.

Tuesday, August 9, 2011

MUIGIZAJI NYOTA AFARIKI DUNIA...............


 Sam  loco efe ambaye ni comedian mzuri kutoka nchini Nigeria na kushiriki movie mbalimbali amefariki juzi akiwa chumbani kwake( hotelini) walipokuwa wameenda kurecord movie yao mpya.

Mbali na uigizaji pia alikuwa mtunzi, mwandishi wa script na ni muimbaji pia na anatambulika kama mmoja ya watu muhimu katika movie ya THING FALL APART ,wengi wetu tunaijua enzi za secondary

VODACOM MISS TANZANIA YAANZA KAMBI....................

Warembo 30 wanaotarajia kushindana katika mashindano ya Vodacom Miss Tanzania, wakiwa Makao Makuu ya Vodacom, Mlimani City, Dar es Salaam, wakijiandaa kwenda kuanza kambi yao katika Hoteli ya Giraffe.

Warembo 30 kutoka kanda tofauti nchini jana walianza rasmi kambi ya Vodacom Miss Tanzania 2011 kwa ajili ya fainali zilizopangwa kufanyika Septemba 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini.

Malkia wa Vodacom Miss Tanzania 2010, Genevive Mpangala (katikati) akigongeana glasi na warembo hao wanaoanza kambi leo

Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza amesema kuwa sababu kubwa ya kuanzisha utaratibu mpya ni kuwapa nafasi zaidi warembo hao kujifunza mambo mengi wakiwa kambini kama mashindano ya “Big Brother Africa”.

BONGO MOVIES WAKATAA KUBURUZWA............

Jacob Steven 'JB' mwenyekiti wa bongo movies club

Waigizaji nyota wa filamu wanaounda timu ya soka ya Bongo Movies wamesema hawataki kuburuzwa na mtu yoyote kwani biashara ya kazi zao ni ya hiari.

Wasaanii wa Bongo Movie kutoka kushoto JB,Steve Nyerere na Vicent Kigosi 'Ray'

Mwenyekiti wa bongo movies Jacob Steven maarufu kama JB kwa niaba ya wenzake amesema kuwa kuna migogorobaina ya wasambazaji wa kazi zao kutokana na kuoneana wivu wa kibiashara ambapo amesema wao kama wasaanii  wana hiari ya kuamua kazi zao zisamabazwe na nani lakini kuna watu wanapita mitaani na kueneza maneno ya uchonganishi kwa wasanii kwa maslahi yao binafsi.