.

Friday, May 6, 2011

ALIYEJICHOMA MOTO KUFUNGULIWA MGAHAWA.

MWANAMKE mmoja [32] mkazi wa jijini Dar es Salaam, aliyeweza kujiunguza na maji ya moto ili aweze kuomba barabarani apatiwe mtaji, nduguze wamfungulia mradi wa kuendesha mgahawa eneo la Buguruni.

Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, ndugu waliomkataza aachane na kuomba barabarani kwa pamoja walishirikiana kumtafutia mtaji na kumfungulia mgahawa ikiwa ni kumtaka aendeshe maisha yake pasipo kuomba.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo tayari ameshaanza biashara hiyo mwanzoni mwa wiki hii na kudaiwa kuwashukuru ndugu zake waliojitolea kumfungulia biashara hiyo.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo anaapa kutokuwa na hamu ya kuolewa kwa kuwa tayari alishapata mateso kutoka kwa mtalaka wake ambaye alimtelekeza na mtoto na kuishi maisha magumu yaliyompelekea kuomba ili ndugu zake waweze kumsaidia.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alitumia mbinu ya kuomba barabarani ili aweze kupatiwa msada na ndugu zake kwa kuwa ndugu hao hakuna aliyeamini kama angekosa mtaji kwa kuwa ilidaiwa alikuwa na maisha ya juu alipokuwa na mumuwe huyo.

No comments:

Post a Comment