.

Tuesday, May 3, 2011

OSAMA ALIVYOULIWA..

Wamarekani wameendelea kushangilia kuuliwa kwa Osama bin Laden huku kiongozi wa kundi la Hamas la Palestina akilaani mauaji hayo. Picha na habari zaidi za jinsi Osama bin Laden alivyouliwa zimeanza kujitokeza.Osama bin Laden ambaye alikuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda aliuliwa kwa kupigwa risasi ya jicho la kushoto baada ya kukataa kujisalimisha kwa majeshi ya Marekani.

Rais wa Marekani, Barack Obama pamoja na maafisa wake wa ulinzi na CIA walilifuatilia shambulizi la kumuua Osama bin Laden LIVE kupitia video zilizokuwa zikirekodiwa kwa kutumia video kamera zilizowekwa kwenye helmet za makomandoo wa Marekani walioivamia nyumba ya Osama.

Picha za tukio hilo zilizotolewa na televisheni ya ABC zilionyesha damu zikiwa zimetapakaa kwenye chumba ambacho Osama bin Laden alikuwemo.

Osama aliuliwa kwa kupigwa risasi kwenye jicho lake la kushoto. Maiti yake ilichukuliwa na kupelekwa kwenye kambi ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan.

Baada ya vipimo vya DNA kuthibitisha kwa asilimia 99 kuwa mtu waliyemuua alikuwa ni Osama bin Laden baada ya kulinganishwa na vipimo vya DNA vya ndugu zake, maiti yake ilizikwa baharini baada ya Saudi Arabia na nchi zingine kuukataa mwili wake.

Helikopta moja kati ya nne za jeshi la Marekani zilizotumika kufanya mashambulizi toka angani, ilitunguliwa na roketi zilizorushwa na wapambe wa Osama bin Laden.

Nyumba aliyokuwa akiishi Osama ilikuwa takribani mita 200 toka kituo cha polisi na kilomita mbili toka kambi ya jeshi la Pakistan.

Taarifa ya Marekani ilisema kuwa maafisa wa Pakistan walikuwa hawajui kuwa Osama alikuwa amejificha kwenye jumba hilo lenye thamani ya dola milioni moja ambalo lilijengwa miaka mitano iliyopita likiwa na uzio mrefu wa kuta nene.

Wamarekani wameendelea kushangilia kuuliwa kwa Osama bin Laden ambaye alikuwa ndiye mtu aliyekuwa akitafutwa sana kuliko watu wote duniani.

Kiongozi wa Hamas katika ukanda wa Gazza, Ismail Haniyeh akiongelea kuuliwa kwa bin Laden alisema kuwa kuuliwa kwa bin Laden ni muendelezo wa umwagaji damu za Waarabu na waislamu unaofanywa na Marekani.

"Tunalaani kuuliwa kwa shujaa mtukufu wa Waarabu, Osama bin Laden na tunamuomba Mwenyezimungu amrehemu na kumweka mahali pema pamoja na waja wake wema", alisema kiongozi huyo wa Hamas.

OSAMA AWA CHAKULA CHA SAMAKI.

Baada ya kuuwawa kwa kiongozi huyo, maafisa waandamizi nchini Pakistan walisema maziko yake yatatekelezwa kwa taratibu na tamaduni za dini ya Kiislamu. Taratibu hizo ni pamoja na mwili wake kuzikwa katika kipindi cha masaa 24 baada ya kutokea kifo. Ama kwa upande wao wanachama wa mtandao wa Al- Qaeda katika Rasi ya Uarabuni, Mtandao wa Osama Bin Laden, nchini Yemen wamekiita kifo cha Osama kuwa ni janga kubwa katika harakati zao.
Akizungumza kwa njia ya simu na Shirika la Habari la Ufaransa, AFP, mmoja kati ya wanamtandao hao, amesema hawakuamini waliposikia taarifa za kifo cha kiongozi wao. Amesema, hata hivyo, aliwasiliana na wenzao wa Pakistan ambao walithibitisha kifo hicho.
Awali, Rais Barack Obama wa Marekani alitangaza kwamba Osama Bin Laden ameuwawa katika mashambulizi yaliyofanyika jana nchini Pakistan na kumaliza harakati zilizodumu kwa takribani miaka 10 za kumwinda kiongozi huyo aliyepanga shambulio la Septemba 11 mwaka 2001.
Akizungumza usiku wa kuamkia leo katika Ikulu ya Marekani, Rais Obama amesema " haki imetendeka" dhidi ya kiongozi huyo wa wapiganaji wa kiislamu aliyefanikisha mashambulizi kadhaa katika maeneo tofauti duniani kote.
"Marekani iliendesha operesheni iliyofanikisa kuuwawa kwa Osama Bin Laden. Kiongozi wa Al- Qaeda. Gaidi aliyeshiriki mauwaji ya maelfu ya watu wasio na hatia, wanawake na watoto." Amesema Rais Obama.
Kifo cha Bin Laden ni hatua muhimu ingawa haijawa wazi kama inaweza kubadili vita ya kimataifa dhidi ya mtandao wa kigaidi au kufanikisha kumalizika haraka kwa vita dhidi ya Taliban nchini Afghastan.
Chanzo kimoja cha habari kutoka katika operesheni za kijeshi za Marekani zinasema Osama alipigwa risasi kichwani. Kifo chake pia kilithibitishwa na maafisa tofauti nchini Pakistan.
Kifo cha Osama kimepokelewa kwa shangwe, nderemo na vifijo katika miji ya Washngton na New York. Hakika umekuwa ushindi mkubwa wa usalama wa kitaifa kwa Obama tangu aingie madarakani mapema 2009 na utampa nguvu ya kisiasa atakapowania tena kiti cha urais 2012.
Obama atakamilisha kwa urahisi vita vya karibu muongo mmoja vya Afghanistan, vilivyoanza Septemba kumi na moja 2001, baada ya shambulio lililowaua takriban watu 3,000 nchini Marekani.
Afrika Mashariki Osama atakumbukwa kutokana na kufanikisha mauaji ya takribani watu 224 huku wengine 5,000 wakijeruhiwa baada ya kufanikisha mashambulizi katika balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya
.

"UTAMTOA BATA WANGU HAIWEZEKANI"

RAHA YA KUFAMANIWA KWENYE DANGURO.

Mwanaume huyu wa nchini China amekuwa maarufu duniani kufuatia kusambazwa kwa picha zake online wakati akihatarisha maisha yake kwa kujaribu kushuka toka ghorofani akiwa uchi wa mnyama akiwakimbia polisi waliovamia danguro alilokuwa akijisevia uroda.
Makahaba wakikimbia Danguro

MAAJABU MSITU WA MZELEZI

ULANGA ni moja ya wilaya tano za Mkoa wa Morogoro. Wilaya hiyo ina misitu minane ya hifadhi, yenye ukubwa wa hekta 8,582. Misitu hiyo ni chanzo kikuu cha maji kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Katika misitu hiyo, msitu wa Mzelezi ndiyo wenye uhifadhi madhubuti, unaofanywa na
serikali kuu, halmashauri ya wilaya na serikali za vijiji vya Isongo na Mzelezi. Msitu huo ni moja ya misitu ya Milima ya Tao la Mashariki, ambayo inatambulika kimataifa kama Urithi wa Dunia.

Msitu huo ni nguzo muhimu katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii wa ndani na nje, kutokana na kuwa na vivutio adimu, ambavyo havipatikani katika eneo lingine duniani. Kwa mujibu wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, msitu huo ulianzishwa Julai
30 mwaka 1954 kwa tamko la serikali namba 216.

Ulianzishwa kutokana na kuwepo kwa bioanuwai nyingi. Kutokana na uhifadhi madhubuti,
hivi leo msitu huo una aina 27 za wanyama wadogo, ambapo aina nne ya wanyama hao, zinapatikana katika msimu huo pekee.

Pia, katika msitu huo kuna aina 109 za ndege na pia kuna aina 336 za mimea. Mbali na wanyama na mimea, kuna aina 68 ya miti katika msitu huo, ikiwemo milengalenga na mikoko.

“Miti hii ni moja ya aina nane za mimea, ambayo inahitaji uhifadhi wa karibu. Aina hizi za miti zipo katika kitabu chekundu cha Shirika la Kimataifa la Kuhifadhi Wanyama na Mimea (IUCN) na aina hizi sasa zinakaribia kutoweka”, inaeleza taarifa hiyo ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.

Taarifa inaeleza pia kuwa msitu huo una aina nane adimu za vipepeo, ambao wanahitaji uhifadhi wa karibu, kwa vile wanapatikana pekee katika msitu huo. Wapo pia vyura 'amphibian’ wa aina tatu, ambao hawapatikani katika msitu mwingine wowote.

Vyura hao ni ‘loveridge’s toad, scarlet snouted frog na southern torrent frog”. Pia kuna vyura ‘reptilian’ aina nane, ambapo aina mbili zinapatikana tu katika msitu huo. Hali kadhalika, kuna mapango makubwa yanayofaa kwa utalii na ikolojia, hususani katika eneo la Mbangayao.

Mapango haya ni kivutio kikubwa cha utalii wa ndani na nje. Hata hivyo, licha ya kuwa na
rasilimali nyingi, msitu huo unakabiliwa na changamoto nyingi, kama vile kilimo ndani ya msitu, uchomaji moto ndani na nje ya msitu na uchimbaji wa madini ndani na jirani na msitu.

Changamoto nyingine ni makazi na kuwepo kwa njia za binadamu ndani ya msitu. Uongozi wa wilaya ya Ulanga, umechukua hatua mbalimbali za kulinda na kuhifadhi msitu huo, kwa kushirikisha wananchi.

Hatua hizo ni pamoja na kuendeleza vyanzo vya maji katika vijiji vya Vigoi na Nawenge. Navyo vijiji vya Isago, Epango, Mkanga, Mdindo, Chikuti na Mzelezi, vina mpango wa pamoja
wa kulinda na kuendeleza hifadhi ya serikali kuu.

Akizungumzia hifadhi za Mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, anasema hifadhi hizo zina ukubwa wa kilometa za mraba 64,000. Machibya anasema kuwa mkoa huo pia una zaidi ya vyanzo 143 vya mito, ambavyo vinahifadhiwa na Serikali kwa kushirikiana na
wananchi.

Anasema, eneo la hifadhi katika mkoa huo ni pamoja na misitu 80 ya hifadhi na mbuga tatu za taifa. Mbuga hizo ni Mikumi na Udzungwa na Pori la Akiba la Wanyama la Selous, lenye umaarufu mkubwa duniani.

Machibya anasema mahitaji ya mazao ya misitu, yanaendelea kuongezeka kila siku; na kwamba uongozi wa serikali katika mkoa huo, unaendelea kushirikiana na wananchi katika kulinda na kusimamia maliasili, ikiwemo misitu.

Anasema ulinzi na usimamizi wa maliasili, ikiwemo upandaji miti, ni suala la kudumu na endelevu.