.

Thursday, July 28, 2011

NICKI MINAJ APIGWA FAINI


Rapa wa kike wa Marekani Nicki Minaj amepigwa faini baada ya kuimba mashairi yenye lugha chafu jukwaani wakati akitumbuiza nchini Jamaica mwishoni mwa wiki.


Mwanamuziki huyo aliwasilishiwa hati ya kuvunja sheria za nchi hiyo baada ya kutumbuiza katika ukumbi wa Reggae Sumfest huko Montego Bay.ambapo alipigwa faini ya dola elfu moja za Jamaica ambazo ni sawa na dola 12 za Marekani kutokana na fedha za nchi hiyo kutokuwa na thamani.

No comments:

Post a Comment