.

Tuesday, August 16, 2011

MBUNGE ATOLEWA NJE KWA KUVAA HERENI..........

Sonko akiwa katupia hereni bungeni

Mbunge machachari wa bunge la Kenya Mbuvi Sonko jana alitolewa bungeni kwa mara ya pili kutokana na kuvaa hereni zenye kung'aa bungeni kama wafanyavyo mastaa na vijana wa kisasa.

Mbunge wa Jimbo la Ikolomoni Bonny Khalwale alikuwa wa kwanza kuhoji jinsi Mbuvi alivyovaa bungeni baada ya kuiona hereni sikioni mwake, hata hivyo spika Kenneth Marende akawa hajashtukia issue.

Lakini mbunge wa Kisumu Magharibi Olago Aluoch alisimama naye kuhoji Mbuvi alivyovaa bungeni na safari hii Spika Marende akamuamuru atoke nje kwa siku nzima hapo ya jana, licha ya kukanusha na kuwataka wabunge wenzie wamkague kama ameificha hereni.


Sonko katika swaga zage