.

Friday, April 22, 2011

MMMH HII NAYO IMEKAAJE JAMANI...


CHADEMA: Tutahoji utajiri wa Ridhiwan.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Willbroad Slaa amesema chama chake kinajipanga kuhoji kile alichodai utajiri mkubwa wa ghafla wa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji na pia Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Dk Slaa alisema hayo jana katika Kijiji cha Ikungi, mkoani Singida alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara. Alisema anajua kuwa mjumbe huyo (jina tunalihifadhi kwa kuwa jitihada za kumpata kujibu tuhuma hizo hazikufanikiwa), licha ya umri wake mdogo hivi sasa ana fedha nyingi. Katika mkutano huo Dk Slaa alimtuhumu kuwa na utajiri uliopindukia ambao alisema haulingani na umri wake. Dk Slaa alisema chama chake kina shaka na wingi wa fedha alizonazo kijana huyo na kwamba atahakikisha kwamba kigogo huyo anaiambia Chadema na Watanzania alipozipata. Alisema kijana huyo alimaliza masomo yake muda mfupi uliopita, lakini tayari amekuwa bilionea akisisitiza kuwa chama chake kitahoji alipopata mabilioni hayo. "Ninajua kwamba ana fedha nyingi, lakini huyu alikuwa mtoto wa shule juzi tu. Leo amekuwa bilionea! Atatuambia amepata wapi hizo fedha, Chadema tutahoji ni wapi amezipata," alisema Dk Slaa. Dk Slaa pia alizungumzia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa kelele za wapinzani hazimnyimi usingizi na kusema watahakikisha halali. Mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana alitoa kauli hiyo alipozungumzia ushindi wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akisema umeimarisha ngome ya upinzani bungeni. "Rais Kikwete alisema kelele za upinzani hazimnyimi usingizi, lakini kwa kumchagua Lissu mmeongeza nguvu ya upinzani na sasa hatalala," alisema na kuongeza: “Ujumbe wangu kwenu ni kwamba sasa mmemchagua mbunge jasiri anayeweza kumwambia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mbele ya Waziri Mkuu kuwa amekuwa mvivu kusoma.” Alisema kutokana na ujasiri huo wa Lissu sasa miswada mibovu haitapelekwa bungeni. Awali, akizungumza katika mkutano huo, Lissu alisema Halmashauri ya Wilaya ya Singida imetenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo akisema kuwa ni mara ya kwanza fedha hizo kutengwa huku akijigamba kwamba ni kutokana na wapinzani kubana mianya ya wizi.

NAONA KAMA VILE MANENO YA MZEE MSEKWA YANA UKWELI FLANI IVI...


Msekwa: Yafaa spika kuwa mwanasheria, Spika Makinda asema si lazima!




MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa amesema ni vigumu kwa mtu asiye na taaluma ya sheria kuliongoza Bunge akiwa Spika.Msekwa ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu mwaka 2000 hadi 2005, aliyasema hayo katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), hivi karibuni akizungumzia utendaji wake akiwa na wadhifa huo. Pia alizungumzia miaka 50 ya Uhuru.

Katika mahojiano hayo, Msekwa alisema alilazimika kurudi shule, kusomea shahada ya sheria ili aweze kuliendesha vyema Bunge.

Kauli hiyo ya Msekwa imekuja wakati Bunge la sasa likishuhudia mivutano ya kisheria baina ya wabunge na Spika wa Bunge hilo la 10, Anne Makinda.

Katika mkutano wa tatu wa Bunge hilo uliomalizika Jumamosi ya wiki iliyopita, Mbunge wa Singida Kusini (Chadema), Tundu Lissu ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba alionekana kuipa wakati mgumu Serikali alipokuwa akipinga kifungu cha sheria kinachowaruhusu wanasiasa kuingilia uhuru wa mahakama.

Katika mvutano huo ambao pia ulimhusisha, Spika Makinda, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alimuunga mkono Lissu licha ya muswada huo kupitishwa.

Katika Bunge la 10 pia kumekuwepo malumbano yanayoashiria wabunge wengi kutozijua vyema Kanuni za Bunge na sheria mbalimbali hivyo kujikuta wakivutana wao kwa wao, wakati mwingine na Spika Makinda.

Hata hivyo, baadaye akizungumza na Mwananchi, Msekwa alirejea kauli hiyo akisema: "Bunge ni la kutunga sheria, kwa hiyo ni muhimu kwa Spika kuwa na taaluma ya sheria."

“Ni kweli walinihoji TBC, ilikuwa ni kuhusu miaka 50 ya Uhuru. Ndiyo lile ni Bunge la kutunga sheria, kwa hiyo ni muhimu kwa Spika kuwa na taaluma ya sheria.”

Msekwa ambaye aliwahi pia kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1962-1970, Katibu Msaidizi wa Bunge kati ya mwaka 1960-1962 na Spika wa Bunge kati ya mwaka 2000-2005 alisema suala la Spika kusoma sheria ni la uamuzi binafsi siyo lazima.

“Huwezi kulilinganisha Bunge la wakati wangu na Bunge la sasa. Ni kweli kazi za Bunge ni zilezile, lakini wabunge wa sasa ni wengine. Siyo lazima kwa Spika kusoma sheria, ni uamuzi wa mtu binafsi," alisema na kufafanua:

"Adam Sapi Mkwawa hakuwa mwanasheria, Chifu Mang’enya hakuwa mwanasheria. Hata mimi nilipoanza sikuwa mwanasheria, lakini baadaye niliona umuhimu wa kusoma sheria.”

Bunge aliloongoza Msekwa lilishuhudia mawaziri wakilazimika kujiuzulu kutokana na kashfa. Hao ni pamoja na Profesa Simon Mbilinyi, Dk Juma Ngasongwa na baadaye Idi Simba wote hao kutokana na nguvu ya Bunge.
Akizungumzia kauli hiyo ya Msemwa, Spika Makinda licha ya kukiri kutosomea sheria moja kwa moja, alisema uzoefu alioupata Bungeni tangu alipotoka shule ndiyo unaomwezesha kuliendesha kwa ufanisi.

“Nimekulia na kuzeekea bungeni, taaluma yangu ni uhasibu, lakini mimi ni kati ya wabunge wakongwe. Tangu nimetoka shule niko bungeni,” alisema.

Alipoulizwa iwapo ana mpango wa kusomea sheria ili kumudu vyema zaidi uendeshaji wa Bunge, Makinda alisema kuwa amesomea sheria katika taaluma yake ya uhasibu ambayo inamsaidia pia kuzielewa Kanuni za Bunge.

“Kwani mimi sijasoma sheria? Mimi ni ‘accountant by professional’, (mhasibu kitaaluma) na huko nimesomea sheria. Ni kweli sina ‘bachelor’ (shahada) ya sheria, lakini, nina uelewa wa sheria," alisema.
Makinda alijigamba: " Nimekuwa mbunge, 'chief whip' (mnadhimu) kwa muda wa miaka minane, nimekuwa mwenyekiti wa Bunge, yote hayo yamenipa uwezo.”

Kuhusu changamoto anazokabiliana nazo katika nafasi hiyo, Spika Makinda alisema kuwa hilo jambo la kawaida kwake, lakini akasema tatizo na jambo kubwa ni wabunge kutokuelewa kanuni.

Hata hivyo, alisema anajitahidi kuwafundisha Kanuni za Bunge ili waendane na mwenendo wake.

“Unajua kipindi hiki wabunge ndiyo wamekuja, wengi wao hawajui Kanuni za Bunge, wanafanya makosa na utundu mwingi. Lakini tutawafundisha kanuni, naamini, Bunge litakuwa ‘smart’ siku zijazo,” alisema na kuongeza:

“Kwa mfano, sasa kuna kitu kinachoitwa ‘adjoin motion’ ambapo mbunge anamtaarifu Spika pale anapokuwa akiahirisha Bunge kuwa ana hoja ya kulitaarifu Bunge, basi Mbunge anapewa dakika 15 za kujieleza. Yote hayo tutawafundisha na wengi wameshaleta maoni ya kufanya hivyo.”

Akizungumzia tukio la hivi karibuni ambalo Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje alitoa kauli iliyosababisha wabunge kurushiana maneno, Spika Makinda alisema kuwa tukio hilo lilikuwa ni kinyume cha Kanuni za Bunge.

“Kanuni zinakataza wabunge ku-shout hovyo (Kupayuka). Ile ilikuwa ni makosa. Unajua wabunge bado wanajifunza na tutafanya ‘amendments’ (marekebisho) ya kanuni ili kuwawezesha wabunge kuzoea Bunge. Kwa mfano, sasa kuna kitu kinaitwa “Committee of supply,” yaani wakati wa mbunge kutoa shilingi Bungeni. Hilo nalo tutawafundisha ili waelewe,” alisema.




Mmmh WAVIVU utawajua tu maana wengine tumesimama tunashangilia wao wamekaa haaa ahaaaa ila tunaonyesha umoja wetu, pichani kuanzia kushoto ni TINO, RAY, RICHIE RICHIE, CHIKOKA na STEVE NYERERE wakiufatilia kwa makini mchezo unavyoendelea...

STEVE NYERERE na MAINDA nao walikuwepo, na vimo vyao pia vinalingana daaah...

Nguli JAQ WOLPER akionyesha Ufundi uku SHILOLE akiwa tayari kutoa msaada...

Hayaa mechi ndio inaanza na MASANJA nae akageuka mpiga picha wa KUJITEGEMEA...

Timu zimejipanga tayari kwa ukaguzi then mechi ndio ianze...

Mawaidha lazma yawepo ili watu wafuate sheria atiii...

Mkongwe KATIE nae yupo kwenye Timu ya Bongo Movie queen 'KUWAHAMASISHA' vijana...

Hiki ndio kikosi kamili cha BONGO MOVIE QUEENS kinachojumuisha wacheza Filamu woote wa kike nchini ambacho weekend iliyopita ilifungwa kwa TAAABU na timu ya TTCL kwenye mechi kali iliyofanyika kwenye viwanja vya TTCL kijitonyama! Vijana wanazidi kuiva kimazoezi kilasiku saa moja asubuhi pale kwenye viwanja vya Leaderz Kinondoni...
Hapa wanaonekana kina MAYA, JAQ WOLPER, COLETTA na wengineo wakifanya mpango wa 'sala' kidogo kabla mechi haijaanza...
Sala ikiendelea...





Bendi ya FM ACADEMIA aka 'wazee wa ngwasuma' kama kawa walimwaga 'SEBENE' la nguvu jana Jumapili ndani ya ukumbi wa Msasani Club ulioko maeneo ya Morocco jijini Dar! Kwakweli jamaa wanajua muziki ni nini na kwenye kumwaga 'MAUNO' nadhani kila mdau wa muziki anwatambua hawa mabwana, ilikuwa 'HAATWARIII' jana! Pichani nikiwa na 'Rapa' namba moja wa Bendi hiyo KHALIJO MWANA KITOKOLOLO...

Katikati ni Rais wa Bendi hiyo ya FM NYOSHI EL SAADAT aka 'Sauti ya simba' akiwa na ROGEE MUZUNGU kulia, wakiimba kwa hisia jana...

Mkaanga 'CHIPS' akiwa kazini...

Wanenguaji nao hawakufanya AJIZI, na walileta 'Ladha' safi saanaaa...

Mwimbaji nguli PATCHO MWAMBA aka 'Tajiri' akiwa sambamba na mwimbaji mpya wa kike wa Bendi hiyo aitwae Mariam ndani ya Msasani Club jana Jumapili...

Huyu anaitwa B52, ni mpiga gita la 'Solo' mkongwe nchini ambaye kwa wale wanaomkumbuka mwanamama SAIDA KALORI alivyotamba na zile nyimbo zake kwenye Album ya 'chambua kama karanga' basi huyu bwana ndie mtunzi na mpigaji wa gita katika ile Album yooote na kumpaisha sana SAIDA KALORI, kwasasa yupo na FM ACADEMIA...

Huyu anaitwa Queen Suzy, ni mnenguaji 'HATARI' ila ni bingwa wa kuhama Bendi, na tabia hiyo imemsababishia 'uadui' mkubwa kila anakoenda na 'kibaya' zaidi huwa anatokaga FM ACADEMIA anahamia TWANGA PEPETA, alafu anaondoka TWANGA anarudi tena FM ACADEMIA looh! Sasa ameshahama mara na kurudi maranyingi sana na majuzi alitoroka TWANGA akaenda OMAN basi ile kurudi Bongo akaenda kutua FM moja kwa moja daah...

QUEEN SUZY akiwajibika Jukwaani jana Jumapili ndani ya Msasani Club...

Weeeweeeee chezeeaaaa....

Rapa namba moja wa FM ACADEMIA aka 'wazee wa ngwasuma' KALIDJO MWANA KITOKOLOLO aka 'KUKU' akirapu kwa hisia kali jana ndani ya Msasani Club maeneo ya Morocco...

Ni mwendo wa 'SHOWBIZE' tu weee...

Kwakweli madansa wa Fm Academia ni wakali sanaaa, jaribi kwenda kushuhudia uone...


HII NI HADITHI YA KWELI KWA WALE WOOOTE WANAOTAKA KWENDA LOLIONDO KWA 'BABU'...


Hii ni hadithi ya ndugu yangu mmoja aliyekwenda LOLIONDO majuzi. Anasimulia hivi, ni usiku wenye baridi kali, mvua inayoambatana na upepo inanyesha. Katika hali ya kawaida, baridi hii haivumiliki kwani nawaona kina baba wakiota moto katika jiko linalotumiwa na mama lishe.Natamani kuungana nao lakini nashindwa kwani jiko lenyewe ni dogo na idadi ya watu waliolizunguka ni kubwa. Lakini pia ugeni wangu katika eneo hilo unakuwa kikwazo cha shauku yangu ya kujiunga nao.Mbele yangu nawaona kina mama na watoto wao wengi kiasi, wakiwa wamelala barazani katika moja ya nyumba za wageni zilizopo katika eneo liitwalo Wasso.Wasso ni kitongoji maarufu katika eneo la Loliondo. Kitongoji hiki ni sehemu ya mji wa Loliondo na kwa mujibu wa wenyeji wa mji huu, Wasso ni mji mpya unaopanua ukubwa wa mji wa asili wa Loliondo.Eneo hili linachangamshwa na uwepo wa shughuli nyingi za kibiashara, nyumba za wageni na hata gulio kubwa ambalo hufanyika kila Jumamosi likiwavuta wafanyabiashara wengi kutoka nchini Kenya. Lakini usiku, halitamaniki kutokana na baridi kali.Katika baraza au kwenye veranda ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Sayi, ndipo walipolala kina mama hawa. Udadisi wangu unabaini kuwa hawa ni wenyeji wa maeneo ya Wilaya ya Ngorongoro na wako safarini kwenda Samunge kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapila kunywa dawa.“Usiku umewakuta hapa hivyo lazima walale halafu kesho asubuhi na mapema, wanaamka kwenda kwa babu kunywa dawa," anasema mmoja wa wahudumu wa nyumba ya wageni aliyejitambulisha kwa jina moja la Fatma na kuongeza: “Hapa ni kawaida, tena leo wamepungua, huwa wanakuwa wengi hadi tunawatimua (kuwafukuza). ”Nilimwuliza Fatma kwamba watu hawa wanatumia usafiri gani kwenda Samunge? Jibu lake lilikuwa ni fupi tu kwamba “…..hawa wanatembea”. Umbali kutoka Wasso hadi Samunge ni karibu kilometa 70 lakini, kwa mujibu wa wenyeji, matumizi ya njia za mkato huwawezesha kupunguza umbali huo hadi kufikia kilometa zisizopungua 40.Kwa maana hiyo wenyeji wanasema hutumia muda wa kati ya saa tano hadi sita kufika Samunge na baada ya kupata kikombe cha babu huanza tena safari ya kutembea kurudi makwao. Ng’ambo ya barabara kutoka ilipo nyumba hii ya wageni ya Sayi, ipo nyumba nyingine ya kulala wageni iitwayo Selemani. Hivyo jibu la Fatma lilinipa wajibu wa kuvuka barabara ili kwenda kuona iwapo kuna watu wengine waliolala barazani.Hali niliyoikuta ni ileile. Kina mama kwa kina baba walikuwa wakihangaika kujisitiri kwa mashuka na makoti waliyokuwa nayo. Katika hali ya ubinadamu, nawahurumia lakini sina la kufanya kwani hata kama ningekuwa na fedha za kugharamia malazi yao, vyumba katika nyumba za wageni zilizopo Wasso zilikuwa zimejaa. Malazi kwa Babu Samunge Wakati fulani nikiwa Loliondo, nililazimika kulala katika Kijiji cha Samunge ambako Mchungaji Mwasapila anatoa dawa ya magonjwa sugu.Siku ya kwanza tulipoamua kwamba tutalala Samunge mimi na wenzangu, Mussa Juma na Fidelis Felix tuliazimia kutafuta sehemu ya kulala usiku ule. Wakati tukiwa katika harakati za kutafuta malazi, nilibaini kwamba watu wengi ambao wanasubiri zamu za kunywa dawa hawana mahali pa kulala. Wengi wamechukua mikeka mabusati na kuyatandika pembezoni mwa magari yao na kulala hapo. Wengine wamekuwa katika foleni, wakilala kwa ‘staili’ hii kwa muda wa siku sita au zaidi.Lakini hawa wana ahueni kwani wana uwezo wa kufanya hivyo. Kuna wengine ambao maisha yao ni magumu zaidi ya haya. Hawa wanalala kwenye magari hasa magari makubwa kama malori mengine yakiwa ni Fuso. Humo kuna watu ambao wako taabani. Hawa hawalioni jua kwani hawana uwezo wa kutoka nje. Kutwa, kucha wamo ndani ya magari yao wakisogea taratibu kuelekea kwa Mchungaji Mwasapila.Katika gari mojawapo aina ya Fuso lililokuwa likitokea mkoani Mara, kulikuwa na abiria wasiopungua 100, wakiwemo wazee, watoto na wagonjwa ambao walikuwa hawajiwezi. Lakini pamoja na adha hiyo, watu wote katika eneo hilo wanavumilia tabu hizo wakiwa na shauku kubwa ya kukutana na Mchungaji Mwasapila ili awape kikombe. Kambi za mahemaKatika kutafuta malazi, tuliingia katika eneo lenye mahema na kuanza kuulizia gharama za kukodi kwa usiku mmoja.Katika eneo la kwanza tulionyeshwa mahema ya aina tatu. Moja ni hema ambalo kulala kwa usiku mmoja gharama yake ilikuwa Sh60,000. Hema hili ni kubwa na lina magodoro mawili madogo ya shule (futi mbili na nusu kwa tano).Pia tukapelekwa kwenye hema lenye ukubwa wa kati ambalo lilikuwa na godoro moja dogo. Gharama yake ni Sh45,000.Hema la tatu lilikuwa dogo na gharama yake ni Sh35,000. Hema hilo lilikuwa na godoro moja ndani. Kwa kuangalia uwezo wetu kifedha, tulilazimika kutafuta eneo jingine na baada ya kuzunguka katika maeneo kadhaa, tulibahatika kupata hema kwa gharama ‘nafuu’ ya Sh25,000. Hema hilo kwa mujibu wa msimamizi wake, lilikuwa na uwezo wa kulaza watu watatu kwa wakati mmoja. Katika eneo lile kulikuwa na mahema yasiyopungua 20 na wakati tulipofika, saa 4.20 usiku, lilikuwa limebaki hema moja tu, ambalo ndilo tulilopewa na kulipa kiasi hicho cha fedha. Hema hili liligeuka kuwa makazi yetu ya muda kwani kila tulipofika kulala Samunge katika siku zote 14 tulizokaa Loliondo, tukiendelea na kazi zetu za kihabari, tulikuwa tukilitumia. Usiku wa taabuUsiku wa kwanza ulikuwa wa tabu kwetu kutokana na hema hilo kuwa na dogoro moja tu dogo. Ilibidi tuweke vichwa na sehemu ya viwiliwili vyetu kwenye godoro hili huku sehemu ya miili yetu ikibaki chini katika ‘sakafu’ ya hema hilo ambalo kwa jinsi lilivyotengenzwa ni kama suti kuanzia sakafu, kuta mpaka paa. Hatukuwa na shuka, blanketi, kanga wala kitenge kwa ajili yakujisitiri na baridi. Pamoja na kwamba Samunge si sehemu yenye baridi ya kutisha, lakini ulipofika usiku wa manane, tulilazimika kuyatafuta majaketi na makoti yetu.Baridi ilianza kuingia katika miili yetu kwa mbali. Kweli, ulikuwa ni usiku wa tabu na kila mmoja wetu alitamani kuche haraka ili tuweze kuondokana na adha hiyo. Haya yalithibitika asubuhi pale kila mmoja wetu alipokuwa akiusimulia ‘usiku wake’ ulivyokuwa. Ulifika wakati tukataka kuweka azimio la kutolala tena Samunge lakini, kwa jinsi mazingira yalivyokuwa, azimio hili halikutekelezeka kwani tulirejea kulala kijijini hapa mara tatu zaidi.Hali hii inanikumbusha usiku wa mvua na baridi kule Wasso ambako kina mama na watoto wao walikuwa wamelala barazani baada ya kukosa malazi. Nilijiuliza moyoni, ikiwa sisi ambao tumepata hema tunapata tabu kiasi hicho, hali ilikuwaje kwa wale waliolala nje bila hata ya kuwa na nguo ya kujisitiri?Pamoja na hali hii, watu bado walionekana kuwa na shauku kubwa ya kufika Samunge kupata kikombe kwa Mchungaji Mwasapila.Mwisho



KAENI MKAO WA KULA KUPATA BOONGE LA 'MOVIE' KATI YANGU NA AUNT EZEKIEL, PICHA ZINGINE BAADAE...


Hii ni 'SCENE' ya Ufukweni nikiwa na AUNT EZEKIEL ambayo pia tulifunika sana kwenye hii Movie yetu itakayotoka soon...

Mambo juu ya mambo, HAATWAARRIIIII....

Cameraman wangu huyu anaitwa AMANI, ni mkali sana na amefanya kazi kuubwa saana kushooot hii Movie daah...

Hii ni 'SCENE' ya nyumbani kwangu nikiwa na rafiki yangu STEVE SANDHU...

'MITEGO' kama hii lazma iwepo kwenye Movie ila ndio 'UNAVUMILIA' tu...

SCENE yangu na AUNT EZEKIEL ikiendelea, hii movie itakuwa 'BALAA' ikitoka daah......

Na hapa tukiwa na mwigizaji mwingine aitwae STEVE SANDHU ambaye nae 'AMENYONGA' sana kwenye Movie hii itakayotoka soon...

Hii ni 'SCENE' nyingine kati yangu na AUNT EZEKIEL ikiendelea, ni balaa nakwambia...

IJUE FILAMU ILIYOTENGENEZWA KWA 'GHARAMA' KUBWA ZAIDI DUNIANI...


Kwa taarifa yako hii ni Filamu ya 'AVATAR' ambayo ndio Filamu iliyotengenezwa kwa bei 'MBAYA' zaidi duniani mpaka sasa! Filamu hii ya 'AVATAR' imetengenezwa kwa gharama ya Dola millioni 500 sawa na Bilioni 740 za kibongo kutokana na vifaa vilivyotumika kuitengeneza Filamu hiyo na mfano ni 'Camera' zilizotumika kushoot Filamu hiyo zilitengenezwa maalum kwa ajili ya Filamu hiyo tuu! JAMES CAMEROON ndie alikuwa muongozaji wa Filamu hiyo iliyoshirikisha nyota kama vile SAM WORTHNGTON, ZOE SALDANA, STEOHEN LANG, MICHELLE RODRIGUEZ, JOEL MOORE, GIOVANNI RIBISI na SIGOURNEY WEAVER.