.

Thursday, December 30, 2010

Tuesday, December 28, 2010

Khadija Kopa alizwa

Hivi karibuni bi Khadija Omari Kopa ambayae kwa sasa anafanya kipindi cha yaliyomo yamo kwenye segment ya kimasomaso aliibiwa baadhi ya vitu vyake vya ndani na vito vyake vyote vya dhahabu na watu wasiojulukana.
Pole bi Khadija Kopa kwa Maswahiba yaliyokukuta

Tabia za kuepuka ili kuwa na ngozi nzuri

 Mwanamke anafaa kuweka ngozi yake ivutie na kuwa nadhifu wakati wote. Kuna baadhi ya wanawake wanadhani kuwa nadhifu na kuvutia ni kupaka vipodozi vya aina mbalimbali na vya gharama, hapana, suala la muhimu zaidi ni kujua namna gani unaweza kuitunza ngozi yako ili ipendeze na kuwa yenye afya.
 Kwanza kabisa unapaswa kuepuka msongo wa mawazo na hasira, wakati wote jaribu kuwa mtu mwenye furaha zaidi. Wataalam wanasema mikunjo inayoonekana kwenye nyuso za wanawake wengi, inasababishwa na wao kuwa wenye huzuni au kuwaza mambo mengi yanayopelekea kutoweka kwa furaha yao.
Hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unaepuka vitu vinavyosababisha hasira katika maisha ya kila siku na kama ni ngumu kuepuka basi hakikisha hauviweki moyoni ili kudumisha furaha yako.
 Pili, wanawake tumekuwa muda wetu mwingi tunautumia katika mihangaiko na tunasahau kupumzisha miili yetu vya kutosha. Ila ili uwe na ngozi yenye afya unapaswa kulala saa 6 mpaka 8 kwa siku ya saa 24, nikimaanisha ukilala saa 4 uamke saa 12 asubuhi na siyo mapema zaidi ya hapo.
 Vyakula tunavyokula pia vinachangia uzuri wa ngozi yako, hivyo tunapaswa kuwa makini sana. Vya kuzingatia katika chakula chetu ni samaki na jamii ya vyakula vya baharini ambavyohusaidia kung’arisha na kulainisha ngozi, matunda haswa machungwa, machenza na maparachichi ni mazuri kwa kulainisha ngozi na kuifanya isiwe kavu, mbogamboga pia ni muhimu katika kutakasha ngozi hususan caroti, mboga za majani na viazi vitamu na mwisho ni nafaka zisizokobolewa kama vile mahindi, mtama au uyoga pia husaidia kuondoa madoa na mabaka kwenye ngozi.
 Kama nilivyosema awali lishe ni muhimu sana katika kuimarisha ngozi yako, pia zingatia vinywaji unavyotumia, vilevi au pombe kali ni sumu kubwa ya ngozi kutokana na tabia ya kusababisha mwili kukaukiwa na maji wakati mwingi. Hivyo ukiwa mtumiaji wa vilevi hakikisha unakunywa maji mengi zaidi ya kawaida ili kufidia maji yanayopotea, na hata bila kutumia pombe maji ni muhimu sana katika kuboresha ngozi. Tumia lita moja na nusu hadi mbili kwa siku.


Juisi ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu, husaidia kufanya ngozi yako kuwa nyororo na hata kuondoa mikunyanzi , matunda pia ni muhimu sanaaaaaaaa.

Usafi wa ngozi pia ni muhimu sana katika urembo, ngozi hususan ya uso ni muhimu kuoshwa mara mbili au tatu kwa siku yani asubuhi na jioni, kama ikiwekana mchana pia kulingana na aina ya ngozi yako na mahitaji yake. Tumia maji ya uvuguvugu kusafisha uso ila kuondoa uchafu na mafuta yasiyohitajika usoni, pia zingatia aina ya sabuni unayotumia iendanena ngozi yako, kama inawezekana nunua sabuni maalum kwa ajili ya uso.

Usiku kabla ya kwenda kulala hakikisha unapaka losheni maalum kwa ajili ya kutunza unyevu wa ngozi yako. Ukienda kwenye maduka ya dawa au vipodozi ulizia “moisturizer ya ngozi” ili kuhakikisha ngozi yako haikauki wala kukakamaa.

Na kwa wale wavutaji wa sigara, matokeo mazuri ya ngozi hayatapatikana isipokuwa kwa kuacha kuvuta sigara. Sumu inayotokana na sigara husababisha ngozi kusinyaa na kuzeeka, hivyo kufanya ngozi kupoteza mvuto wake.

Natumaini kwa leo umejifunza mambo mengi kuhusiana na ngozi pamoja na matunzo yake. Mambo muhimu ya kuzingatia ni lishe, usafi, muda wa kupumzika na pia kuepuka sigara, pombe na mawazo ya mara kwa mara.

Friday, December 24, 2010

NDANI YA DUKA LA SHEAR ILLUSITION MILLENIUM TOWER

 Ni Grace Luhinda, kutoka Shear Illusion ambaye unampata kila Jumanne na Jumatano katika makala ya urembo ndani ya Yaliyomo Yamo usikose
 Grace Luhinda na Salma Dacotha

Wednesday, December 22, 2010