.

Monday, August 22, 2011

LADY HANIFA'S BIRTHDAY PARTY.........!!!!!!!!

Jumamosi ya tarehe 20 August ilikuwa siku ya kuzaliwa ya bibie Hanifa Hamidu aka Lady Hanifa ambaye ni mtankgazaji mahiri wa kituo cha ITV na radio One katika kipindi cha yaliyomo yamo kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Alhamisi saa tatu kamili asubuhi hadi sita mchana.....

Maandalizi yalianza kwa futari kwa rafiki yake kipenzi Salma Dacotha na baadae party kiaina.....


Maakuli yalikuwa kama hivyo ftari mwezi mtukufu
Hanifa akijisevia
Salma akipata ftari
Keki ilikuwa ya Chelsea cz Hanifa ni mpenzi wa timu hiyo na siku hiyo ilikuwa inacheza

Hanifa na rafiki yake ambaye wamezaliwa siku moja wote ni birthday girls
Hanifa akimlisha keki shostito wake Salma Dacotha

BATA TIME!!!............NJOO TULE BATA NA CRUISE PARTY!!!!!!!

YAMEMFIKA GADAFFI....................HALI MBAYA TRIPOLI..!!!!!

Mapigano makali yanaendelea katika maeneo yanayozunguka makazi ya kiongozi wa Libya kanali Muammar Gaddafi baada ya majeshi ya waasi kushika udhibiti wa mji huo jana jioni.

Usiku kucha mji huo uligubikwa na sherehe kutoka kwa maelfu ya watu waliokusanyika katikati ya mji huo katika eneo maarufu linatambulika kama uwanja wa kijani(Green Square)
Msemaji wa jeshi la waasi amesema jeshi hilo lilikabiliwa na upinzani kidogo wakati wakilitwaa eneo la mashariki,kusini na magharibu mwa mji wa Tripoli.

AY NA FA,SHUSHO NA MSONDO WANYAKUA TUZO ZA EEMA'S


Mabeste,AY na B12 wakiwakilisha kupokea tuzo hizo

Siku ya Jumamosi zimefanyika Tuzo za East Africa Music Award (EMAS) kule Nairobi Kenya na kutoka Tanzania walioshinda ni Msondo Ngoma katika Best Group of Rumba.

Best Group of Rumba Msondo Ngoma
Best Collabo Urban Contemporary ni AY & Mwana FA ambapo kwenye Female Gospel Category mshindi ni mwimbaji wa Injili mahiri Christina Shusho. 

Best Collabo Urban Contemporary AY & Mwana FA
Female Gospel Category Christina Shusho. 

CHAMELEONE AOMBA RADHI WAISLAMU..............!!!!!!!!!

Jose Chameleone
Msanii kutoka Uganda Jose Chameleone aka Joseph Mayanja leo ameandika barua kwa jamii ya waislamu akiomba msamaha kwa kushindwa kutimiza ahadi yake ya kiimani ambapo hivi karibuni alibadili dini na kuwa muislamu na siku chache kurejea kwenye dini yake ya kikristu.

Barua yeyenyewe ilikuwa inasomeka hivi ambayo imeelezea nafasi yake na kwanini amechukua uamuzi huo.


Date: 22nd August 2011

To: THE MUSLIM COMMUNITY

C/o: Prince Kassim Nnakibinge

Dear Sir,

RE: APOLOGY.

I Joseph Chameleone Mayanja humbly writes this letter to thank you for everything you are doing for the Islamic community, Buganda and Uganda at large.

Sir,

Through you, I kindly apologise to the entire Muslim community for not fulfilling my testimony of faith. As I promised before you, my Muslim brothers and sisters. I, on my own, decided to join the Islamic faith hardly knowing of the fore coming hardships and unfair judgment I would face.

I would never be bothered by simple public opinion and judgment until my Clan, Family and Wife who have been very supportive in my life condemned me without mercy and out casted me.

Sir in all due respect for Islam,

I ask for mercy and forgiveness.

Thank you.

Truly Yours

Joseph Mayanja Chameleone.

Cc: The Imam

Kibuli Mosque

Cc: The Mufti,

Muslim Community of Uganda.

KIM KARDASHIAN NA KRIS HUMPHRIES WAFUNGA NDOA..................

Mlimbwende Kim Kardashian na mchezaji wa mpira wa kikapu wa NBA Kris Humphries wamefunga ndoa huko katika jimbo la Montecito,California siku ya Jumamosi usiku.

Kardashian alitupia gauni matata lililobuniwa na Vera Wang ambalo kwa mujibu wa ripoti lilikuwa Inspired na gauni alilovaa Pippa Middleton katika harusi ya kifalme iliyofungwa Uingereza Aprili mwaka huu ambapo wasimamizi pamoja na mama yake Kardashian walivaa nguo za Disigner huyo.

Maceleb waliofika katika party hiyo ni pamoja na Eva Longoria, Lindsay Lohan na Melanie Brown, ambaye alikuwa na hofu ya ukubwa wa ujauzito wake kumkosesha siku hiyo kubwa.

Endelea kufatilia blog hii kwa picha kamili za siku hiyo kubwa kwa bibie Kim K.........