.

Monday, May 2, 2011

UNATAKA KUTOA TALAKA? KEKI HII HAPA.

TABASAMU LA MWAKA.

OSAMA AUWAWA.

Mwanzilishi na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Osama Bin Laden ameuwawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan, rais Obama amesema.
Kiongozi huyo wa al-qaeda aliuwawa katika operesheni ya ardhini nje ya mji wa Islamabad kwa mujibu wa taarifa za kijasusi.
Bw Obama amasema baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani ilichukua mwili wake.
Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ukatili ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington, mnamo Septemba 11, 2001.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa kundi la al-qaeda lakini kuelezea hofu kuwa huenda wakashambuliwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.
Bw Obama anasema alielezea Agosti, mwaka uliopita, kuhusu kule Osama Bin Laden amejifisha. Kufuatia uchunguzi wa ujasusi waligundua amejificha mjini Pakistan.

Wiki iliyopita rais Obama alitoa amri kwa operesheni kufanyika ''kumsaka Bin Laden'' . Bw Obama amesema operesheni hiyo iliendeshwa na kundi ndogo la wanajeshi wa Marekani katika eneo la Abbottabad, Kaskazini mwa Islamabad.

''Baada ya ufyatulianaji wa risasi, Bin Laden aliuwawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani'' rais Barack Obama amesema. 

KUMBE KUSMA NI KUDHOHOFISHA AKILI!

WASOMI zaidi ya 1,200 katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wamesimamishwa masomo baada ya juhudi za kushinikiza madai yao kugonga mwamba.
Wasomi hao wanalilia vitendea kazi, zikiwamo laptop (kompyuta) ili ziwawezeshe kuendana na dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia.
Niliposikia madai yao sikushangaa. Sikushangaa kwa sababu tumekubali kuwa na jamii inayotaka ilimiwe mashamba, ipandiwe, ivuniwe, iandaliwe chakula, ilishwe; na ikiwezekana isaidiwe kujisaidia, na hata ikibidi kuzoa uchafu, basi wawepo wazoaji!
Sikushangaa kusikia madai ya kutaka “vitendea kazi”, lakini nilipigwa na bumbuwazi kusikia aina ya madai! Madai yao yamenifanya niingie kwenye maduka kuangalia bei za laptop.
Nikaangalia bei ya laptop mpya na zilizokwishatumiwa Ulaya na Marekani. Nikakuta bei ya laptop mpya inaanzisha Sh 700,000. Mitumba inauzwa Sh 400,000 hadi Sh 500,000.
Wasomi wetu wamekuwa na hiari ya kurejea makwao kwa sababu Bodi ya Mikopo imeshindwa kuwapa mikopo kwa ajili ya kununua vifaa hivyo.
Aidha, madai yao yalikolezwa chachandu ya kauli wanayosema ilitolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ya kupewa kompyuta hizo.
Februari, mwaka huu niliandika makala ya kuwaunga mkono Wachina walioingia kwa wingi, si Tanzania tu, bali katika kila nchi katika dunia yetu.
Tunaweza kudhani kuwa wingi wa Wachina hapa nchini unatokana na wingi wao, lakini ukweli ni kwamba ndani ya mioyo na akili za Wachina, kuna kitu cha ziada kinachowafanya wawe wa kugaagaa na upwa!
Wachina wameujua ujasiriamali. Wametii miiko na taratibu zake. Wanajua hawana nafasi ya kwenda kula na kuishi kwa mjomba wala kwa jirani.
Maisha ya Mchina yanatokana na juhudi zake binafsi na nyongeza ya mazingira mazuri ya kuwezeshwa yaliyowekwa na Serikali yao.
Nimepata kuzungumza na Wachina kadhaa wanaofanya kazi ya kusukuma mikokoteni pale Kariakoo jijini Dar es Salaam. Nimezungumza na Wachina wanaofanya kazi nyingi za uchuuzi katika maeneo mbalimbali nchini.
Kati ya wote hao, nilibaini kuwa mwenye elimu ya chini ana elimu ya juu ya sekondari. Huyo ndiye hakusoma. Wengi wana shahada za uzamili na uzamivu.
Fikiria, mtu mwenye shahada ya uzamivu anajishusha hata kukubali kusukuma mkokoteni ili aweze kutengeneza maisha yake. Tena, basi, Wachina wangependa kuona muda wa kufanya kazi, muda wa kufungua na kufunga maduka unakuwa saa 24. Hawataki kupumzika.
Turejee kwa wasomi wetu wa Dodoma. Kudai laptop leo ni aibu kwa msomi wa chuo kikuu. Kudai laptop inayouzwa Sh 500,000 kwa mtu aliyefikia ngazi hiyo ya elimu, ni upuuzi usiokubalika.
Wasomi wa Tanzania ndiyo pekee ambao wakiwa katika vyuo vikuu, hawataki kujishughulisha na kazi za kuwaingizia kipato.
Wasomi wetu wakiingia katika vyuo vikuu wanabadilika na kujiona kuwa na haki ya kutendewa zaidi kuliko kutenda. Usomi ni ubwana na ubibi. Ni u-mangimeza.
Wasomi wa vyuo vya elimu ya juu wanapaswa wabadilike. Waingie madarasani kama kawaida, lakini wawe na muda wa kufanya kazi za ziada za kuwaingia mapato.
Haya ninayoyasema hapa yanafahamika vema mno na Watanzania waliokwenda kusoma ng’ambo. Wengi wanaokwenda huko wanajilipia ada.
Wanajilipia ada kwa ujira wanaopata kutokana na kazi za kuosha sufuria, kusafisha vyoo, kusafisha mabanda ya wanyama, kuchuma matunda, kutunza wazee, kujfagia barabara na kadhalika.
Kwa bahati nzuri kazi mbaya mbaya Ulaya na Marekani malipo yake ni manono. Pengine wasomi Watanzania kwa kutambua kuwa wapo mbali na nyumbani kwao, na hakuna anayewatambua kwa sura, hukubali kuzifanya kazi hizo na kujipatia fedha nyingi.
Tunapoona nyumba au magari ya wasomi wetu walio ughaibuni, tutambue kuwa fedha zilizonunua vitu hivyo zimepatikana kwa shughuli kadha wa kadha, zikiwamo za kuwaosha vikongwe!
Suala la kujitafutia fedha kwa ajili ya maendeleo si la kuonea aibu. Wasomi wetu wa Dodoma na kwingineko nchini hawapo tayari kutumia muda usio wa masomo kufanya kazi ya mapokezi katika hoteli, kufuga kuku, kuuza baa au hotelini, kufagia barabara wala kufanya shughuli yoyote halali ya kuwaingizia fedha.
Matokeo ya malezi haya hatari ndiyo haya tunayoona sasa. Wanafunzi wanadai hata laptop ambazo kimsingi wangeweza kujibidisha wenyewe na kupata fedha za kuwawezesha kuzinunua.
Elimu bado haijawasaidia wasomi wa Tanzania. Kwa Tanzania heri ambaye hakusoma kuliko mtu aliyepata elimu ya chuo kikuu. Wakati wa mgawo mkali wa umeme mwezi Januari na Fabruari mwaka huu nilijifunza kitu kingine kwa wasomi wetu.
Barabara yangu ya kwenda na kutoka kazini ni ile ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Chuo kile kina mandhari nzuri, pengine kuliko chuo chochote katika Afrika. Wakati wa mgawo wa umeme usiku, chuo kile kinatisha! Kinatisha kwa giza nene kutokana na misitu mingi na mizuri iliyokizunguka.
Ajabu ni kwamba nilipokuwa nikipita katika chuo hicho, sikuona dalili yoyote ya mwanga, si kwenye ofisi za maprofesa na madktari, wala katika mabweni yaliyosheheni maelfu ya wanafunzi.
Katika hali ya kawaida ya usomi, chuo kikuu ndio ingekuwa sehemu ya mwisho ya watu kulalamika kukosa umeme. Maelfu ya wanafunzi wanaolala kwenye mabweni yake ni hazina kubwa ya kupata umeme.
Kinyesi kinachotoka kwenye mabweni yale ni chanzo muhimu sana cha nishati. Katika hali ya kawaida ya usomi uliotukuka, sisi wapita njia tungepata faraja kuona umeme ukiwaka kwenye vyumba vya wasomi hao.
Umeme huo ungetokana na nguvu za kinyesi kinachozalishwa na wanafunzi hao. Umeme ambao ungezalishwa hapo bila shaka ungekuwa na uwezo wa kuwasha taa katika vyumba na ofisi zote bila kuwasha viyoyozi.
Sikuwasikia wasomi wetu wa sayansi wakiomba japo fedha za kuwawezesha kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia hiyo ambayo ni nyepesi mno.
Sikuwasikia wala wakijadili namna ya kupata fedha za kuwawezesha kufunga vifaa vya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za jua.
Maisha ya msomi yanapokuwa ya kijima, sawa na ndugu zetu waishio vijijini, hakuna maana ya kuwa na wasomi. Maisha ya msomi yanapaswa yaonyeshe tofauti kati yake na mtu ambaye hakupata elimu. Kama mwananchi kijiji mwenye ng’ombe wawili anaweza kupata umeme kwa kinyesi cha ng’ombe, iweje hawa wasomi maelfu kwa maelfu kinyesi chao kisitumike kuwasha japo balbu moja?
Kwa wasomi wa Dodoma, kama kweli Waziri Mkuu aliwaahidi kuwa watapata mikopo ya laptop, alipotoka. Miaka minne katika chuo ni mingi. Watafute mashamba ya zabibu walime. Wauze baa wapate fedha.
Kila Jumamosi mjini Dodoma kuna mnada. Wauze nyama na vinywaji vingine ili wajipatie fedha zitakazowawezesha kujinunulia vitu kama laptop.
Serikali ibaki na dhima ya kuhangaikia mambo makubwa makubwa ya majengo, wahadhiri, vifaa vya kujifunzia, fedha za mafunzo kwa vitendo na kadhalika.
Wasomi waingie mitaani wachape kazi kwa bidii kubwa. Wasomi waache kudeka. Wao si watoto wadogo. Wafanye kazi za ziada.
Wapo waliothubutu kufanya hivyo, na mambo yamewaendea vizuri. Bila kubadili tabia hizi za kipuuzi, wasomi wetu watakuwa hawana tofauti na walemavu wanaostahili kutunzwa na jamii.

GADDAFI ANATAKA MAZUNGUMZO

Katika hotuba yake Jumamosi asubuhi, kiongozi wa Libya alisema yuko tayari kutoa amri kuwa mapigano yasitishwe na kuanza mazungumzo, endapo NATO itaacha mashambulio ya mabomu.
Lakini alikataa lile dai kubwa la wapiganaji na jumuiya ya kimataifa, kwamba yeye aondoke.
Alisema hatong'atuka wala kuihama Libya.
Wengi serikalini wanaona kuwa wameshakaribisha mazungumzo kwa kukubali mpago wa Umoja wa Afrika wa kurejesha amani; lakini wanahisi upinzani ndio hautaki kumaliza mapigano, kwa sababu unakataa kuzungumza na serikali ya Kanali Gaddafi.
Alipokuwa Kanali Gaddafi anazungumza, NATO ilidondosha makombora matatu mjini Tripoli, kwenye yale yaliyoonekana kama majengo ya serikali.
Hotuba ya Kanali Gaddafi, ilikuwa mchanganyiko wa kukaza na kulegeza kamba.
Alisema kila mwananchi wa Libya sasa anakabili mambo mawili : uhuru ama kifo.
Hakuna kusalliam amri, hakuna hofu wala kuondoka.

BIASHARA YA UTUMWA BADO IPO AFRIKA.

Kampuni moja nchini Uganda, inayojulikana kama Uganda Veterans Development Ltd ilikuwa inatafuta wanawake wa kwenda kufanya kazi katika maduka yaliyo ndani ya kambi za jeshi la Marekani nchini Iraq.
Hakusita na pamoja na wanawake wengine 146 wakatia saini mikataba.
Lakini alipowasili mjini Baghdad, aligundua kuwa kumbe kanunuliwa kama bidhaa na wakala mmoja wa Iraq kwa dola za kimarekani 3,500 sawa na pauni za Uingereza 2,200. Na kazi aliyoajiriwa kufanya ni mhudumu wa ndani kwa familia moja ya Iraq.
Kama wenzake, alilazimishwa kufanya kazi kwa saa nyingi, mara nyingi kuanzia alfajiri saa kumi na moja hadi usiku wa manane. Chakula alichopewa ni kidogo na maji pia ilikuwa shida huku akifungiwa ndani ya nyumba.
Kwa kauli yake, ameiambia BBC kuwa, nilikuwa na kibarua kwa sababu, unavyofahamu Iraq ni nchi yenye mchanga mwingi na hivyo vumbi huongezeka mara kwa mara, kwa hiyo inabidi ufagio usitoke mkononi, alisema Prossie.
Prossie alipojaribu kulalamika kuhusu kazi, aliambiwa na muajiri wake kuwa tumelipa fedha nyingi kukupata wewe na tuliambiwa kuwa nyinyi watu hamchoki wala maradhi hayawezi kuwapata. Kwa hiyo endelea kuchapa kazi.
Prossie alibakwa na mwenyeji wake ndani ya nyumba. Wanawake kadhaa kutoka Uganda waliozungumza na BBC walisema kuwa nao walibakwa pia.
Upande mwingine wa mkoa wa Baghdad, kwenye kituo cha jeshi la Marekani, mlinzi mmoja kutoka Uganda, Samuel Tumwesigye alisikia habari kuhusu yanayowasibu wanawake hawa.
Jitihada zake zikamwezesha kupata simu ya mwanamke anayejulikana kwa jina la Agnes, na kuwasiliana naye akiahidi kusaidia.
Tumwesige anasema kuwa "Jambo la kwanza nililofanya nilikwenda chumbani kwangu nikainama kumuomba Mungu, anisaidie nitekeleze hili nililolianza na nifanikiwe.
Alimuomba Agnes kama angeweza kutoroka kutoka nyumba hiyo na kwenda sehemu moja karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad panapojulikana kama Flying Man statue.

HI NI HATARI JAMANI

Dereva wa Tax akijaribu kurekebisha gari yake baadaya kuzimika wakati akijaribu kutoka kwenye kivuko cha Ferry. Hii ni hatari kwani anaweza kuhatarisha maisha yake na mali zake.

KILA KINYOZI ANA KINYOZI WAKE.

Aaron Ramsey akishangilia goli lake la pekee aliloifungia washika bunduki wa London Arsenal The Gunners dhidi ya wapinzani wao Mashetani wekundu Manchenster United. Ramsey ambaye alikua majeruhi wa muda mrefu na kuweza kuipatia timu yake goli pekee na la ushindi. Arsenal ilishinda 1-0