.

Thursday, July 28, 2011

BIG BROTHER GRAND FINALE!!!!!!!!!.................

Shindano la Big Brother ambalo lilianza Mei 1 mwaka huu linafikia tamati yake Jumapili wiki hii huku washiriki saba wakiwa bado ndani jumba hilo kugombea kitita cha 200 000 ambapo kwa mwa huu kutakuwa na washjindi wawili ambao watanyakua kitita hicho kila mmoja.














Washiriki waliobaki ni pamoja na Hanni wa Ethiopia,wawakilishi wa Nigeria Vina na Karen,Luclay ambaye anatoka Afrika Kusini,Lomwe wa Malawi,Wendal wa Zimbabwe pamoja na Sharon O ambaye ni mwakilishi pekee aliyebaki kutoka Afrika Mashariki wa nchini Uganda.



Katika fainali hizo wasanii mbalimbali watatoa burudani ambapo Tanzania inawakilishwa na mwanamuziki wa miondoko ya Crunk C PWAA,Fally Ipupa kutoka DRC,WizKid na Mo’Cheddah kutoka Naija Nigeria,Professor na Speedy kutoka Afrika kusini.

Kaa tayari Jumapili hii kuona nani atabahatika baada ya mchakamchaka wa siku 91 zenye furaha,majonzi,mabishano,mivutano,mahusiano na kila aina ya vituko vilivyofanyika ndani ya BIG BROTHER AMPLIFIED 2011 ambayo Tanzania iliwakilishwa vyema vya wanadada Bhoke Egina pamoja na Lotus Kyamba.


No comments:

Post a Comment