.

Friday, April 29, 2011

PWEZA IKER ATABIRI USHINDI MECHI YA MARUDIANO KATI YA MADRID NA BARCELONA

Pweza aliyepewa jina la Iker wa nchini Hispania ametabiri kuwa Real Madrid wataigaragaza Barcelona na hatimaye kufanikiwa kucheza fainali ya kombe la mabingwa wa ulaya.
Pweza huyo ambaye awali utabiri wake kwa mechi mbili za wababe hao wa Hispania ulikuwa wa kweli, ametabiri kwa mara nyingine kuwa Real Madrid watafanikiwa kuitoa Barcelona kwenye mechi za nusu fainali ya kombe la mabingwa ulaya.

Pweza huyo aliyepewa jina la Iker kwa heshima ya golikipa mkongwe wa Real Madrid, Iker Casillas alitabiri mechi mbili zilizopita za watani hao wa jadi ambapo ya kwanza walitoka sare ya 1-1 wakati mechi ya pili Madrid walishinda 1-0.

Pweza huyo mwenye uzito wa kilo 16 aliwekwa kwenye Aquarium kwenye mji wa Benalmadena uliopo kusini mwa Hispania ambapo alikimbilia kwenye sanduku lenye bendera ya Real Madrid na kuliacha sanduku lenye bendera ya Barcelona. Masanduku yote mawili yalikuwa na chakula kwaajili ya kumvutia Pweza huyo.

Madrid na Barcelona wanapambana kesho jumatano kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali itakayochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu wakati mechi ya marudiano itakuwa kwenye uwanja wa Barcelona, Nou Camp mnamo mei tatu.

Timu itakayofanikiwa kumtoa mwenzake itakutana na mshindi kati ya Manchester United ya Uingereza na Schalke 04 ya Ujerumani.

No comments:

Post a Comment