.

Thursday, July 14, 2011

''RAIS WA TAFF JIUZULU AMANI IPATIKANE''

Baadhi ya wasanii wa Filamu wa Bongo Movie Club wamemtaka rasi wa shirikisho la wasanii wa filamu TAFF Bw. Simon Mwakifyamba kujiuzuru mara moja ili amani ipatikane katika tasnia hiyo kwani wamedai yeye ndio chanzo cha mvurugano uliotokea hivi sasa unaowasabishia malumbano baina yao.

Wasanii hao Jacob Steven''JB'',Steven Kanumba,Chiki Mochoma ambaye ni mmoja wa viongozi wa klabu hiyo pamoja na mwanadada Jackline Wolper wamedai kuwa Simon ndio mchonganishi na anawachafua wao pamoja washirika wake na kusema wao klabu yao imesajiliwa na wana mamlaka ya kufanya vyovyote kwasababu haihusiani na tasnia ya filamu.

Katika sakata la Wolper kudaiwa kutaka kumpiga rais wa Shirikisho katika mkutano uliofanyika Leaders Club Wolper mwenyewe amejitetea kuwa hakuwa na nia ya kupigana bali alikuwa anataka kupishwa kwenda kumwelewesha rais alikuwa anakosea.