.

Thursday, March 24, 2011

Simanzi kubwa...

Katika siku ambazo tumekumbwa na majonzi ni pale tulipopata taarifa za ajali mbaya iliyotokea mjini Morogoro na kusababisha vifo kwa wasanii 13 wa 5 Star Modern Taarab. Hili ni pigo kwa wengi hasa wapenzi wa muziki wa Taarab. Wengi wetu tumejiuliza ni nini tulichomuudhi mwenyezi Mungu kufikia kupata pigo kubwa namna hii.

Yote ni kumshukuru na kumuomba Mungu kila siku kwani hakuna ajuae siku itakayomfika mauti.

inna lillahi wa inna ilaihi rajioon

MWENYEZI MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI. AMIN

Siku miili ya marehemu ilipowasili hali ilikuwa tafrani...
Isha Mashauzi akilia kwa uchungu kwa kupoteza wafanyakazi wenzie

Hawa ni baadhi tu ya ndugu wa marehemu akiomboleza

Maiti zikipandishwa kwenye gari kwenda mazikoni ambapo wengine walizikwa bila baadhi ya viungo vyao...

Na hivi ndivyo basi walilosafiria lilivyokuwa upande mzima ulikatika...

Thursday, March 17, 2011

Kwikwi...

Wadau wa blog ya Yaliyomo Yamo tunaomba radhi kwa kutokuwepo hewani kipindi kirefu ni kutokana na kwikwi za kiufundi. Tunarekebisha mitambo hivyo tutarudi hewani siku za karibu...

Wednesday, March 9, 2011

WANAWAKE TUACHE TABIA ZA KUWAKOMOA WANAUME


     Kunabaadhi ya wanawake wamekuwa na tabia za ajabu  endapo mwanaume atamtamkia kuwa anamuitaji kimapenzi. Ukweli ni tabia mbaya sana kwani unamkomoa hujuwi analengo gani kwako  inawezekana akawa mumeo badae  na wewe ulishamkomoa siku za nyuma. Labda utajiuliza kumkomoa mwanaume kwa njia gani ?   Unamkuta mwanamke anaitwa  sehemu na mpenzi wake ambae wanaanza mapenzi basi anawapitia shoga zake na kwenda sehemu alioitwa akifika watakula na kunya bila kujuwa yule kiumbe wawatu kama anapesa au hana , ukweli si vizuri kufanya hivyo kwani uko ni kumkomoa  wanaume na kuomba pesa mara kwa mara  .Achani kuwakomoa wanaume na kama humtaki basi acha kumbomoa  tabia mbaya wanawake wenzetu  tubadilike.  Kwaleo tuishie hapa

MAMBOYOTE LOLIONDO

 JAMANI KAMA MGONJWA WAKO YUKO HOSPITAL USIMKATISHE MATIBABU
Loliondo hapatoshi kama utakuwa mfatiliaji mzuri wa vyombo vya habari hili si jambo  geni kwako .Loliondo kwa Mchungaji  mstaafu Ambilike Ambwakise  kwa kupata  dawa ya mitishamba na kupona  pia dawa hiyo huambatana na maombi  kwa imani yako utapona . watu wengi wamejitokeza na kukimbilia kwa baba  ukweli foleni haifai na tiba inatolewa kwa kiasi kidogo cha pesa shilingi 500 tu.

Jamani wagonjwa tuko wengi  wote hawa wanasubiri huduma

hapa dawa inaandaliwa
 
Hapa dawa ipo tayari kwa  kunywa


Tuesday, March 8, 2011

MAPACHA WATATU WAOMBA KURA ZENU

Hawa ndio mapacha watatu Jose Mara, Khalidi Chokoraa, Kalala Juniour

 Wakiwa mzigoni

Moja kati ya  vipande vya picha ya video ya wimbo wa shika ushikapo ,ambao uko katika category ya best swahili song of the year katika tuzo za kill music  2011....Ili kufanikisha vijana hawa kunyakua tuzo hiyo wapigie kura kwa kutuma sms yenye maneno G173 kwenda 15747.......
Kumpigia kura khalid Chokoraa kupata tuzo ya rapa bora wa bendi tuma sms andika M 110 kwenda 15747...
TUWAPE SUPPORT YA KUTOSHA JAMANIIIIIIIIIIII