.

Wednesday, May 4, 2011

KWLI UBISHI NOMA JAMANI.

Mwanaume mmoja toka Urusi ambaye alikuwa akibishana na wageni wake kuwa bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu Mike Tyson ni mkali zaidi kuliko wababe wa sasa duniani katika ngumi hizo ndugu wawili wa familia ya Klitscho toka Ukraine, ubishi huo umepelekea mwanaume huyo amuue rafiki yake. Ubishi uliozuka kwenye nyumba ya mwalimu Nikolai Makayev wa mji wa Tyumen nchini Urusi ulipelekea mwalimu huyo awacharange kwa kisu wageni wake wawili.

Katika ubishi huo, Nikolai alikuwa akibishana na wageni wake juu ya nani mkali kati ya Mike Tyson na ndugu wawili toka Ukraine wa familia ya Klitschko ambao hivi sasa ndio wanaotamba duniani katika anga ya ngumi za uzito wa juu.

Nikolai ambaye alikuwa akipata ulabu pamoja na wageni wake hao wawili, alitamba kuwa Tyson ndio mkali zaidi kuliko Vitali Klitschko na ndugu yake Wladimir Klitschko.

Wageni wake walimshutumu Nikolai kuwa hana uzalendo kwa kumshabikia Tyson ambaye ni bondia wa Marekani na kuwaacha akina Klitchko ambao wao ni Warusi.

Nikolai alikasirika kuambiwa hivyo na ghafla alichukua kisu na kuanza kumshambulia mgongoni mmoja wa wageni wake.

Mgeni mwingine ambaye naye alikuwa ni rafiki wa karibu wa Nikolai, aliamua kukimbilia nyumbani kwake kunusuru maisha yake ingawa naye alikuwa tayari ameishajeruhiwa kwa kuchomwa na kisu na Nikolai.

Polisi waliitwa lakini hadi wanafika tayari Nikolai alikuwa ameishamuua mmoja wa wageni wake.

Vifo vinavyosababishwa na pombe vimekuwa vikiongezeka nchini Urusi ambapo watu 500,000 huuliwa au hufariki kutokana na ulevi.

Hali hiyo imewaathiri zaidi wanaume nchini Urusi ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki kutokana na ulevi au matatizo yanayotokana na pombe, hali hiyo imesababisha kuwe na idadi kubwa ya wanawake kuliko idadi ya wanaume nchini Urusi
.

"KUMBE OSAMA HAKUA NA SILAHA NYUMBANI KWAKE?"

Kiongozi wa kundi Al-Qaeda Osama Bin Laden hakuwa amejihami wakati alipouawa na majeshi ya Marekani siku ya jumapili baada ya kukataa kukamatwa, ikulu ya White House imesema.
Shirika la kijasusi la Marekani(CIA) limesema halikujulisha Pakistan kuhusu uvamizi huo kutokana na hofu kuwa huenda ingehatarisha operesheni yao.
Pakistan imekanusha ufahamu wa uvamizi huo na idara ya ujasusi wa nchi hiyo imesema imeaibika na kutofaulu kwao.
Maafisa wa Marekani wamesema bado hawajaamua lini watoe picha ''za kutisha'' za mwili wa Bin Laden.
Lakini mkurugenzi wa CIA Leon Panetta ameiambia kituo cha televisheni cha NBC nchini Marekani kuwa bila shaka picha ya mwili wake itatolewa wakati mmoja.
Msemaji wa ikulu ya White House Jay Carney amesema mke wa Bin Laden alipigwa risasi kwenye mguu wake lakini hakuuawa.
Jumapili iliyopita, ikulu ya White House ilisema mwanamke huyo aliuawa katika makabiliano baada ya Bin Laden kumtumia kama ngao.
Bin Laden, mwenye umri wa 54, alikuwa mwanzilishi na kiongozi wa kundi la al-Qaeda. Inaaminika aliamuru mashambulizi yaliyotokea mjini New York na Washington 11 Septemba 2001, pamoja na mashambulizi mengine ambapo watu waliuwawa.

OBAMA -1 OSAMA -0

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa maiti ya Osama bin Laden ilipewa heshima zote na kusaliwa kiislamu kabla ya kuzikwa baharini, lakini maswali mengi yamezuka kwanini azikwe baharini wakati Marekani ingeweza kumzika kwenye ardhi ya sehemu yeyote ile?.
 
Taratibu za kiislamu zinataka maiti izikwe mapema iwezekanavyo badala ya kucheleweshwa isipokuwa iwapo uchunguzi wa kifo cha mtu aliyefariki utahitajika.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa walizingatia sana taratibu za kiislamu kwa kuuzika mwili wa Osama bin Laden ndani ya masaa machache.

"Taratibu za mazishi katika dini ya kiislamu zilifuatwa, maiti yake ilifanyiwa taratibu zote za kidini kwenye kambi ya jeshi, mwili wake ulivalishwa sanda nyeupe, uliwekwa ndani ya mfuko uliowekwa vitu vizito ili uweze kuzama baharini na kisha ulidondoshwa kwenye peninsula ya Uarabuni katika bahari ya Hindi.

Maafisa wa Marekani walisema kuwa tukio hilo lilitokea masaa 12 baada ya Obama kuuliwa kwa kupigwa risasi ya kichwa. Taarifa ya televisheni ya ABC ilisema Osama alipigwa risasi ya pili kwenye kichwa ili kuhakikisha kuwa amefariki dunia.

Mwili wake ulisafirishwa hadi kwenye kambi ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan ambapo sampo yake ya DNA ilipimwa ambapo ilionekana kushahibiana kwa asilimia 99 na sampo za ndugu kadhaa wa Osama.

Ulichukuliwa na kuwekwa kwenye meli ya kivita ya Marekani, USS Carl Vinson iliyopo kaskazini mwa bahari ya Uarabuni ambapo taratibu za kidini zilifanyika na baadae mwili wake ulizikwa baharini.

Marekani ilisema kuwa iliamua kumzika Osama baharini baada ya kukosekana kwa mtu ambaye angeikubali kuizika maiti yake. Iliripotiwa kuwa Saudi Arabia iliukataa mwili wa Osama bin Laden.

Hata hivyo kumekuwa na maswali mengi kwanini Marekani iliamua kumzika Osama bin Laden baharini.

Kwa mujibu wa imamu Dr Abduljalil Sajid wa Uingereza ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la waislamu nchini Uingereza alisema kuwa si kweli kwamba hakuna mtu ambaye angejitolea kuupokea na kuuzika mwili wa Osama bin Laden.

Imamu Sajid alisema kuwa lazima kungekuwepo na mtu ambaye angejitolea kumzika kati ya ndugu zake wengi au mmoja wa watu wanaoshabikia itikadi zake za kigaidi.

Naye profesa wa sheria za kiislamu katika chuo kikuu cha University of Jordan, Mohammed Qudah alisema kuwa kumzika mtu baharini haikatazwi katika dini ya kiislamu lakini kwa sharti la kukosekana kwa mtu atakayekubali kuipokea maiti na kuizika kiislamu.

"Si kweli na wala si sahihi kusema kwamba hakuna mtu katika ulimwengu wa waislamu ambaye angekuwa tayari kuupokea mwili wa Osama bin Laden", alisema profesa Qudah.

"Kama familia imekataa kuipokea maiti, ni jambo rahisi katika uislamu, chimba kaburi kwenye ardhi yoyote ile hata porini, isalie maiti na kuizika", alisema mufti mkuu wa Dubai, Mohammed al-Qubaisi alipohojiwa kuhusiana na suala hilo.

Marekani katika kutoa maelezo ya mjadala huu imetoa sababu mbili za kuamua kuizika maiti ya Osama baharini, kwanza ili kuepuka kaburi lake kufanywa kama kaburi la shujaa na hivyo kujijengea umaarufu kwa watu wengi kulitembelea.

Pili serikali ya Marekani imesema kuwa haikuwa na muda wa kujaribu kutafuta muafaka na nchi zingine kuukubali kuuzika mwili wa Osama bin
Laden.
 

"TUNATAKA UBINGWA"

Barcelona imejikatika tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kutoka sare ya 1-1 na Real Madrid kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali.
Katika mchezo wa kwanza uliojaa na misukosuko Barcelona ilipata ushindi wa mabao 2-0.
Pedro aliipatia Barcelona goli hilo, huku Marcelo akisawazisha bao hilo.
Barcelona sasa watapambana na mshindi kati ya Manchester United au Schalke 04.
Fainali itachezwa Mei 28 kwenye uwanja wa Wembley, jijini London.