.

Friday, May 6, 2011

"JAMANI MIMI SIYO BILLIONEA NI VIJISENT TU HIVI VYA MBOGA"

MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete ameukana ubilionea aliovishwa na wanasiasa wa vyama vya upinzani.
  Amekanusha hayo baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, kuutangazia umma kuwa ni Ridhiwani Kikwete ni bilionea na kuhoji ubilionea wake umetoka wapi.

Ridhiwani aliwataka Watanzania wasimhukumu kwa kumuona mitaani akiendesha magari ya bei ghali.

“Mi naishi na watu vizuri hapa mjini jamani, tunaishi kimjini mjini na si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake,”, alisema Ridhiwani.

"Hii inatokana na malezi ya wazazi wangu yaliyonieleza kuishi na watu vizuri”, alieleza Ridhiwani

“Hayo wanayonizushia mimi kuwa ni bilionea na namiliki kampuni ya malori 150 na kampuni ya ujenzi pamoja na ghorofa za kupangisha mjini mimi nasema si kweli”.

Alibainisha kuwa habari hizo ni za uongo na uzushi na zimelenga kumchafua yeye na mzazi wake na kupandikiza chuki dhidi ya familia yake na jamii.

Alisema hatua waliyochukua si nzuri na kubainisha kuwa anawaheshimu sana kutokana na umri wao na kuwataka watoe ushahidi wa hayo kwenye vyombo vya habari

Hata hivyo Ridhiwani alibainisha mali zake anazomiliki kuwa ni shamba la hekari moja na nusu lililopo Bagamoyo, gari aina ya Toyota Cami na akaunti mbili katika benki za Stanbic na NBC.

No comments:

Post a Comment