.

Tuesday, May 10, 2011

ANCELOTTI APATA MKOMBOZI.

Meneja msaidizi wa zamani wa Chelsea Ray Wilkins, amesema meneja wa Chelsea anayekabiliwa na chagizo kubwa la kuondolewa, Carlo Ancelotti hapaswi kutimuliwa mwishoni mwa msimu huu wa ligi.
 
Mustakabali wa Ancelotti unatokana na tetesi nyingi zinazoenea hivi sasa baada ya Chelsea kumaliza msimu mikono mitupu.
Lakini Wilkins aliiambia BBC Radio 5: "Sidhani kama klabu inahitaji mabadiliko ya haraka... lakini kwa hakika wachezaji wapya ndio wanahitajika kuongeza nguvu katika kikosi kilichopo.
"Mabadiliko ya jumla, kwa kuanzia kwa kocha, itakuwa ni makosa makubwa."
Chelsea inajiandaa kumaliza msimu bila kombe lolote baada ya kuchapwa na Manchester United siku ya Jumapili, wakiwa na matumaini ya kumaliza nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya England.
United pia iliiondoa Chelsea katika mashindano ya ligi kuwania Ubingwa wa Ulaya mwezi wa Aprili.
Meneja wa zamani wa Chelsea Guus Hiddink, aliyeiongoza klabu hiyo kuchukua kombe la FA mwaka 2009, amekuwa akitajwa-tajwa huenda akarejea Stamford Bridge, ingawa kocha huyo Mrusi inaarifiwa hapendelei kazi hiyo.
Waholazi wawili Marco van Basten na Frank Rijkaard pia wametajwa kuwa nao wanaweza wakapewa kazi ya kuinoa Chelsea msimu ujao, pamoja na Andre Villas-Boas, aliyeiwezesha Porto kufika hatua ya fainali ya Europa msimu huu.
Mwengine anayehusishwa kupewa kazi ya kuifundisha Chelsea ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Gianfranco Zola aliyewahi kuwa meneja wa West Ham.
Ancelotti, ambaye mkataba wake umesalia mwaka mmoja, alikiri siku ya Jumatatu kwamba timu yake haikuwa imara msimu huu, lakini akakanusha mabadiliko makubwa yanahitajika katika kikosi chake.

No comments:

Post a Comment