Kwanza ni muhimu kujua nini kinasababisha mtu kunuka au kunukia.
Jasho linalotoka katika mwili wa mtu ni namna ya kupunguza joto la mwili, hili jasho ni mchanganyiko wa maji na kemikali za mwili ambazo zikikutana na bakteria husababisha harufu.
Jasho linalotoka katika mwili wa mtu ni namna ya kupunguza joto la mwili, hili jasho ni mchanganyiko wa maji na kemikali za mwili ambazo zikikutana na bakteria husababisha harufu.
Cha kufanya kuepuka hii harufu. Usafi wa hali ya juu yani kuoga mara kwa mara na vile vile matumizi ya pafyumu au bidhaa zinazotumika kupambana na jasho (antiperspirant) au kuondoa harufu ya jasho
(deodorant). Na matumizi haya yanapaswa kwenda sambamba na kazi au shughuli unazofanya.
Kama shughuli unazofanya zinahitaji nguvu na unatokwa na jasho sana basi unahitaji kuchagua bidhaa ambazo zitahimili mazingira yako ya kazi na kukuacha ukinukia vizuri wakati wote. Pia ni muhimu
kuzingatia suala la bei, tahadhari za matumizi na kudumu kwake.
Kudumu kwa pafyumu kunatokana na wingi wa mafuta kiujazo yani katika utengenezaji kuna kiwango cha mafuta ambacho kinatumika kuitengeneza. Wingi wa mafuta kwenye pafyumu kunasaidia mtumiaji.
kubaki ana nukia kwa muda mrefu “Eau de Perfumes (EDP) and Eau de Toilette (EDT).”
Kwa matumizi ya deodorant na antiperspirant, paka kwenye makwapa tu wakati unapohitajika kufanya hivyo hususan unapotoka kuoga.
Sehemu muhimu za kupaka pafyumu ili idumu kwa muda mrefu ni; nyuma ya masikio, shingoni, kwenye kiungio cha kuganja, nyuma ya kiwiko cha mkono na nyuma ya magoti. Kisha pulizia kidogo hewani kukuelekea wewe ili mwili wote uweze kuingiwa na unyevunyevu wa pafyumu
Na mwisho ni vizuri kupaka pafyumu unapotoka kuoga tu ila kuifanya idumu kwa muda mrefu, kwa wale wanaojifukiza kwa udi wanaelewa.
Na unashauriwa usipake pafyumu moja kwa moja kwenye makwapa kwa sababu inasababisha weusi na pia ina haribu nguo ikipakwa moja kwa moja kwenye nguo.