.

Friday, May 6, 2011

KOVA: WANAWAKE KUWENI MAKINI.

JESHI la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewatahadharisha wanawake nchini, kutodanganyika kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume papo kwa papo kwa kuwa kumekuwa na wimbi la mauaji wanawake baada ya kujitokeza mwanaume anayewarubuni.
  Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suileman Kova, amesema amejitokeza mwanaume anayetuhumiwa kuua wanawake waliofikia wanne jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Tandika, Keko, Mtoni kwa Azizi Ally na Buguruni kwa Mnyamani katika kipindi cha miezi mitatu.

Amesema mwanaume huyo amekuwa akirubuni wanawake hao kimapenzi kwa kuwaahidi donge nono la fedha na kisha kwenda nao katika nyumba za kulala wageni na kuwalazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile na anapomaliza haja zake kuwanyonga.

Kova amesema katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi limebaini kuwa katika nyumba zote za wageni walizouawa wanawake hao wamebaini ni mwanaume wa aina moja ambaye wahudumu wa nyumba hizo walipoeleza mazingira na maelezo yao yamefafana na kudai kuwa mwanaume huyo hupendelea kuvaa vazi la T-shirt na suruali aina ya jeans, mweupe, mtanashati na kukadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 32.

Kova amesema mtuhumiwa huyo ambaye anasakwa ameonekana kuwalenga wanawake ambao wako ndoani [wake za watu] kwa kuwarubuni kuwaahidi fedha nzuri na kasha kuwanyonga na kutokome bila hata kuiba kitu chochote kutoka kwa marehemu.
.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kumsaka mtuhumiwa huyo kumkamata na kumchukulia hatua zinazostahili na jamii wametakwi kutoa ushirikiano katika suala hilo.

No comments:

Post a Comment