.

Monday, August 15, 2011

THE GAME AKABILIWA NA MASHTAKA............!!!!!!!!

The Game
Rapa Jayceon Terrell Taylor ''The Game'' anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu baada ya kuweka namba ya mkuu wa kituo cha polisi cha Los Angeles kwenye Twitter na kuwataka mashabiki wake waipige.

Inasemekana aliwaambia wafuasi wake kuipiga namba hiyo ya Kituo cha Campton,California ili awapatie nafasi ya kibarua cha muda cha kujifunza kazi.

Mamia ya mashabiki wa The Game walifuata maelekezo hayo na simu ya kitengo hicho cha polisi ilizidiwa na wingi wa simu zilizopigwa kwa wakati mmoja, na kusababisha kituo kushindwa kutoa huduma za dharura kwa wakati.

JESSICA ALBA AJIFUNGUA MTOTO MWINGINE..........!!!!!!

Jessica akiwa na mumewe Cash Warren

Muigizaji nyota Jessica Alba amebahatika kupata mtoto mwingine wa kike ambapo amejifungua siku ya Jumamosi ya tarehe 13 na kumleta duniani ndugu wa mtoto wake wa kike mwenye miaka 3.

Jessica na mtoto wao mdogo

Alba ambaye ni nyota wa Sin City alitangaza kupitia mtandao wa facebook kuwa yeye na mume wake Cash Warren wamepata mtoto mwingine na wana furaha sana.

Jessica na mumewe pamoja na mtoto wao mkubwa wa kike

TUSKER PROJECT ALL STARS YAMALIZIKA........!!!!!MSECHU ASHINDA........


Peter Msechu wa Tanzania

Shindano la Tusker All Stars lililoanza 26 June,2011 limefikia fainali jana kwa washindi watatu kupatikana ambapo Alpha Rwirangira toka Rwanda (TPF 3 - Winner),Peter Msechu toka Tanzania (Mshindi wa 2 – TPF 4) na Davis Ntare toka Uganda (TPF 4 – Winner) wameibuka washindi na wamepata shavu la kupiga show same stage na wasanii wa kimataifa baadaye mwaka huu nchini Kenya.

Alpha Rwirangira toka Rwanda (TPF 3 - Winner)

Washiriki wengine walikua Hemedi Suleiman toka Tanzania,Caroline Nabulime na Amileena Mwenesi toka Kenya,Bernard Ng'ang'a na Patricia Kihoro toka Kenya walishiriki na walikaa wiki 8.

Davis Ntare toka Uganda (TPF 4 – Winner)

CHAMELEONE ABADILI DINI.........!!!!!


Chameleone akiwa anapongezwa

Mwanamuziki nguli nchini uganda Jose Chameleone ameamua kubadilisha dini na kuwa muislamu ambapo alisilimu kwenye msikiti wa Kibuli jijini Kampala na amedilisha jina la Joseph na kujiita Gadaffi.

Akiwa katika matukio tofauti ndani ya msikiti wa Kabul