.

Thursday, July 28, 2011

JAY DEE MWANAMUZIKI ANAEHESHIMIKA KWA MATENDO YAKE............


Ijumaa iliyopita tarehe 22 July 2011 bendi inayoongozwa na mwanadada mahiri na anaheshimika nchini Tanzania Judith Wambura wengi tunamfahamu kama Lady Jay Dee ilitimiza miaka 6 tangu kuanzishwa kwake na kudhihirisha furaha na kuthamini mchango wawanaomzunguka Jay Dee aliamua kutoa tuzo wafanyakazi wake ikiwemo tuzo ya mfanyakazi bora,mfanyakazi mwenye nidhamu,mfanyakazi aliyeudumu n bendi kwa muda mrefu n.k vile aliweza kutoa tuzo kwa mashabiki wake ikiwemo best female na male suporter.





Hakika Jaydee atabaki kuwa mwanamuziki anayeheshimika siku zote nchini Tanzania kutokana na kujua anachokifanya katika kazi yake ya muziki ikiwemo kubuni vitu mbalimbali ambavyo vitaendelea kumuweka katika gemu muda mrefu kama hivi karibuni tulivyoona akizundua maji yake ya kunywa ya Jay Dee Pure Drinking water na kufanya vitu vingi katika jamii.

Blog Hii inamtakia kila la kheri Judith Wambura Mbibo ''Lady Jay Dee'' katika kila analofanya Mungu ataendelea kubariki kazi ya mikono yako kila siku endelea kuwa mfano wa kuigwa kila siku kwa wanamuziki wa sasa na wa baadae.....

No comments:

Post a Comment