Mtoto Lu Hao wa nchini China pamoja na kwamba ana umri wa miaka 3 ana uzito ambao ni mara tano zaidi ya uzito wa mtoto wa umri wake, ana jumla ya kilo 60. Lu Hao, mtoto wa miaka mitatu wa nchini China, alizaliwa akiwa na uzito usiozidi kilo 2.5 lakini hivi sasa ana uzito ambao ni sawa na uzito wa watoto watano wa umri wake wakiwekwa pamoja.
Uzito wa Lu Hao mbali ya kuwashangaza wazazi wake, umewashangaza pia madaktari wa nchini China ambao wameshindwa kujua nini kimemsibu mtoto huyo.
Wazazi wake wamejaribu kila njia ya tiba ya mtoto huyo bila mafanikio na majaribio ya kumlazimisha Lu Hao kula kiasi kidogo cha chakula yamefeli kutokana na mtoto Lu Hao kuangua kilio muda wote mpaka anapopewa chakula chake.
Katika mlo mmoja mtoto huyo huweza kufagia sahani kadhaa za wali na nyama.
"Inatubidi tumuache awe jinsi anavyotaka, tunapomnyima chakula huangua kilio bila kupumzika", alisema mama yake Lu Hao, Chen Yuan.
"Katika mlo mmoja, humaliza sahani tatu kubwa za wali", alisema baba wa mtoto huyo na kuongeza "Tusipompa chakula hufanya vurugu na kuangua kilio siku nzima".
Mtoto Lu Hao anapenda kuogelea lakini hapendi kutembea hali iliyowafanya wazazi wake wawe wanampeleka shule ya chekechea kwa pikipiki.
Wazazi wake wamemtengenezea sehemu ya mazoezi ambapo kila wanapomlazimisha kufanya mazoezi ndivyo anavyosikia njaa zaidi na kula sana na hivyo kuzidi kunenepa.
No comments:
Post a Comment