.

Monday, April 25, 2011

Kiwanda cha kutengeneza samani.

YALIOJIFICHA NDANI YA GEREZA LA TIHAR LILILOPO KUSINI MWA ASIA




 Tihar Prisons, ambayo pia hujulikana kana Tihar Ashram, ni gereza kubwa Asia kusini. Lipo katika kijiji cha Tihar takribani kilomita 7 kutoka Chanakya Puri, magharibi mwa New Delhi, India. Inazungukwa na Hari Nagar.

 Gereza linatunzwa na taasisi ya marekebisho . dhumuni lake ni kubadili tabia za wafungwa kuwa raia wa kawaida katika jamii kwa kuwapa ujuzi, elimu na kufuata taratibu maalum. Bidhaa zote zinazotengenezwa ndani ya gereza hili hupewa jina la Tihar.

NICKI MINAJ NA RIHANA KUFANYA VIDEO YA WIMBO WA "FLY" PAMOJA

Wasanii maarufu katika tasnia ya muziki nchini Marekani Rihanna na Nicki Minajkufanya video kwa ajili ya track ya “Fly.”
Akizungumza na vyombo vya habari nchini Marekani Nicki alisema kuwa wanatengeneza video hiyo yeye pamoja na Rihanna weekend hii na kwamba watautumikia ulimwengu kwa njia nyingi tu na sii hiyo video watakayoitengeneza.
Minaj alikiri kuwa Rihanna ni Mwanamuziki wa kike ambaye anamfeel.
Nicki alisema kuwa angependa kushirikiana na wanamuziki wengine wa muziki mbalimbali  na kwamba huwa hasikilizi muziki wa aina moja tu na angependa watu wote wangesikiliza hivyo kama yeye.  “ninasikiliza miziki ya kila aina, ninasikiliza sana miziki ya injili” alisema Minaj.

UNAFAHAMU MAVAZI YA KUVAA NIGHT CLUB?

Kupendelea kutoka nyakati za usiku hasa siku za weekend ni njia moja wapo ya kupata good tym, kukutana na watu wapya na ku-hang out na marafiki. Watu wengi hupendelea hasa kwenda katika kumbi za starehe (night clubs). Si tu kwa kuwa unahitaji kuwa na marafiki bali pia kusikiliza muziki kwa sauti kubwa na kucheza kadiri moyo wao utakavyo. Hata hivyo, kwenda katika nyt clubs huzingatia uvaaji wa mavazi.

SIKIA NDOTO ZA MAPACHA HAWA WA NIGERIA


MAPACHA wanaotamba kwenye filamu za Nigeria, Chidinma na Chidiebere Aneke wanatamani kuolewa na wanaume mapacha na wazae mapacha kama wao. Wasanii hao wa kike wamesema:  'Tunatamani tukiolewa tuzae mapacha wa aina mbili, wawili wa kike na wawili wa kiume na tuishi kwa amani na waume zetu. Tunatamani pia kuolewa siku moja wote wawili, na ikiwezekana na wanaume ambao ni mapacha kama sisi. Lakini tuna imani Mungu atatuchagulia wanaume wanaotufaa. Hatutaki sana kujadili maisha yetu binafsi lakini kifupi ni kwamba tunaishi kwa raha sana na mambo mengine ni siri sana hatuwezi kuyasema'.

MHHHH!!!! USHER RAYMOND NA RIHANA WAZUA TETESI ZA KUA MWILI MMOJA


Usher Raymond

KUNA dalili za uhusiano wa kimapenzi kati ya wanamuziki Usher Raymond na Rihanna.

Ishara zilijionyesha wakati wa sherehe iliyoandaliwa na kampuni ya mavazi ya Armani huko Coachella, California.

Jarida la OK! linaripoti kuwa Usher aliomba kuandaliwa meza ya kukaa na Rihanna.

�Usher aliomba mapema kuandaliwa meza ya kukaa karibu na Rihanna,� mtu mmoja alikaririwa na jarida la OK!

�Rihanna ndiye alitangulia kwenye eneo la tukio akiwa na walinzi wake na kufuatiwa na Usher.�

Watu hao wawili inasemekana walikuwa bize wakicheza pamoja usiku wote wa shughuli.

Rafiki yao mmoja wa karibu amedai kuwa watu hao wamekuwa karibu katika siku za karibuni.

UNATAKA KUA NA NGOZI NYORORO YENYE KUWAKA? NISIKILIZE MIMI


KILA mtu anapenda kuwa na ngozi laini na ya kuvutia, kuna wengine wanafanikiwa kuwa na ngozi hizo lakini wengine wanashindwa kuwa na ngozi laini kama ya mtoto kutokana na kukosea baadhi ya mambo.

Makala ya leo inachambua hatua muhimu za kuhakikisha unakuwa na ngozi laini wakati wote.

Kitu cha kwanza cha kuzingatia ni kuhakikisha unanawa uso wako mara tatu kwa siku, hiyo itasaidia kutoa uchafu ambao unaweza kung'ang'ania na kufanya uso usiwe na mng'ao wa asili na husaidia kuzuia chunusi.

Kitu kingine ni kuhakikisha unanawa uso kwa sabuni ambayo inakwenda sawa na ngozi yako, kama ngozi yako ni ya mafuta hakikisha unatumia sabuni ambayo itakuacha ukiwa mkavu na kama ngozi yako ina ukavu, jioshe na sabuni itakayokufanya uwe na unyevu kiasi (sabuni hizo zinapatikana kwenye maduka ya vipodozi).

Vile vile mhusika anatakiwa kuwa na krimu mbili, yaani ile inayopaswa kupaka mchana na ya usiku. Ikumbukwe kuwa wakati wa usiku ngozi inatakiwa kupakwa krimu laini zaidi kuliko mchana.

Mhusika pia anatakiwa kusugua ngozi yake au kufanya 'scrub' mara mbili mpaka tatu kwa wiki, hiyo itasaidia kutoa uchafu ambao unaweza kujificha katika vinyweleo. Sasa basi kwa mfano mimi mwenyewe Binafsi nina masharti yangu ya kila siku ili kuiweka vizuri ngozi yangu na ndio maana wengi wakikutana LIVE na mimi wananiuliza 'Oooh BEN unatumia nini kwenye ngozi yako? Sasa kwa mfano mimi, kila nikiamka asubuhi lazma ninywe maji glass 2 kabla ya kupiga 'MSWAKI' na mara nyingi mie sinywagi 'CHAI' ila nahakikisha saa 4 ivi napata Juice au 'FRUITS' mchanganyiko tena 'ORIGINO' na sio ya BOX huku mwili wako ukiusindikizia na maji ya kunwa kila baada ya muda flani na pia yakupasa ujue una Ngozi ya aina gani ili utumie 'LOTION' au 'CREAM' ya aina gani yatakayokufaa zaidi mwilini. Alafu hakikisha kila mara unafanya mazoezi na mwili utoke JASHO jingi ili ngozi itoe uchafu kwenye 'VITUNDU! Na pia hakikisha kabla hujalala unakunywa tena Glass 2 za maji na pia ni marufuku kulala na 'MAKE UP' usoni na endapo utaaamka usiku kwenda 'MSALANI' kunywa tena 2, fululiza ivyo kwa wiki 2 utanipa majibu mwenyewe! Mimi ni mtaalamu wa ngozi maana nilishapitiaga 'KOZI' iyo ya wiki 2 iliyoandaliwa na kampuni ya 'VENUS' kwaiyo nina uwezo wa kukuangalia tu alafu ninakushauri utumie Vipodozi gani ili Ngozi yako iwe 'BOMBA' hata kama una 'MAPELE' kibao, TRUST ME!

KAZI NI KAZI.......


Moshi Hemba Mfaume

WASWAHILI husema, ‘kazi ni kazi, bora mkono uende kinywani’, hivi ndivyo ilivyo kwa Moshi Hemba Mfaume ambaye kwa miaka 32 amekuwa akichinja ng’ombe katika machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Ni kazi ambayo kwa jumla inawezekana imemwezesha kuwachinja ng’ombe 1,152,000 kwa muda wote wa kazi yake ile.

“Naipenda sana kazi yangu kwa kuwa ndio ambayo imenifanya nifike hapa nilipo kwa kuniwezesha kupata maendeleo yangu na familia yangu, japo sikuwahi kuwaza kama ningekuwa mchinjaji katika maisha yangu, lakini namshukuru mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuipata.”

Hiyo ni kauli yake mzee huyu mwenye umri wa miaka 61, mkazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam ambaye anakiri kuwa yeye ni mchinjaji mkongwe wa ng’ombe katika machinjio hayo ya serikali.

Hemba ambaye anasema kuwa ni mzaliwa wa Kisarawe, Pwani alipata elimu ya msingi katika Shule ya Kisarawe miaka ya ‘50 ambapo alishindwa kuendelea na masomo ya darasa la tano baada ya matokeo ya darasa la nne kutokuwa mazuri.

Anasema kuwa alianza kufanya biashara ya kuuza karanga, muhogo na bidhaa mbalimbali sokoni lengo lake likiwa ni kujikimu kwa kipato, jambo ambalo lilimsaidia kufanikiwa kuendesha maisha yake ya kila siku.

Kutokana na uwezo wake mkubwa katika kucheza soka, Hemba anasema kuwa mwaka 1972 alipata ajira katika karakana ya iliyokuwa Idara ya Ujenzi, Mawasiliano na Barabara (sasa Wizara ya Ujenzi) ambako alikuwa akifanya kazi ya ufundi wa kutengeneza magari ambayo aliifanya kwa takribani miaka minne.

Anasema kuwa akiwa katika karakana hiyo alikuwa akilipwa mshahara wa Sh240 kwa mwezi, kiasi ambacho anakiri kuwa kwa wakati huo kilitosha kwa mahitaji yake ya kila siku.


“Nilipata faraja sana baada ya kupata kazi katika karakana hiyo na niliongeza bidii katika soka kwa kuwa hicho ndicho kilikuwa kigezo cha kupata ajira mahala hapo.

“Kwa bahati mbaya, mwaka 1976 timu yetu ya Ujenzi ilivunjwa na hivyo kunikosesha kazi nikaondoka na kwenda kiwanda cha nguo cha Kilitex cha mjini Arusha ambako hata hivyo sikukaa kwa muda mrefu na hatimaye nikarejea Dar es Salaam,” anasimulia.

Anasema kuwa aliporejea Dar es Salaam alijiunga na kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill kilichoko Tegeta ambapo alikuwa akifanya kazi ya kukusanya saruji iliyomwagika, kazi za usafi na nyinginezo ambapo hata hivyo hakudumu nazo sana kwani aliamua kuachana na kazi hiyo na kutafuta kazi nyingine.

Anasema mwaka 1977 alilazimika kufanya kazi kwa kujitolea katika machinjio ya Vingunguti baada ya kuona maisha yanazidi kuwa magumu na alijitolea kwa kazi hiyo akipiga deki na kufanya usafi mwingine.

“Nilijitolea kwa miaka miwili katika machinjio haya wakati huo yakiwa chini ya Mwarabu aitwaye Salehe Dahari kabla ya serikali kuchukua vitega uchumi vyake mwaka 1979, kazi ilikuwa ngumu sana kama unavyojua kazi za watu wasio na elimu kubwa zina mateso yake,” anasema na kuongeza:

“Sikukata tamaa na nilijitolea kwa miaka miwili huku nikipata posho kidogo tu ambayo ndo ilinisukuma katika masiha yangu, lakini niliamini siku moja nitafanikiwa na maisha yangu yatakuwa mazuri kwa kuwa niliweka nia na kuipenda kazi yangu”

Hemba anasema kuwa mnamo mwaka 1979 baada ya serikali kuchukua vitegauchumi vyake ikiwamo machinjio hayo ya Vingunguti, yeye alifanikiwa kuwekwa katika ajira hasa kutokana na viongozi wake kubaini uwezo na uadilifu wake kazini.

Anasema kuwa aliwaheshimu sana wakuu wake wa kazi jambo ambalo hadi leo analifanya kwa kuwa alijua ni watu muhimu katika kufikia malengo yake katika maisha na kwamba ndio ambao walikuwa wakimshauri kwa mambo mbalimbali.

“Nilifurahi sana nilipopata kazi ya kuajiriwa kwa kuwa hicho ndicho kitu nilichokuwa nikikililia kwa siku nyingi, niliahidi kuendelea kuwa mwadilifu kazini kwa kuwaheshimu na kuwatii wakuu wangu wa kazi na kufuata sheria za kazi, hiyo ndio siri ya mafanikio yangu,” anasema

Anasema kuwa kazi ya kuchinja aliianza rasmi mwaka 1979 ambapo kwa kupewa mwongozo mzuri na Iddi Kondo Sewando alipata ujasiri wa kufanya kazi hiyo ya kuchinja ng’ombe kiasi ambacho aliwakuna watu wengi machinjioni hapo.

Anasema kuwa siku ya kwanza alipata tabu kidogo kwa kuwa alikuwa akikiona kitendo hicho cha kuchinja katika mawazo yake siku nzima na kumfanya ashtuke mara kwa mara kutokana na hisia hizo ambazo baada ya kuzoea kazi ziliondoka zenyewe kichwani mwake.

“Kama unavyojua ng’ombe ni kiumbe hai kwa hiyo unapomchinja hushtuka, siku ya kwanza hata mimi mwili ulisisimka, nilishtuka tena niliogopa, lakini kwa kuwa nilitaka kuwa na utendaji bora katika kazi yangu niliongeza ujasiri na hatimaye kuizoea kazi hiyo,” anasema

Anaongeza kuwa baaadye alibobea katika kazi hiyo na kwamba sasa anachinja ng’ombe kati ya 100 hadi 150 kwa usiku mmoja jambo ambalo kwake limekuwa ni la kawaida.

“Kila siku nachinja ng’ombe kati ya 100 hadi 150 na nimeizoea kazi hii sasa najua mbinu nyingi tu za kumchinja ng’ombe tena bila usumbufu na hivyo sio kitu cha kutisha tena kwangu,” anasema

Anasema kuwa alijawa na furaha ya ajabu baada ya kupata mshahara wake wa kwanza akiwa machinjioni hapo ambao ulikuwa ni Sh 380, pesa ambayo alikuwa hajawahi kuipata kama mshahara na hivyo pesa ilimwongezea bidii katika kazi yake hiyo.

Anasema anaipenda sana kazi yake ya uchinjaji kwa kuwa imemletea tija tofauti na kazi alizokuwa akizifanya kipindi cha nyuma na kwamba hali hiyo imemwezesha kujijenga kimaisha na kununua mahitaji muhimu ya familia.

Anasema kuwa kazi hiyo imemwezesha kujenga nyumba ya kuishi iliyoko Buguruni na kuwasomesha watoto wake wanne hadi kufikia kiwango cha elimu ya sekondari na vyuo, ambapo watoto wake wawili ni madereva wa magari wakati, mmoja mwalimu na mwingine ni nesi.

Anasema kuwa uadilifu wake kazini umemjengea heshima kubwa miongoni mwa wafanyakazi wenzake na wakuu wake wa kazi ikiwa ni pamoja na ndugu, jamaa na marafiki ambao wamekuwa wakimpongeza kwa kazi yake hiyo.

“Naishukuru familia na ndugu zangu kwa kuniunga mkono kwa kazi yangu hakuna aliyeonyesha kutoikubali pamoja na kwamba watu wengi wanaiona ni kazi ngumu na inayotia kinyaa lakini ndugu zangu wananipa faraja kwa kuwa wako nyuma yangu wakinipa nguvu ya kusonga mbele katika maisha” anasema

Anasema kuwa changamoto ambazo zinamkabili katika kazi yake ni pamoja na kupata shida ya macho kuona kutokana na madhara yanayotokana na kuona maji ya mimba ya za ng’ombe ambayo yanaathari kubwa katika macho.

Anasema pamoja na kutumia miwani maalumu ya macho lakini bado tatizo hilo ni kikwazo kwake kwa kuwa limemuathiri kwa kiasi kikubwa japo bado yupo imara katika kufanya kazi yake hiyo ya uchinjaji.

Aidha, anasema kuwa changamoto nyingine ni suala la kutopata usingizi wa kutosha hasa kwa kuwa kazi yao huwataka kuifanya kuanzia saa tano usiku hadi saa kumi za alfajiri na wakati mwingine kujikuta wakiendelea kufanya kazi za nyumbani wakati wa mchana.

Anasema zamani wakati akiishi katika nyumba za kupanga majirani zake walibaki na maswali na wengine kumhisi vibaya kuwa labda ni mwizi hasa kutokana na kufanya kazi usiku na mchana kulala huku familia yake ikikaangiza nyama kila siku.

“Changamoto nyingi ni za kawaida tu, lakini hili la madhara ya maji ya mamba za ng’ombe ndilo kubwa zaidi na inahitaji umakini zaidi vinginevyo unaweza kuishia kuwa kipofu hapo baadaye,” anasema

Hata hivyo, Hemba anawashauri vijana kujishughulisha na kuacha kusubiri kupata kazi kirahisi kama ambayo vijana wengi wamekuwa wakidhania na kukaa vijiweni kusubiri kupata kazi rahisirahisi na zenye mshahara mkubwa.

Anasema kuwa wakati anaanza yeye kazi alijitolea kwa miaka miwili na baadae kuajiriwa jamno ambalo hata vijana wa leo wanapaswa kuliiga kwa kuwa subira huvuta heri na huonyesha ukomavu na nia ya kazi husika.

“Vijana wanapaswa kutambua kuwa huu sio wakati wa kuzembea kusubiri kazi rahisi rahisi tena zenye mshahara mkubwa, mimi nilianza kuuza karanga, kufanya kazi kwenya mashirika kama kibarua na hatimaye sasa niko hapa machinjioni ni matunda ya uvumilivu wangu” anasema Hemba

Aidha Hemba anawashauri vijana ambao watapenda kufanya kazi ya uchinjaji wanaweza kufika katika machinjio hayo kwa kuwa kuna mafunzo mbalimbali huwa yanatolewa kwa vijana kwa ajili ya kuandaa wachinjaji wa kizazi kijacho.

“Baada ya kuifanya kazi hii kwa miaka 32 ninatarajia kustaafu kazi hii mwakani, kwa hiyo ni vizuri kupata vijana ambao wataendeleza fani hii na kuna mafunzo mengi yamekuwa yakiendeshwa na asasi mbalimbali za kiraia juu ya namna ya kuchinja kwa ubora zaidi kwa hiyo vijana wasisite kujitokeza ili kujifunza,” anamalizia.

SHIKAMOO BABU.

Mtoto Colins Mustafa, akimsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye tamasha la pasaka lilofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

KIBONGO BONGO HII IMEKAAJE?

  • Waandishi Habari wawili waliokuwa wamekamatwa nchini Uganda kutokana na kibonzo kilichochapishwa katika jarida lao wameachiliwa kwa dhamana, lakini wameamriwa kuripoti katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi, CID, ili kujieleza. Walifika huko siku ya Alhamisi lakini wamesema hakuna walichoambiwa bali kuamriwa kurudi tena siku ya Ijumaa.
  • Mhariri wa jarida la kila mwezi Summit Business Review, Mustapha Mugisa pamoja na mchapishaji wake Dk Samuel Sejjaka, inadaiwa walikuwa na nia ya kumkejeli kiongozi wa taifa.
  • Walikamatwa mapema wiki hii, na wakili wao, Murungi Godwin, alisema wateja wake wamekuwa wakiripoti katika kituo cha polisi, pasipo kuchelewa, na kilichofanyika Alhamisi, ni kama kuwaongezea dhamana.
  • "Waliachiliwa kwa dhamana, na kutakikana kuripoti jana, na tulipofika hapo, afisa aliyekuwa anasimamia kesi hiyo, alitueleza turipoti tena leo", alielezea Murungi.
  • Mhariri wa jarida hilo ambalo huchapishwa kwa Kiingereza, Mustapha Mugisa, alisema askari wapatao kumi waliingia afisini mwake, na kumuuliza ikiwa yeye ndiye mhariri wa jarida hilo, na alipothibitisha hayo, walimuelezea lilikuwa na kibonzo, na ilielekea jarida lilikuwa na nia mbaya ya kisiasa, na hivyo wakamkamata.