.

Thursday, March 24, 2011

Simanzi kubwa...

Katika siku ambazo tumekumbwa na majonzi ni pale tulipopata taarifa za ajali mbaya iliyotokea mjini Morogoro na kusababisha vifo kwa wasanii 13 wa 5 Star Modern Taarab. Hili ni pigo kwa wengi hasa wapenzi wa muziki wa Taarab. Wengi wetu tumejiuliza ni nini tulichomuudhi mwenyezi Mungu kufikia kupata pigo kubwa namna hii.

Yote ni kumshukuru na kumuomba Mungu kila siku kwani hakuna ajuae siku itakayomfika mauti.

inna lillahi wa inna ilaihi rajioon

MWENYEZI MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI. AMIN

Siku miili ya marehemu ilipowasili hali ilikuwa tafrani...
Isha Mashauzi akilia kwa uchungu kwa kupoteza wafanyakazi wenzie

Hawa ni baadhi tu ya ndugu wa marehemu akiomboleza

Maiti zikipandishwa kwenye gari kwenda mazikoni ambapo wengine walizikwa bila baadhi ya viungo vyao...

Na hivi ndivyo basi walilosafiria lilivyokuwa upande mzima ulikatika...