.

Thursday, May 19, 2011

"UNASHANGAAAA NINI? HII NDIYO STYLE YANGU MPYA YA SURUALI"

 



















 Hivi majuzi mwanamuziki wa Hip Hop wa nchini Marekani, Jay-Z alikuwa jijini Paris pamoja na mkewe, Beyonce, ambaye pia ni mwanamuziki nyota. Inasemekana wawili hawa walikuwa nchini Ufaransa ili kufanikisha utayarishaji wa video ya Beyonce inayokwenda kwa jina la "Run The World (Girls)." Video hii imetinga katika duka la mtandaoni, iTunes, siku za hivi karibuni.
Habari za udaku toka kwa paparazi wa Ufaransa zinasema wawili hawa walikwenda kupata chakula cha mchana katika mgahawa. Wanasema waliwaona wawili hawa wakiingia pamoja na suruali ya Jay-Z ikiwa katika hali ya kawaida lakini mara walipomaliza chakula na kuinuka ili kuondoka waligundua kwamba mtindo wa suruali ya Jay-Z ulikuwa umebadilika ghafla (picha zinajieleza).
 
Paparazi hawa wanasema Jay-Z alionekana kuwa na wakati mgumu katika harakati zake za kuirejesha suruali yake katika 'mtindo wa awali' bila ya mafanikio yeyote.
Baadhi ya watu waliopitia habari hii walikuwa na msawali mengi sana ya kujiuliza mara baada ya kuziona picha hizi. Mmoja wao aliuliza, "Ni maongezi gani yaliyokuwa yakiendelea kati yao wakati wa chakula hadi jamaa kukutwa na zahma ile?", mwingine alisikika akisema, "Inaelekea Beyonce ni mke mwema na mwenye kuifahamu vyema kazi yake kama mke. Ukiwa na mke kama Beyonce huwezi kuwa na nyumba ndogo, maana anakukamata vile inatakiwa. Hongera Jay-Z kwa kuonesha hisia zako za kweli."
Lakini pia wapo waliosema kitendo hiki cha Jay-Z kuharibu 'mtindo' wa suruali yake kimefanywa makusudi na kwa kupangwa na wawili hawa ili kuitangaza video hii ya Beyonce. "Walikuwa wanajua wanachofanya, walijua paparazi wanawafatilia. Ukitazama jina la wimbo na video hiyo halafu ukatazama mchezo wa Jay-Z na vile Beyonce amevaa, basi huwezi kusita kusema kwamba jamaa wametuchezea senema. Shukrani nyingi kwa ubunifu wa wawili hawa katika kuuza kazi zao. Nimesikia kuhusu video hii kupitiai habari hii na nitainunua."
 
Wasanii wa Kibongo mna jambo la kujifunza hapa, kumbe haitoshi kusema tu kwamba umetoa singo au albamu, ni lazima utengeneze na ka-drama kidogo ka kuonesha msisitizo kwa kile unachosema. Nakumbuka mtu aliyekuwa na mautundu kama haya kwa hapa kwetu alikuwa ni Ali Choki ambaye aliishia kufahamika almaarufu kama "Mzee wa Farasi" baada ya kuingia ukumbini akiwa kabebwa na farasi, ilikuwa habari kubwa siku ya pili kwenye magazeti.
Kwenye kila jamboa, lipo jema unaweza kujifunza ili kukuza usanii wako. Simaanishi na nyie kesho muende na mademu wenu kwenye migahawa na kubadili 'mitindo' ya suruali, la hasa, mtafungiwa kufanya kazi zenu.
Siku njema.

No comments:

Post a Comment