.

Friday, May 6, 2011

Siku kadhaa sasa toka kutangazwa kuuawa kwa kiongozi wa ugaidi Duniani Osama Ben Laden, Jiji la New York City ulinzi umeongezeka maradufu kila pande , hasa sehemu huska ya milipoko ya majengo marefu ya WTC. na ni kituo kukubwa na Train ya chini inayoelekea New Jersey ijulikanayo kwajina la PATH. Sehemu hiyo kama unavyoiona watu wanaendelea kuweka maua kama heshima ya kuwa kumbuka ndugu na jamaa, na vyombo vya habari kutoka kila pande wameweka kambi muda hapo hili mradi tu waweze kutoa habari  LIVE kutoka sehemu hii ambayo ujenzi wake unaendelea. Na pia wakimsubiri Mh Rais wa Marekani Barack Obama ambae anakuja siku ya alhamisi   kuongea na ndugu na jamaa  waliopoteza wapendwa wao. pia kuja kutoa shukrani kwa jeshi lake kwa kazi kubwa waliyoifanya na kufanikiwa kumwangamiza kiongozi huyo wa ugaidi duniani. Picha kwa hisani ya (NY Ebra wa NYC) alietembelea sehemu hiyo kuangalia hali inavyoendelea kwa sasa baada ya kutangazwa  kuuawa kwa Osama Ben Laden.
Ulinzi mkali uk5 c X[apey6l0p45-ey o6m-45ks,h -94kiyh7iendelea New York City
Wakaazi wa mji huo wakiendelea kuweka maua Ground Zero
Waandishi wa vyombo mabali mbali vya habari ndani na nje ya Marekani wakiendelea kufunga mitambo yao kwa kuwatangazia wadau LIVE nini kinachoendelea Ground Zero

HILI NDIYO TAIFA LA KESHO.

KOVA: WANAWAKE KUWENI MAKINI.

JESHI la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewatahadharisha wanawake nchini, kutodanganyika kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume papo kwa papo kwa kuwa kumekuwa na wimbi la mauaji wanawake baada ya kujitokeza mwanaume anayewarubuni.
  Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suileman Kova, amesema amejitokeza mwanaume anayetuhumiwa kuua wanawake waliofikia wanne jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Tandika, Keko, Mtoni kwa Azizi Ally na Buguruni kwa Mnyamani katika kipindi cha miezi mitatu.

Amesema mwanaume huyo amekuwa akirubuni wanawake hao kimapenzi kwa kuwaahidi donge nono la fedha na kisha kwenda nao katika nyumba za kulala wageni na kuwalazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile na anapomaliza haja zake kuwanyonga.

Kova amesema katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi limebaini kuwa katika nyumba zote za wageni walizouawa wanawake hao wamebaini ni mwanaume wa aina moja ambaye wahudumu wa nyumba hizo walipoeleza mazingira na maelezo yao yamefafana na kudai kuwa mwanaume huyo hupendelea kuvaa vazi la T-shirt na suruali aina ya jeans, mweupe, mtanashati na kukadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 32.

Kova amesema mtuhumiwa huyo ambaye anasakwa ameonekana kuwalenga wanawake ambao wako ndoani [wake za watu] kwa kuwarubuni kuwaahidi fedha nzuri na kasha kuwanyonga na kutokome bila hata kuiba kitu chochote kutoka kwa marehemu.
.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kumsaka mtuhumiwa huyo kumkamata na kumchukulia hatua zinazostahili na jamii wametakwi kutoa ushirikiano katika suala hilo.

CHACHU NA TAMU YA MAPENZI.

Mwanaume mmoja wa nchini Italia alitumia zaidi ya dola nusu milioni kwaajili ya zawadi na maandalizi ya harusi na mchumba wake lakini siku ya harusi alibaki akilia baada ya kuachwa solemba kanisani huku bi harusi wake akitoroka na mwanaume mwingine.
 
Mwanaume wa nchini ya Italia ambaye alionja chachu ya mapenzi baada ya kutorokwa na mpenzi wake siku harusi ameenda mahakamani kudai fidia ya dola za Kimarekani 743,000 kwa kuvunjwa moyo na kuchezewa hisia zake na pia kupoteza kiasi kikubwa cha pesa.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 32 alitumia pesa nyingi kwaajili ya maandalizi ya harusi na mchumba wake huyo lakini siku ya harusi mchumba wake aliroroka na mwanaume mwingine.

Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Riccardo, alikodisha jumba la kifahari kwaajili ya harusi yao nje kidogo ya jiji la Rome, alikodisha hoteli kwenye kisiwa kimoja cha Pacific kwaajili ya Honeymoon (fungate) na pia aliifanyia marekebisho makubwa nyumba yake ili kukidhi mahitaji ya mke wake mtarajiwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Italia, ANSA, siku ya harusi Riccardo na familia yake na ndugu na jamaa walikuwa tayari kanisani wakimsubiri bi harusi awasili lakini badala yake aliwasili kaka wa bi harusi ambaye alimwambia Riccardo kuwa dada yake hatakuja kwenye harusi.

Mchungaji alilazimika kuvunja shughuli zote za harusi baada ya kuambiwa kuwa bi harusi ameteroka na mwanaume mwingine ambaye alikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Taarifa zimesema kuwa Riccardo amekodisha wanasheria kwaajili ya kumfungulia kesi aliyekuwa bi harusi wake akimtaka yeye na familia yake walipe gharama zote za harusi alizoingia.

"JAMANI MIMI SIYO BILLIONEA NI VIJISENT TU HIVI VYA MBOGA"

MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete ameukana ubilionea aliovishwa na wanasiasa wa vyama vya upinzani.
  Amekanusha hayo baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, kuutangazia umma kuwa ni Ridhiwani Kikwete ni bilionea na kuhoji ubilionea wake umetoka wapi.

Ridhiwani aliwataka Watanzania wasimhukumu kwa kumuona mitaani akiendesha magari ya bei ghali.

“Mi naishi na watu vizuri hapa mjini jamani, tunaishi kimjini mjini na si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake,”, alisema Ridhiwani.

"Hii inatokana na malezi ya wazazi wangu yaliyonieleza kuishi na watu vizuri”, alieleza Ridhiwani

“Hayo wanayonizushia mimi kuwa ni bilionea na namiliki kampuni ya malori 150 na kampuni ya ujenzi pamoja na ghorofa za kupangisha mjini mimi nasema si kweli”.

Alibainisha kuwa habari hizo ni za uongo na uzushi na zimelenga kumchafua yeye na mzazi wake na kupandikiza chuki dhidi ya familia yake na jamii.

Alisema hatua waliyochukua si nzuri na kubainisha kuwa anawaheshimu sana kutokana na umri wao na kuwataka watoe ushahidi wa hayo kwenye vyombo vya habari

Hata hivyo Ridhiwani alibainisha mali zake anazomiliki kuwa ni shamba la hekari moja na nusu lililopo Bagamoyo, gari aina ya Toyota Cami na akaunti mbili katika benki za Stanbic na NBC.

"KWELI BABA YANGU KAUWAWA"

Mtoto wa kike wa Osama bin Laden amesema kuwa baba yake alikamatwa akiwa hai kabla ya kuuliwa kwa kupigwa risasi mbele yake na wanajeshi wa kikosi maalumu cha Marekani.
Televisheni ya Al-Arabiya iliwanukuu maafisa usalama wa ngazi za juu wa Pakistan wakisema kuwa binti huyo wa Osama mwenye umri wa miaka 12, aliwaambia kuwa baba yake aliuliwa mbele ya familia yake na kisha mwili wake kuburuzwa hadi kwenye helikopta ya Marekani.

Mwili wa mtoto wa kiume wa Osama nao ulichukuliwa na wanajeshi wa Marekani na kupakizwa kwenye helikopta.

Televisheni ya Al-Arabiya iliwanukuu maafisa usalama wa Pakistan wakisema kuwa watoto sita wa Osama bin Laden, mmoja wa wake zake na mwanamke mmoja toka Yemen ambaye inasemekana alikuwa daktari wake walisafirishwa hadi kwenye mji wa Rawalpindi karibu na mji wa Islamabad, kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya jeshi.

"Hivi sasa wanapatiwa matibabu kwenye hospitali ya jeshi ya Rawalpindi" alisema mmoja wa Maafisa usalama wa Pakistan na kuongeza kuwa mke wa Osama bin Laden aliwaambia kuwa wamekuwa wakiishi Abbottabad kwenye nyumba hiyo kwa miezi sita sasa.

Afisa mwingine wa ngazi za juu wa Pakistan alisema kuwa baadhi ya taarifa zilizotolewa na Marekani kuhusiana na kukamatwa na kuuliwa kwa Osama hazina ukweli ndani yake.

"Hakuna hata risasi moja iliyopigwa toka kwenye nyumba ya Osama, ndege yao ya kivita ilipata matatizo ya kiufundi angani na ilianguka kwenye eneo la tukio".

Maafisa usalama wa Pakistan walisema kuwa hawakukuta silaha yoyote wala mabomu wakati walipofanya msako wa nguvu ndani ya nyumba ya Osama baada ya maiti yake kuchukuliwa na Marekani.

Uchunguzi wa kwanza ulifanyika jumatatu na jumanne walirudia kufanya msako kwenye nyumba hiyo yenye vyumba 13. Walichokuta ndani ya nyumba ya Osama ni nyati wawili, ng'ombe mmoja na kuku wapatao 150.

"Kulikuwa hakuna handaki wala sehemu maalumu ya kujificha ndani ya nyumba hiyo, ndio maana sielewi kwanini mtu anayetafutwa kuliko watu wote duniani alienda kuishi pale", alisema afisa huyo wa Usalama wa Pakistan.

KWELI PALICHIMBIKA.

Picha hizi za kutisha za maiti za watu waliouliwa ndani ya nyumba ya Osama bin Laden unaweza ukaziona lakini picha za maiti ya Osama bin Laden mwenyewe hautaiona kamwe kwani rais Barack Obama wa Marekani ameishatangaza kuwa picha hizo hazitatolewa kamwe.
Picha hizi za kutisha zinaonyesha maiti za wapambe wa Osama bin Laden ambao waliuliwa wakati kikosi maalumu cha jeshi la Marekani kilipovamia nyumba ya Osama bin Laden na kumuua Osama bin Laden.

Picha hizi zilipigwa na maafisa usalama wa Pakistan ambao waliingia kwenye nyumba ya Osama bin Laden mapema asubuhi ya jumatatu baada ya Marekani kuvamia kwenye nyumba hiyo kumuua Osama bin Laden na kisha kuondoka na maiti yake.

Maafisa usalama wa Pakistan ambao hawakutaka kutaja majina yao walizipiga picha hizo na kisha kuziuza kwa gazeti la The Gurdian la Uingereza.

Shirika la habari la Reuters limethibitisha kuwa picha hizo ni za kweli na zilipigwa eneo la tukio.

Kuhusiana na picha ya maiti ya Osama bin Laden, Rais Barack Obama wa Marekani alisema kuwa picha hizo hazitaonyeshwa kamwe kwani zitasababisha mtafaruku na pia zitatumiwa na wapinzani wa Marekani kueneza propaganda za chuki.

Rais Obama alisema kuwa picha za maiti ya Osama bin Laden hazitatolwa na wala picha au video zake wakati akizikwa hazitatolewa lakini aliwahakikishia watu kuwa Osama ameuliwa kweli na kamwe hataonekana tena akitembea kwenye ardhi ya dunia hii.

Gonga linki chini kuona picha za hali ilivyokuwa ndani ya nyumba ya Osama bin Laden na picha maiti za watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo.

WANA NDOA SOMENI HII.

Mwarabu mmoja wa Dubai amefikishwa mahakamani na mkewe na kufunguliwa madai ya fidia ya dola milioni 12.25 kwa kushindwa kumfikisha kileleni mkewe kwenye mambo ya malavi davi na hivyo kumsababishia mkewe mawazo mengi na kumchanganya akili.
Mke wa mwanaume huyo ambaye hakutajwa jina lake aliiambia mahakama kuwa mume wake alikuwa akizua sababu mbalimbali kumnyima unyumba kwa miezi minne ya mwanzo ya ndoa yao iliyofungwa mwaka 2008.

Mwanamke huyo aliendelea kusema kuwa baadae aligundua kuwa mumewe hawezi kazi kitandani kwani alikuwa akisumbuliwa na tatizo la uume wake kutosimama 'dede' hata aimbiwe nyimbo gani, limeripoti gazeti la Gulf News.

"Kwa kuangalia misingi ya tamaduni za kiarabu na jinsi mwanamke anavyochukuliwa katika jamii, niliamua kukaa kimya na kujaribu kuizoea hali hii huku nikiomba Mungu mambo yawe sawa", alisema mwanamke huyo.

Mwanamke huyo aliiambia mahakama kuwa mumewe ameshindwa kumtimizia mahitaji yake.

Aliendelea kuiambia mahakama kuwa mumewe alimsimamisha kazi kabla ya kumuoa na alimvua vidani vyake alivyokuwa navyo wakati huo.

Mwanamke huyo anadai fidia ya dirham milioni 45 ambazo ni sawa na dola milioni 12.25 kama fidia ya mumewe kumchanganya akili na kumsababishia mawazo mengi kwa kutomtimizia mahitaji yake.

ALIYEJICHOMA MOTO KUFUNGULIWA MGAHAWA.

MWANAMKE mmoja [32] mkazi wa jijini Dar es Salaam, aliyeweza kujiunguza na maji ya moto ili aweze kuomba barabarani apatiwe mtaji, nduguze wamfungulia mradi wa kuendesha mgahawa eneo la Buguruni.

Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, ndugu waliomkataza aachane na kuomba barabarani kwa pamoja walishirikiana kumtafutia mtaji na kumfungulia mgahawa ikiwa ni kumtaka aendeshe maisha yake pasipo kuomba.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo tayari ameshaanza biashara hiyo mwanzoni mwa wiki hii na kudaiwa kuwashukuru ndugu zake waliojitolea kumfungulia biashara hiyo.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo anaapa kutokuwa na hamu ya kuolewa kwa kuwa tayari alishapata mateso kutoka kwa mtalaka wake ambaye alimtelekeza na mtoto na kuishi maisha magumu yaliyompelekea kuomba ili ndugu zake waweze kumsaidia.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alitumia mbinu ya kuomba barabarani ili aweze kupatiwa msada na ndugu zake kwa kuwa ndugu hao hakuna aliyeamini kama angekosa mtaji kwa kuwa ilidaiwa alikuwa na maisha ya juu alipokuwa na mumuwe huyo.