.

Saturday, May 7, 2011

"JAMANI MOURINHO JAMANI NDIYO HATUTAMUONA?"

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amepewa adhabu ya mechi tano kwa mechi za Ulaya, kutokana na matukio wakati wa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya, dhidi ya Barcelona.

Chama cha soka Ulaya, UEFA, kimesema Mourinho alitoa matamshi "yasiyofaa", baada ya Real Madrid kufungwa 2-0 na Barcelona, akiwatuhumu waamuzi kwa kujaribu kuisaidia Barcelona.
Mourinho tayari ametumikia adhabu ya mchezo mmoja kukaa jukwaani, katika mchezo wa pili, na michezo mingine mitano itatekelezwa iwapo atafanya makosa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
UEFA pia imemfungia kutocheza mchezo wa fainali kipa wa Barca wa akiba Jose Pinto.

"TOO MUCH IS HARMFULL"

Mbona kila kukicha kuna wimbi la waganga wa jadi wjanajitokeza? hivi hata mikoani kuna mabango ya  MGANGA TOKA DAR? Kwanini wasiungane na kujenga hospitali ya pamoja ili tujue kua huduma zao zinapatikana sehemu flani. Mara utaona huyu anatibu hiki mara kile ilimradi tu ni mganga hata kama hana uzoefu na kitu hicho.