.
Monday, May 30, 2011
KUJIAMINI KATIKA MAISHA
Katika maisha ya kila siku jitahidi sana kujiamini kwa kila unachokifanya itakusaidia sana . Jitahidi katika Kazi,Mapenzi, Masomo, Biashara na mambo mbalimbali itakusaidia kufika mbali sana .
Monday, May 23, 2011
Waombolezaji wakiupokea mwili tayari ya kuupeleka msikitini kwa maombi zaidi kabla ya maziko. |
Msafara ulianza kuelekea msikitini |
Mwili wa Mnajimu ukiwa tayari umeshaombewa dua tayari kwa maziko. |
Vijana wa Kiislam wakizkri wakati wa kuelekea kaburini. |
Mwili ukiwasili kwenye makaburi ya Tambaza kwaajili ya maziko. |
Waombolezaji wakisikiliza kwa makini Swala iliyokua ikitolewa na mmoja wa viongozi wa dini ya Kiislam. |
Chekibudi ni mmoja wa Wasanii waliohudhuria msiba huo. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimfariji mtoto wa Sheigh Yahaya Husein wakati akifuatilia maziko ya baba yake yakiendelea kaburini hapo. |
Baadhi ya watoto wa marehemu na viongozi wa dini ya Kiislam wakiupokea mwili wa Marehem kwaajili ya kuungiza mwandani. |
Hapa wakimuingiza mwandani. |
Pumzika Mnajimu wetu. |
Viongozi mbalimbali nao waliungana na ndugu wa marehem katika kuomboleza. Hapa Shamsi Vuai Nahodha akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu. |
Mzee wa Upako naye akiweka udongo. |
Steven Wasira akionesha upendo kwa marehemu. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dr. Jakaya M. Kikwete akiweka udongo kwa huzuni mkubwa. |
"Baba kwaheri tangulia sisi tuko nyuma yako" Mtoto wa Sheigh Yahaya Husein akiweka udongo kwenye kaburi la baba yake. |
Hii ni baadhi ya gari aliloacha Marehem likiwa limebeba watoto wa marehemu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali panapostahili kulingana na matendo yake na imani yake Amen. |
Saturday, May 21, 2011
JAMAA ANAKULA BATA KWA WACHINA.
Wabogojo mcheza Yoga maarufu nchini Tanzania ambaye aliwahi kucheza hata kwenye baadhi ya nyimbo za Lucas Mkenda a.k.a Mr. Nice, kwa sasa Wabogojo anakula bata nchini china akiendelea na shughuli yake hiyohiyo ya sanaa ya Yoga. Kwa taarifa zisizo rasmi, jamaa anadondoka jijini hivi karibuni kwaajili ya mapumziko.
SHEIGH YAHAYA HUSEIN HATUNAYE TENA.
MNAJIMU Mashuhuri Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein (81), amefariki dunia.Sheikh Yahya alifariki dunia jana majira ya saa nne asubuhi muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mtakatifu Ukombozi, Kinondoni Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla.
Mdogo wa marehemu, Nuru Hussein alisema kaka yake ambaye alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda wa miaka mitatu sasa, aliamka jana akiwa na afya njema na kuanza kuwatibu wagonjwa wake.“Alikuwa anaendelea vizuri tangu alivyoamka asubuhi. Aliwatibu hata wagonjwa wake waliokuwa na ratiba yakumwona leo (jana)," alisema na kuongeza:"Baada ya kumaliza kuwatibu, aliagiza juisi na hapo ndipo afya yake ilipobadilika.
Tulipompeleka hospitali akafariki.”Mtoto wa marehemu, Hussein Yahya alisema afya ya baba yake haikuwa mbaya alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake jana asubuhi lakini, ilibadilika ghafla baadaye.“Ni kweli Sheikh Yahya amefariki, ni kama majira ya saa nne na dakika kadhaa hivi asubuhi.
Tangu saa 12 alfajiri nilipofika kumsalimia alikuwa na afya njema tu, lakini ghafla hali ilibadilika na alipopelekwa hospitalini, alikata roho,” alisema Yahya na kuongeza:“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Ukombozi na utaratibu wa kuupeleka Hospitali ya (Jeshi) Lugalo unafanyika.
”Yahya alisema baba yake alikuwa anasambuliwa na maradhi ya moyo na aliwahi kupelekwa India kwa matibabu na kupata nafuu kwa kiwango kikubwa.Alisema baba yake ameacha watoto zaidi ya 20 na wajukuu wapatao 30.
“Nimekuwa mtu wa karibu sana kwa baba yangu. Nakumbuka siku tatu kabla ya kufikwa na mauti, kauli yake ya mwisho na ya msingi aliniuliza kuwa duniani kuna habari gani, nilipomweleza kuwa kiongozi wa upinzani wa Yemen Hassan Baoum ameachiwa, aliitikia sawa,”alisema.
Akizungumzia kazi ya utabiri wa nyota aliyokuwa akifanya baba yake, Yahya alisema, marehamu alikuwa anatabiri matukio mengi ambayo yalikuwa yanatokea akisema utabiri wake wa mwisho ni ule wa vifo vya wasanii wa Five Star uliotokana na ajali ya gari.
“Mzee alikuwa mtu wa kutabiri na kuacha matokeo yatokee. Tayari imethibitishwa kuwa alikuwa ni mtu mwenye elimu kubwa sana ya unajimu,” alisema.Yahya alisema ataendelea kufanya shughuli zote za utabiriakisema baba yake amemfundisha kazi hiyo.
“Utabiri utaendelea kama kawaida, amenifundisha kazi na nimekuwa nikifanya baadhi ya kazi zake wakati alipokuwa mgonjwa na hata leo (jana) nilipopata taarifa za kifo chake, nilikuwa Redio Uhuru kwenye kipindi cha nyota,” alisema.
Mwenyekiti wa kamati ya msiba huo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema marehemu atazikwa leo katika makaburi ya Tambaza, Dar es Salaam.Ibada ya mazishi ya Sheikh Yahya itafanyika leo saa 7:00 mchana katika Msikiti wa Tambaza, Upanga.
“Msiba huu ni mkubwa kwetu. Marehemu alikuwa kiongozi wetu mkubwa na tulimtegemea kwa mambo mengi. Atazikwa kesho (leo) alasiri, swala itafanyika katika Msikiti wa Tambaza na atazikwa katika makaburi ya Tambaza,” alisema.“Tulimpenda sana lakini Mungu amempenda zaidi. Tunaamini kila nafsi lazima ionje umauti hivyo Sheikh Yahya ndiyo siku yake ya mwisho.”
Utabiri wa Shekhe YahyaMoja ya utabiri aliowahi kutoa Sheikh Yahya Hussein enzi za uhai wake ni ule wa mwaka 2005, aliposema kuwa ipo siku CCM na CUF wataunda serikali moja.Mwaka huo 2005 Sheikh Yahya pia alitabiri kuwa Rais Benjamin Mkapa ataongezewa muda wa kutawala zaidi ya ule wa kikatiba.
Utabiri huo ulikuja kuwa wa kweli baada ya uchaguzi mkuu kusogezwa mbele kutokana kifo na mgombea mwenza wa Chadema. Katika kipindi hicho Mkapa aliendelea kuwa madarakani kwa miezi mitatu zaidi kabla ya uchaguzi mwingine kuitishwa.
Yahya aliwaambia waandishi wa habari kuwa aliona kinyota kuwa kuna mgombea atapoteza maisha lakini, kistaarabu hukusema hivyo.
Hata uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2000 alitabiri kuwa utarudiwa na ukawa kweli.
Julai 26 mwaka 2009, Sheikh Yahya pia alitoa utabiri mwingine uliotekenya fikra za watu pale alipoeleza kuwa kuna Rais wa nchi moja ya mashariki mwa Afrika atatekwa akiwa kwenye ndege au kupinduliwa.
Alisema tukio hilo, litatokana na hali ya kupatwa kwa jua kulikotokea Julai 24, 2009 huko China na kwingineko barani Asia.Katika utabiri huo Sheikh Yahya alieleza kuwa pia kutatokea matatizo katika mambo ya ulinzi na usalama kwa viongozi wa nchi mbalimbali za Mashariki ya Afrika.
"Pia natabiri baadhi ya wabunge kadhaa kufungwa na wengine kufa ghafla," akasema. Akaongeza kuwa baadhi ya maofisa wa ngazi za juu serikalini watafukuzwa kazi wakiwa nje ya nchi zao kwa kashfa mbalimbali.Hata hivyo baadhi ya utabiri wa Sheikh Yahya haukuwahi kutokea. Moja ya utabiri wake ambao haukutokea ni ule wa Oktoba 29, 2010 alipoeleza kuwa Uchaguzi Mkuu usingefanyika.
Mwenyewe aliwahi kutetea hoja hiyo kuwa ingawa uchaguzi haukuahirishwa kitendo cha watu kujitokeza kutaka usitishwe ni sehemu ya matokeo ya nyota yake na alisisitiza kuwa jambo hilo linaashiria kwamba elimu ya nyota huwa haisemi uongo.
Lakini Sheikh Yahya alitahadharisha kuwa kwa kawaida akishatabiri kitu kinachofuata ni kusubiri na siyo kazi yake kuhakikisha kwamba kile alichotabiri kinatokea.
“Kwa kawaida mtabiri anapotabiri siyo kazi yake tena kuhakikisha kile alichokitabiri kinatokea, kwa hiyo watu wasubiri tu waone kwa sababu siku bado zipo kabla ya uchaguzi,” alisema Shekhe Yahya.
Alikuwa akisisitiza kuwa utabiri wake hautumii uchawi kama wengi wanavyofikiri, isipokuwa anatumia hesabu za kinyota na wala siyo utashi wake au wa watu anaowatabiria.
Wasifu wa SheikhYahya Hussein
Sheikh Yahya Hussein, alizaliwa mwaka 1932 wilayani Bagamoyo katika familia ya Kabila la Kimanyema lenye asili ya Mkoa wa Kigoma.
Alipata elimu yake ya awali katika Shule ya Al-Hassanain Muslim ya Dar-es-Salaam. Baadaye alijiunga na Chuo cha Muslim Academy cha Zanzibar kilichokuwa kinamilikiwa na Sheikh Abdallah Swaleh Al-Farsy ambaye alikuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar wakati huo.
Alipohitimu mafunzo yake, alikwenda Misri kuendelea na masomo ya dini katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar kilichopo Cairo.Alirejea nchini mwanzoni mwa miaka ya 1960 na kuanza kazi ya kutabiri kwa kutumia nyota.
Wabogojo mcheza yoga, ambaye hapo awli alikua mcheza shoe kwenye baadhi ya nyimbo za Mr. Nice, sasa jamaa anakula bata mbele kwa jamaa zetu wa China. Kwa habari zisizo rasmi ni kwamba jamaa anakaribi kutua jijini kwaajili ya mapumziko. Tunaomba uzidi kututembelea tutazidi kukupa habari zaidi za maziko yake.

Thursday, May 19, 2011
"UNASHANGAAAA NINI? HII NDIYO STYLE YANGU MPYA YA SURUALI"
Hivi majuzi mwanamuziki wa Hip Hop wa nchini Marekani, Jay-Z alikuwa jijini Paris pamoja na mkewe, Beyonce, ambaye pia ni mwanamuziki nyota. Inasemekana wawili hawa walikuwa nchini Ufaransa ili kufanikisha utayarishaji wa video ya Beyonce inayokwenda kwa jina la "Run The World (Girls)." Video hii imetinga katika duka la mtandaoni, iTunes, siku za hivi karibuni.
Habari za udaku toka kwa paparazi wa Ufaransa zinasema wawili hawa walikwenda kupata chakula cha mchana katika mgahawa. Wanasema waliwaona wawili hawa wakiingia pamoja na suruali ya Jay-Z ikiwa katika hali ya kawaida lakini mara walipomaliza chakula na kuinuka ili kuondoka waligundua kwamba mtindo wa suruali ya Jay-Z ulikuwa umebadilika ghafla (picha zinajieleza).
Paparazi hawa wanasema Jay-Z alionekana kuwa na wakati mgumu katika harakati zake za kuirejesha suruali yake katika 'mtindo wa awali' bila ya mafanikio yeyote.
Baadhi ya watu waliopitia habari hii walikuwa na msawali mengi sana ya kujiuliza mara baada ya kuziona picha hizi. Mmoja wao aliuliza, "Ni maongezi gani yaliyokuwa yakiendelea kati yao wakati wa chakula hadi jamaa kukutwa na zahma ile?", mwingine alisikika akisema, "Inaelekea Beyonce ni mke mwema na mwenye kuifahamu vyema kazi yake kama mke. Ukiwa na mke kama Beyonce huwezi kuwa na nyumba ndogo, maana anakukamata vile inatakiwa. Hongera Jay-Z kwa kuonesha hisia zako za kweli."
Lakini pia wapo waliosema kitendo hiki cha Jay-Z kuharibu 'mtindo' wa suruali yake kimefanywa makusudi na kwa kupangwa na wawili hawa ili kuitangaza video hii ya Beyonce. "Walikuwa wanajua wanachofanya, walijua paparazi wanawafatilia. Ukitazama jina la wimbo na video hiyo halafu ukatazama mchezo wa Jay-Z na vile Beyonce amevaa, basi huwezi kusita kusema kwamba jamaa wametuchezea senema. Shukrani nyingi kwa ubunifu wa wawili hawa katika kuuza kazi zao. Nimesikia kuhusu video hii kupitiai habari hii na nitainunua."
Wasanii wa Kibongo mna jambo la kujifunza hapa, kumbe haitoshi kusema tu kwamba umetoa singo au albamu, ni lazima utengeneze na ka-drama kidogo ka kuonesha msisitizo kwa kile unachosema. Nakumbuka mtu aliyekuwa na mautundu kama haya kwa hapa kwetu alikuwa ni Ali Choki ambaye aliishia kufahamika almaarufu kama "Mzee wa Farasi" baada ya kuingia ukumbini akiwa kabebwa na farasi, ilikuwa habari kubwa siku ya pili kwenye magazeti.
Kwenye kila jamboa, lipo jema unaweza kujifunza ili kukuza usanii wako. Simaanishi na nyie kesho muende na mademu wenu kwenye migahawa na kubadili 'mitindo' ya suruali, la hasa, mtafungiwa kufanya kazi zenu.
Siku njema.
RIHHANA APONEA CHUPUCHUPU KUUZWA.
Baba-mwana uhusiano wa mwimbaji maarufu kutoka Barbados si "paa cool sweep makasia" nguvu na vitendo "kuuzwa nje" binti yake kwa vyombo vya habari za mtu huyu fedha.
Katika mazungumzo na suala Vogue idadi gazeti 4 / 2011, mwimbaji Umbrella umebaini kuwa hadithi yake ni wengi heartbreaking ya baba yake - Mheshimiwa Ronald Fenty, labda ya hadithi alielezea katika kipindi na hata vunjwa yote ya picha yake ya utotoni na kuuza mbali Photographers.
"Ni hufanyaMimi ajabu ambaye baba yangu ni kama. Yeye walijivuna kama mimi si binti yake, sikuwa na thamani yake hivyo, "alisema Rihanna na machozi.
Anaongeza: "Ni weird! Na mimi pia na maneno kabisa kuelezea kile uzoefu. Mimi ilikua juu ya baba, najua naye, mimi ni sehemu ya maisha yake. Na hatimaye yeye ana tabia ambayo mimi siwezi kuelewa. "
"Mimi daima kusikia hadithi ya nyuma trampled, kuuzwa nje ya hadithi wapendwa wengi, lakini bado nadhani:". Hiyo si kutokea katika familia yangu baba yangu hawezi kufanya hivyo ".. Bado hatimaye akaenda kuona baba yangu na kuwaambia waandishi wa habari kuhusu rundo la uongo Daraja. Kamwe kuitwa baba yangu, si kujaribu kujua jinsi mimi kuishi. Anapenda kuuliza vyombo vya habari zaidi. Hivi karibuni, alifanya hivyo ...," Rihanna imeonekana sana haraka.
Hatimaye, msichana ilionyesha nguvu na ngumu kama milele: "Sasa huna haja makini au inajaribu ndoano mtu kama kwamba kufanya."
CAF YASIKILIZA KILIO CHA SIMBA SC.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeipa unafuu, Simba katika mechi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Wyadad de Casablanca Morocco kwa kuipeleka
mbele kwa siku kumi kuanzia jana.
Mechi hiyo ambayo Simba, inacheza na Wyadad, baada ya Mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kuenguliwa na CAF kwa kumchzesha Janvier Besala Bokungu aliyekuwa na mkataba na timu ya Esperance ya Tunisia, itachezwa kati ya Mei 27, 28 na 29 mwaka huu katika uwanja huru.
Taarifa hiyo ya CAF iliyotumwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuchezwa tarehe hizo inaonekana kuwa ahueni kwa Simba kwani kwa sasa itakuwa na muda wa kujiandaa vyema, tofauti na taarifa za awali ambazo zilidai mechi hiyo ingechezwa wiki hii wakati wawakilishi hao wa Tanzania wakiwa hawajakaa sawa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alieleza kuwa Simba na Wydad de Casablanca ya Morocco ndizo zitakazopambana katika mechi hiyo ya mkondo mmoja.
Alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), linatarajia kutaja katika muda mfupi ujao nchi ambayo mechi hiyo itachezwa.
Wambura alisema timu itakayoshinda mechi hiyo itaingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, ikiwa kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, Esperence ya Tunisia na Moloudia Club d’Algerya Algeria.
Aliongeza kwamba pia timu itakayoshindwa katika mechi hiyo, itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya kwanza nyumbani na Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na 12 mwaka huu.

KAMA WEWE NI KIBONGE NA UNATAKA KUPUNGUZA UBONGE, ZINGATIA YAFUATAYO.
1-ULAJI
Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila.
Unavyokula.
-Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili.
(PENDEKEZO la kwanza. Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi…)
-Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga.
Tatizo ni kwamba mipangilio yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula. Vimeng’enya chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga. Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini, nk.
Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu.
-Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (acid) na vile vinavyomumunyuka haraka (alkine) havitakiwi viliwe pamoja. Mfano ni matunda. Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi: ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumeng’enywa.
Hali hiyo pia iko katika nyama. Nyama nyeupe (ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu (ng’ombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti.
Chakula unachokula
Waafrika hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.
Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame. Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika. Kenya na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi.
Ulaji wa mboga mbichi ni upi?
Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karote. Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene.
(PENDEKEZO LA 2. Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani.)
2-UNYWAJI MAJI
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake. Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo. Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi na gesi za kisasa kama Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai. Kuliko maji. Na maji haya hutakiwa dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada ya chakula. Ukila chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu una kiu. Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu viwili tofauti. Ila utawaona watu wanakula huku wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion).
Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu tumboni. Matokeo wengi wetu tuna matumbo makubwa. Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk.
3-SUALA LA UMENG’ENYAJI
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa lugha iliyozoeleka) mdomoni. Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama kikipita hakisaidii lolote mwilini. Utafunaji wa taratibu husaidia umeng’enyaji. Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini. Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho. Kule uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini.
Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona watu wengine wanakula sana lakini hawana afya. Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara moja au mbili kwa siku) nk.
4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA
Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake shurti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana. Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani “protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).
Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma (nyama nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri shauri hayatoki, huganda. Chukua nyama ya kuku na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya.
Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini.
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.
PENDEKEZO LA 3- Kula mbegu mbegu za korosho, karanga au mlozi (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.
Chips za Magimbi zilizopikwa na kuonyeshwa ndani ya tovuti ya Miriam Rose , dada wa Kibongo anayetukuza mapishi ya Kitanzania duniani. Habari zaidi tembelea : www.tasteoftanzania.com
5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO
Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.
Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.
Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.
Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu. Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk) …
Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.
Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku. Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa.
6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI
Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na pumzi. Haya ya pili ni kama Yoga (India) , Tai Chi Chuan (China) na aina mpya mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates). Haya laini yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80 hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili.
Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk. Mataifa yenye watu wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk huwa na wachapa kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao.
7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI
Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha. Kisayansi vyakula vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha maisha. Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.
Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha. Mtu ukiwa na kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea kuutesa mwili. Kwa vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana vifo vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha haupiti miaka 50.
Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari. Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema.
8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA
-Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza mwaka jana kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na purukshani) kwa asilia mia 42 kama utakula matunda na mboga za majani peke yake kila siku, juu ya msosi wa kawaida.
(PENDEKEZO LA KULA- Na 4- Kula mlo wako. Baada ya saa mbili au tatu, sakatia tunda au matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya mseto wa mboga mbichi kama karote na matango. Utaona tofauti ya afya, ngozi, wajihi, kinyesi, usingizi, nk. Kidesturi tumezoea kunywa chai au soda za sukari sukari na gesi kati kati nya milo badala ya matunda na mboga mbichi za majani).
-Utafiti uliofanywa na wanasayansi chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea.
Zoezi la kuogelea lina faida zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa asili mia hamsini.
-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya umeeleza (desemba 2009) kwamba kulala nusu saa kila mchana (“nap”) husaidia kupunguza ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37.
-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania mwanzoni mwa 2010 umethibitisha kwamba ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging) unaongeza nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa kwa watu wa makamo mnaoanza kupoteza nguvu za urijali.
-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza mwanzoni mwa 2010 umeonyesha unapotembea kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa na mioshi ya magari (pollution) unapunguza matatizo ya maradhi ya hewa chafu kama pumu, mapafu na appendix.
-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka 2010 umegundua kwamba kula tunda la divai nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza kupata ugonjwa wa kisukari.
-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na bara la Asia wanakumbwa zaidi na ugonjwa wa kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na gesi (fizzy drinks). Ukinywa kiasi cha miligramu 300 za vinywaji hivi (Cocacola, Red Bull, Fanta, nk) kwa siku unajitahadharisha kupata kisukari.
9-KUFUNGA
Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo (Lenti nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini tofauti na haya ya kiafya.
Mathalani wafungaji hawa hula chakula kingi usiku; ukihesabu wanafunga wastani wa saa 12 tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka nyingine mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji saa 20 kuendelea.
Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendelea…
Ufungaji ni nini?
Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi. Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.
Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk.
Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.
1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea…
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea…
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea…
Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua. Ukianza kula tena, unaanza taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu. Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika. Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu.
Maana lengo lake ni kusafisha mwili.
PENDEKEZO LA 5- Kwa wenye imani za kidini. Unaweza pia kufunga hivi ukawa pia unasali au kuvaa mavazi yanayokufanya mtu wa amani. Ukifanya hivi unajitakasa kimwili na kiroho. Si lazima ungojee ile miezi ya kufunga na wengine.
10-USINGAJI
Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene. Ikiwa unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri. Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na taswira yako mwanadamu. Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.
Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama nyumba au hekalu lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi, tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza taratibu…
Wednesday, May 18, 2011
Bob Marley & The Wailers ilikuwa bendi ya muziki wa reggae ambayo ilianzishwa na Bob Marley mnamo 1974, baada ya Peter Tosh na Bunny Wailer kuondoka katika bendi ya awali, The Wailers. Ndugu wawili Carlton (ngoma) na Aston "Family Man" Barrett (besi) – ambao walijiunga na The Wailers miaka minne kabla – wameamua kubaki na Marley.
Barret ndugu awali walipiga na Wailers wakati wapo kwenye studio ya Lee "Scratch" Perry na bendi ya The Upsetters [1]
Bob Marley & The Wailers inaunganishwa na Bob Marley mwenyewe akiwa kama mpiga gitaa, mtunzi wa nyimbo na mwimbaji kiongozi wa bendi, kina Wailers Band ipo kama bendi saidizi, na kina I Threes wakiwa kama waimbaji wasaidizi. The Wailers Band inajumlisha ndugu wawili ambao ni Carlton na Aston "Family Man" Barrett katika upande ngoma na besi kwa ujumla, Junior Marvin na Al Anderson yupo kwenye upande wa gitaa kuu, Tyrone Downie na Earl "Wya" Lindo kwenye upande wa vinanda, na Alvin "Seeco" PattersonRita Marley, Judy MowattMarcia Griffiths. kwenye upande wa tumba. The I Threes, wanasindikizana na mke wa Bob Marley na
Wakati mwingine, hasa kwa sababu za kimasoko, rekodi hizi hutofautisha kwa ajili ya "Bob Marley", "The Wailers", au "Bob Marley & the Wailers".
FANYA KINWA CHAKO KIWE SAFI NA KUJIKINGA NA MARADHI.
Zirostomia (Xerostomia) ni neno la kigiriki litumikalo kwenye tiba kumaanisha hali ya kinywa kikavu (xeros – kavu, stomia – hali ya kinywa) . Udhaifu wa tezi za mate ni tafsiri nyingine ya Zirostomia. Hali ya kinywa kikavu hujitokeza pale mtu anapohisi ukavu wa kinywa kutokana na kupungua kwa mate kinywani. Hakika hali ya kinywa kikavu sio ugonjwa bali ni dalili za ugongwa fulani. Kuwapo kwa dalili hii kunaashiria upungufu wa uzalishwaji wa mate kinywani kwa kiwango fulani
Zirostomia inasababishwa na nini?
Kuna sababu kadhaa zinazosababisha hali ya kinywa kikavu zikiwamo:-
- Uvutaji wa sigara: hiki ni chanzo kikuu cha hali ya kinywa kikavu
- Baadhi ya madawa yanayotumika kutibu baadhi ya magonjwa hudhoofisha ufanisi wa tezi mate. Tafiti zinaonesha kuwa zaidi ya aina 400 ya madawa yanayotumika hospitalini husababisha dalili za hali ya kinywa kikavu. Mfano madawa yatumikayo kudhibiti shinikizo la damu, dawa zitumikazo kutibu ugonjwa wa Parkinson, dawa zitumikazo kutibu mzio, dawa za kutibu mafua , dawa zitumikazo kutibu vidonda vya tumbo na baadhi ya dawa za maumivu husababisha hali ya kinywa kikavu.
- Hali zinazosababisha upungufu wa maji mwilini kama homa, kuvuja jasho kwa wingi, kutapika ama kuharisha kunaweza kusababisha hali ya kinywa kikavu kwa muda.
- Baadhi ya magonjwa na hali zinazoathiri mwili mzima ikiwamo tezi za mate husababisha hali ya kinywa kikavu i.e. (ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa parkinson, HIV/AIDS etc)
- Tiba ya kansa (mionzi ama madawa) vinaweza kuharibu tezi za mate na kuathiri uzalishaji na usambazaji wa mate kinywani.
Zirostomia ina athari zipi kwa utunzaji wa afya ya kinywa na meno?
Zirostomia siyo hali ya kawaida. Imezoeleka kuona damu, mkojo na machozi vikitumika kwenye uchunguzi wa hali ya afya na magonjwa. Wakati huo huo mate (sio makohozi) hayapewi uzito kwenye uchunguzi wa afya na magonjwa. Kazi kubwa ya mate ni kulinda na kutunza afya ya kinywa na meno, vile vile yanasaidia kwenye uyeyushaji wa chakula kinywani, kutambua ladha na hata kuongea na kuimba, isitoshe mate ni kiashiria muhimu cha kutambua hatari ya magonjwa yanayoshambulia mfumo wa damu mwilini na hata hali zingine za mwili kama ujauzito.
Hali ya kinywa kikavu hakika sio kitu cha kawaida, na jamii nzima inapaswa kuelimishwa na kutambua hali hii inapotokea na watu wote wanaokuwa na hali ya kinywa kikavu hawana budi kumwona daktari wa meno kwa ushauri na tiba. Wagonjwa wenye hali ya kinywa kikavu ambao hawapati ushauri na tiba ya kudhibiti hali hii mapema mara nyingi wanapata tatizo kubwa la kuoza meno mengi kwa mpigo na kuvimba kwa kuta zizungukazo kinywa na fizi. Matatizo haya hutokea kwa sababu ya upungufu wa mate kinywani ambayo kwa kawaida huwa na vimeng’enya na viasili ambavyo husaidia kinywa kujisafisha chenyewe na hivyo kuzuia kuoza meno na kuvimba kwa fizi na kuta nyinginezo kinywani.
Nitajuaje kuwa naathirika na Zirostomia?
Kwa kawaida, tezi za mate ni kama kiwanda hivi. Tezi zinahitaji malighafi , machine na umeme ili kuzalisha mazao yaliyokusudiwa. Ikiwa kutatokea mabadiliko kwenye mchakato na mzunguko wa uzalishaji , ni wazi mazao yaliyokusudiwa hayatatokea.
Tukirudi kwenye tezi za mate, tunafahamu kuwa tatizo lolote litakaloathiri upatikanaji wa metabolites kama maji, kuharibiwa kwa tezi kutokana na ugonjwa ama jeraha, na kudhoofu kwa mfumo wa neva za tezi hupunguza uzalishaji wa mate kinywani.
Hatua za awali za zirostomia zaweza kuwa na dalili kidogo zisizoshtua mgonjwa, hata hivyo kadiri muda unavyoendelea hali inaweza kuwa mbaya zaidi hususani mgonjwa anaposhindwa kula na kuongea vizuri. Hatua hii huenda sambamba na kuhisiwa kwa harufu mbaya kutoka kinywani. Ili kubaini kama Zirostomia imefikia hatua mbaya, uchunguzi wa ufanisi wa tezi za mate hufanyika kwa kukusanya mate (kwa kutumia kifaa maalumu) na kupima kiasi cha mate ambacho mgonjwa anazalisha ndani ya dakika tano. Vipimo vingine vitumikavyo kupima ufanisi wa tezi hufanyika kitaalamu zaidi kwa kutumia Ultrasound mashine tezi ama kwa mionzi maalumu ya tezi za mate (Parotid Sialography).
Tafiti zimeonesha kuwa mmoja kati ya watu wazima wanne hulalamika kuwa na hali ya kinywa kikavu ama kuvimba kwa kuta za kinywa na fizi, matokeo ya utafiti huu yanafanana na ukweli kuwa 40% ya watu wazima hulalamika kuwa na hali ya kinywa kikavu kwa vipindi fulani hivyo kuonyesha kuwa Zirostomia ni tatizo bubu miongoni mwa jamii.
Tiba ya Zirostomia ni nini?
Matibabu ya zirostomia inayomkabili mgonjwa yanategemea chanzo chake, baadhi ya njia zitumikazo kutibu Zirostomia ni:-
- Kunywa maji mengi kudhibiti upungufu wa maji mwilini.
- Epuka vyakula vyenye caffeine kwa wingi kama kahawa, chai na baadhi ya vyakula vyenye magadi kwa wingi.
- Epuka uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupindukia
- Tafuna jojo zisizo na sukari ili kuchagiza uzalishwaji mate kinywani
- Tumia “chinese green tea”, chamomile na ginger kuchagiza uzalishwaji mate.
- Ikiwa hali ya kinywa kikavu inasababishwa na dawa, tafadhali mwone daktari wa meno kwa ushauri.
Subscribe to:
Posts (Atom)