.

Monday, May 23, 2011

"SHEIGH YAHAYA KAMA MFALME"

Mamia ya wakazi wa jijini Dar-es-salaam wakiusubiri mwili wa aliyekua Mnajim Mkuu Afrika Mashariki na Kati, Sheigh Yahaya Husein nyumbani kwake Magomeni Mwembechai, kwaajili ya kwenda kuuswalia Dua kabla ya kwenda kuuzika katika makaburi ya Tambaza jijini Dar-es-salaam. Kifo cha Mnajimu kilitokea wakati akiwa anapelekwa hospitalini Mt. Mkombozi Kinondoni Moroko akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo. Kijana ambaye jina lake halikufahamika mapema alisikika akisema "Sheigh Yahaya kama mfalme yaani umati wote huu!"


 Waombolezaji wakiupokea mwili tayari ya kuupeleka msikitini kwa maombi zaidi kabla ya maziko.      



Msafara ulianza kuelekea  msikitini

Mwili wa Mnajimu ukiwa tayari umeshaombewa dua tayari kwa maziko.





Vijana wa Kiislam wakizkri wakati wa kuelekea kaburini.

Mwili ukiwasili kwenye makaburi ya Tambaza kwaajili ya maziko.



Waombolezaji wakisikiliza kwa makini Swala iliyokua ikitolewa na mmoja wa viongozi wa dini ya Kiislam.

Chekibudi ni mmoja wa Wasanii waliohudhuria msiba huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimfariji mtoto wa Sheigh Yahaya Husein wakati akifuatilia maziko ya baba yake yakiendelea kaburini hapo.

Baadhi ya watoto wa marehemu na viongozi wa dini ya Kiislam wakiupokea mwili wa Marehem kwaajili ya kuungiza mwandani.

Hapa wakimuingiza mwandani.

Pumzika Mnajimu wetu.

Viongozi mbalimbali nao waliungana na ndugu wa marehem katika kuomboleza. Hapa Shamsi Vuai Nahodha akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu.

Mzee wa Upako naye akiweka udongo.

Steven Wasira akionesha upendo kwa marehemu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dr. Jakaya M. Kikwete akiweka udongo kwa huzuni mkubwa.

"Baba kwaheri tangulia sisi tuko nyuma yako" Mtoto wa Sheigh Yahaya Husein akiweka udongo kwenye kaburi la baba yake.

Hii ni baadhi ya gari aliloacha Marehem likiwa limebeba watoto wa marehemu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali panapostahili kulingana na matendo yake na imani yake Amen.