.

Friday, July 15, 2011

PATTY LABELLE




Jina lake halisi ni Patricia Louise Holt Edwards alizaliwa miaka 67 iliyopita ni mwanamama mwimbaji kutoka nchini Marekani,mwandishi pamoja na mwigizaji pia.Patty Labelle alitumia miaka 16 kama mwimbaji kiongozi wa kundi la  Patti LaBelle and the Bluebelles ambalo lilibadilisha jina na kuitwa Labelle mwanzoni mwa miaka ya 70 na kutoa nyimbo maarufu ya disco ilipewa jina la "Lady Marmalade".






Mwanamama huyo aliolewa mwaka na mume wake Armstead Edwards Julai 1973 na kumzaa mtoto wao wa kwanza na wa pekee Zuri Kye Edwards na mwishoni mwa mwaka 1970 Labelle na mume wake Edwards waliasili watoto Stanley na Todd baada ya mama yao kufariki kwa ugonjwa wa saratani.




Patty Labelle ameendelea kukonga nyoyo za watu kwa vibao vyake vikali vya miaka hiyo vinavyotamba hadi leo na huchoki kusikia kwenye masikio yako kama ''If You Asked Me To'',"Stir It Up" na "New Attitude" na nyimbo nyingine kama "You Are My Friend" na "Love, Need and Want You" na ameshawahi kupata tuzo nyingi kupitia fani yake ikiwemo hivi karibuni alipopata tuzo ya Life Time Archivement Award ya BET.

JAJI MWENYE HURUMA NCHINI MAREKANI

Jaji mwenye huruma nchini Uingereza amewashangaza watu waliokuwa mahakamani baada ya kuhairisha hukumu ya  kwenda jela ya mama mmoja ili aende kwanza nyumbani kuwaaga watoto wake kabla ya kuswekwa jela.

Jaji huyo John Wait aliafiki kuwa mama huyo Sandra Hook aliyekuwa mhasibu na kuiba paundi elfu 25 za halmashauri, kuwa anapaswa kwenda kuwakumbatia watoto wake na kuwaga kabla ya kifungo.


 
                                                                   Sandra Hook
Jaji huyo wa mahakama ya Wolverhampton Crown alilazimika kuiharisha hukumu hiyo hapo jana hadi leo, ili mama huyo akawaage wanae na kuwaambia hatorudi tena nyumbani kwani anakabiliwa na kifungo jela.

LIL WAYNE ATOA ''MIXTAPE'' YA BURE

Rapa Lil Wayne amewapatia mashabiki wake watiifu mixtape ya bure  kuwashukuru kwa kuwa wavumilivu kungojea album yake mpya ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.





Hali hiyo imemfanya rapa Lil Wayne kujaribu kuwapooza mashabiki wake watiifu kwa mixtape aliyoipachika jina la 'Sorry 4 The Wait'.

CHRIS BROWN AVILAUMU VYOMBO VYA HABARI




Nyota wa RnB Chris Brown amevitupia lawama vyombo vya habari kwa kutengeneza stori inayomtuhumu kuonyesha ishara ya kuwadhihaki mashoga katika mchezo wa mpira wa kikapu uliofanyika hivi karibuni.


Chris Brown akitoa shukrani katika tuzo za BET

Nyota huyo anayejaribu kujenga wasifu wake kwa jamii tangu tukio la mwaka 2009 la kumtwanga aliyekuwa mpenzi wake Rihanna, inadaiwa alishindwa kudhibiti hasira zake wakati akicheza mpira kwenye gym jijini Los Angeles na kuonyesha ishara ya kudhihaki mashoka kwa mchezaji mwingine.

Kwa mujibu wa jarida moja nchini Marekani, Brown alitoa lugha chafu na kumdhihaki mpinzani wake kwa kutembea kishoga pamoja na kumuonyesha ishara kuwadhihaki mashoga.