.

Tuesday, January 18, 2011

RAHA YA PENZI HESHIMA

Ni kweli ukubali au ukatae penzi lenye heshima lina raha yake , kuna watu unawakuta wanaongea lugha ya matusi utadhani sio wapenzi haipendezi ,Na hapo inawezekana  bado hawajawa na  familiia,Hivi  endapo watabahatika kuipata familia jamani itakuwa na maadili yapi kama sio watoto wenye matusi kama wazazi wao????? Haipendezi jamani kama unafanya hivyo acha mpaka mpenzi wako akushangae kwa mabadiliko yako . Penzi likiwa na Heshima kwani ,Hata mpenzi wako anaona raha kukutambulisha kwa rafiki zake anajuwa huwezi kumtia aibu mbele ya watu wake  ,unapokuwa na lugha mbaya unaweza ukawa unakimbiwa hatoki na wewe kwa kujuwa utamtia aibu  na hii ni kwa wote tubadilike.
                                 MPENDE MWENZIO,MPE THAMANI YAKE NA UMUHESHIMU.