ya kuifundisha Chelsea ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Gianfranco Zola aliyewahi kuwa meneja wa West Ham.
Ancelotti, ambaye mkataba wake umesalia mwaka mmoja, alikiri siku ya Jumatatu kwamba timu yake haikuwa imara msimu huu, lakini akakanusha mabadiliko makubwa yanahitajika katika kikosi chake.