.

Thursday, May 19, 2011

CAF YASIKILIZA KILIO CHA SIMBA SC.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeipa unafuu, Simba katika mechi ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Wyadad de Casablanca Morocco kwa kuipeleka
mbele kwa siku kumi kuanzia jana.

Mechi hiyo ambayo Simba, inacheza na Wyadad, baada ya Mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kuenguliwa na CAF kwa kumchzesha Janvier Besala Bokungu aliyekuwa na mkataba na timu ya Esperance ya Tunisia, itachezwa kati ya Mei 27, 28 na 29 mwaka huu katika uwanja huru.

Taarifa hiyo ya CAF iliyotumwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuchezwa tarehe hizo inaonekana kuwa ahueni kwa Simba kwani kwa sasa itakuwa na muda wa kujiandaa vyema, tofauti na taarifa za awali ambazo zilidai mechi hiyo ingechezwa wiki hii wakati wawakilishi hao wa Tanzania wakiwa hawajakaa sawa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alieleza kuwa Simba na Wydad de Casablanca ya Morocco ndizo zitakazopambana katika mechi hiyo ya mkondo mmoja.

Alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), linatarajia kutaja katika muda mfupi ujao nchi ambayo mechi hiyo itachezwa.

Wambura alisema timu itakayoshinda mechi hiyo itaingia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, ikiwa kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, Esperence ya Tunisia na Moloudia Club d’Algerya Algeria.

Aliongeza kwamba pia timu itakayoshindwa katika mechi hiyo, itaingia katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya kwanza nyumbani na Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na 12 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment