.

Monday, January 31, 2011

MAPENZI KUAMINIANA

     Raha ya mapenzi ni kuaminiana .Kama unampenda mpenzi wako ni vyema ukamuamini ili kuwe na mani kati yenu.haipendezi kila anakokwenda mpenzi wako unakuwa na wasiwasi nae hii inamnyima sana amani mpenzi wako na wakati mwingine hukasirika .Jenga tabia ya kuaminiana kwa kumuamini mwenzio kutaleta raha katika penzi lenu pia likadumu kwa muda mrefu kwakuwa mnaaminiana ,Popote atakapokwenda mwenzio utakuwa huna wasiwasi kwa sababu una imani na  penzi lako kwake  . Imani katika penzi ni msingi mzuri wa kuleta amani katika maisha ya mpenzi na wakati wingine hata unapokuwa mbali na mwenzio anakuwa anakukumbuka kwakuwa mnapokuwa pamoja mnakuwa na mazungumzo mazuru vicheko na kila mmja anazidi kuwa na furaha na ndipo hapo mnaamua kuingia katika maamuzi mazuri ya kuwa mwili mmoja .Fanya hivyo itakusaidia sana  jenga imani na mpenzi wako.
 kwa leo tuishie hapa..

Friday, January 28, 2011

UNAWAFAHAMU WATU HAWA??????


Shafi Adam Shafi na Amir  Andanenga,katika kipindi cha kumepambazuka kiswahili Radio One.

                  Shafi Adam Shafi, Maulid Kambaya  na Amir  Andanenga,
 Ni watu wenye mchango mkubwa sana katika nchi yetu  ya Tanzania. hasa katika ukuzaji wa lugha adhimu sana ya kiswahili Pamoja na utambulishaji utamaduni wa mswahili ndani na nje ya mipaka yake.
Shafi Adam Shafi ndiye Mtunzi wa Riwaya ya Siti Binti Saad,Kuli,Vuta Nikuvute,Uhaini na vingine vingi.
 Amir Andanenga yeye ni mtunzi wa ushairi Bahari ya elimu ya Ushairi,Diwani ya Ustadh Andanenga,na sasa yuko katika mkakati wa kutengeneza muswaada wa ushairi tangu 1961
Mtangazaji wa Radio One stereo Maulid Kambaya alipokuwa katika kipindi cha kumepambazuka  kiswahili akiwa na wataalamu wa lugha hii Shafi Adam Shafi na Andanenga

AMINI USIAMINI HII NI ZAHATI .

                               Hii ni Zahanati iliyoko Mkoani Morogoro kijiji cha kisaki Bwakila
                                        Hawa ni baadhi ya wagonjwa katika zahanati hiyo

Thursday, January 27, 2011

WANAWAKE OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

Mwanafunzi aliyeongoza mtihani wa kidato cha nne kitaifa mwaka 2010,Lucylight Mallya (18),amebainika kuwa ni yatima ambaye wazazi wake wote wawili walifariki dunia miaka minne iliyopita.
anasema hakutegemea kama angekuwa wa kwanza na anamshukuru sana mungu na walezi wake waliofanikisha kufika hapo alipo..
Binti huyo alikuwa akisoma katika shule ya sekondari ya marian iliyoko mkoani pwani ,amekuwa akipenda sana kemia na biologia na fizikia .

VODACOM WAZINDUA SIMU MPYA KWA WALEMAVU

Mkuu wa kitengo cha mauzo wa Vodacom Tanzania Upendo Richard akionesha simu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuskia na kuona..kushoto ni meneja mawasilianao wa kampuni hiyo Nector Foya na kulia Msimamizi wa kitengo cha mauzo wa kampuni hiyo Ngope Kiwanga
Simu maalumu kwa watu wenye matatizo ya kusikia na wasioona pia.Baadhi ya huduma zilizopo katika siimu hiyo ni pamoj na maandishi makubwa katika keypard zake,sauti kubwa sana katika spika zake na kingora maalumu juu ya simu kitakachowawezesha  kuwasiliana wakati wa dharura.
Ni tofauti na simu za kawaida kwani huduma zilizopo katika simu hii hazipatikani katika simu za kawaida.
Simu hizo ni pamoja na S306ZTE ambapo zinapatikana katika maduka mbalimbali maarufu kama vodashop au kwa mawakala wote wa Vodacom waliopo nchi nzima.

Tuesday, January 25, 2011

KWA RAHA ZANGU

                                                Nimetoa  sana ofa leo sitaki mtu hapa 

DUNIA INA MAMBO

Wewe maziwa hutaki kunvwa kwa afya wacha niwape maziwa vitoweo vyangu .

IPP MEDIA KATIKA CHAKULA CHA MCHANA NA WALEMAVU

                                     Zoezi hili lilichukua nafasi katika ukumbi wa Diamond jubilee
 Mwenyekiti wa Ipp Media Bw Reginald Mengi akiongea na walemavu waliohudhuria kwa kuwatia moyo wa kutokata tamaa katika maisha.
                                         Wazee wa ze comedy nao hawakuwa nyuma
 Mhalatito tukishow Love kwa kuwahudumia wenzetu walemavu Hanifa Hamidu na Salma Dacotha( WAMILIKI WA BLOG HII .KARIBUNI WADAU)
 Mmmmmmmmhhhhhhhhh!!!!!!! Jamani mtoto mzuri...I feel this babyyyy.
 Salma Dacotha na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi
 Waheshimiwa pia walikuwepo.........hapa hapa ndo pakupigia picha ukienda bungeni ntakupata wapi..mh Olesendeka
 Daaaah kiukweli hili tabasamu ni kwa ajili ya huyu mtoto.alinivutia sana ..so cuteeeeeee!!!Lady Hanifa
 Watangazaji wa Capital Tv na Radio nao hawakuwa nyuma ktk kushow love.Glory,Amri Massare,Sara Kipingu
 Dominic Nyalifa wa EATV akikusanya picha za hi 5.ha ha ha ha ha !!!!!!!
 Kwa upande wa burudani wasanii kibao walipaform.mama some food lady jd akiwapa mzuka walemavu
Alikiba nae akiwapa salamu za R kelly.Walikuwepo pia Chid Benz,Ay & Fa,Banana Zorro,Diamond,Marlaw na wengineo pamoja na vikundi mbalimbali vya burudani vya walemavu....Zoezi lilienda vizuri ,Walifurahi na kumtakia maisha marefu Bw Reginald Mengi.

HAPPY BIRDHDAY OBBY

 Siku ya kuzaliwa mtoto wa Salma Dacotha Palikuwa hapatoshi maeneo ya Picollo Hotel,Salma Dacotha aligeuka Samaki Siku hiyo.Hongera mama kwa Kuleta Handsome Boy duniani.
 Tulijumuika kwa pamoja ma girlfriends.kushoto Salma Dacotha,Mecky,Sara kipingu wa Capital Radio na mtoto wake sasha,hanifa Hamidu (lady hanifa) na handsome obby
                                                          Obby anapenda sana mpira
                 Lovely son Obby- happy Birthday mwaka 1.mmmmmh obby  mbona umenuna
                             Obby akimlisha keki mama yake Salma Dacotha

Thursday, January 20, 2011

KARIBU SUMAITA UHITAJI KWENDA SOKONI


 SUMAITA COMPAN ,wasambazaji wa matunda majumbani,maofisini,   huhitaji kwenda sokoni kwani wao wanakuletea bidhaa uitakayo mpaka mlangoni kwako . Wasiliana nao kwa kuwapigia simu, namba yao  ipo hapo juu kwenye tangazo.  Upande wa malipo ni wewe mwenyewe kuchagua ulipe kwa siku ,mwezi au kwa wiki ,Unatakiwa kumwambia yule atakae kuwa nyumbani  mzingo unapokuja anatakiwa kusaini fomu kama mzigo atakuwa ameupokea kwa walio Tanzania .
                 KARIBU SANA SUMAITA COMPANY TUPO TEGETA BASIHAYA

Tuesday, January 18, 2011

RAHA YA PENZI HESHIMA

Ni kweli ukubali au ukatae penzi lenye heshima lina raha yake , kuna watu unawakuta wanaongea lugha ya matusi utadhani sio wapenzi haipendezi ,Na hapo inawezekana  bado hawajawa na  familiia,Hivi  endapo watabahatika kuipata familia jamani itakuwa na maadili yapi kama sio watoto wenye matusi kama wazazi wao????? Haipendezi jamani kama unafanya hivyo acha mpaka mpenzi wako akushangae kwa mabadiliko yako . Penzi likiwa na Heshima kwani ,Hata mpenzi wako anaona raha kukutambulisha kwa rafiki zake anajuwa huwezi kumtia aibu mbele ya watu wake  ,unapokuwa na lugha mbaya unaweza ukawa unakimbiwa hatoki na wewe kwa kujuwa utamtia aibu  na hii ni kwa wote tubadilike.
                                 MPENDE MWENZIO,MPE THAMANI YAKE NA UMUHESHIMU.

Monday, January 17, 2011

HAPPY BIRTHDAY FIRST LADY


                                                  Hongera mama kwa kutimiza mika 47.
 Ni mtu wa tabasamu muda wote inawezekana ndo maana ana ngozi nzuri

                                                       Kabla hajatupia kitu cha makeup

                                             Tayari ameshatupia kitu cha makeup
                                                        Umeichabo hair style hiyo

                                                            Nyingine hiyooooooooooo

                                                             hapo jeeeeeeeeeeeeeeeeee

 Michelle ni mwanamke wa fasion kiukweli,cheki vivazi vyake

                                     Usisikie anawapenda sana watoto wake,sasha na malia.

Saturday, January 15, 2011

UPEPO UNAPOBADILIK KATIKA MAPENZI


Hali hii huwaumiza watu wengi sana na kuiona dunia chungu na kukumbuka mengi sana

kila mmoja hujionabora awe  peke yake ukweli usiombe hali hii ikukute  mapenzi matam sana ila ikifikia hapa ni machungu sana usukubali haya yakukute


MBWEMBWE ZA MAPENZI MAPYA

Penzi likiwa jipya lina raha sana kwani kila wakati mna raha ajabu hamtamani kuachiliana

mnakuwa kama watoto full kicheko
                            

                                                                        full mibusu

Friday, January 14, 2011

ISOME KIMYA KIMYA

                                                    kifaa kingine cha radio one.Ayam shekifu