.

Thursday, January 27, 2011

WANAWAKE OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

Mwanafunzi aliyeongoza mtihani wa kidato cha nne kitaifa mwaka 2010,Lucylight Mallya (18),amebainika kuwa ni yatima ambaye wazazi wake wote wawili walifariki dunia miaka minne iliyopita.
anasema hakutegemea kama angekuwa wa kwanza na anamshukuru sana mungu na walezi wake waliofanikisha kufika hapo alipo..
Binti huyo alikuwa akisoma katika shule ya sekondari ya marian iliyoko mkoani pwani ,amekuwa akipenda sana kemia na biologia na fizikia .

VODACOM WAZINDUA SIMU MPYA KWA WALEMAVU

Mkuu wa kitengo cha mauzo wa Vodacom Tanzania Upendo Richard akionesha simu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuskia na kuona..kushoto ni meneja mawasilianao wa kampuni hiyo Nector Foya na kulia Msimamizi wa kitengo cha mauzo wa kampuni hiyo Ngope Kiwanga
Simu maalumu kwa watu wenye matatizo ya kusikia na wasioona pia.Baadhi ya huduma zilizopo katika siimu hiyo ni pamoj na maandishi makubwa katika keypard zake,sauti kubwa sana katika spika zake na kingora maalumu juu ya simu kitakachowawezesha  kuwasiliana wakati wa dharura.
Ni tofauti na simu za kawaida kwani huduma zilizopo katika simu hii hazipatikani katika simu za kawaida.
Simu hizo ni pamoja na S306ZTE ambapo zinapatikana katika maduka mbalimbali maarufu kama vodashop au kwa mawakala wote wa Vodacom waliopo nchi nzima.