.

Monday, August 22, 2011

KIM KARDASHIAN NA KRIS HUMPHRIES WAFUNGA NDOA..................

Mlimbwende Kim Kardashian na mchezaji wa mpira wa kikapu wa NBA Kris Humphries wamefunga ndoa huko katika jimbo la Montecito,California siku ya Jumamosi usiku.

Kardashian alitupia gauni matata lililobuniwa na Vera Wang ambalo kwa mujibu wa ripoti lilikuwa Inspired na gauni alilovaa Pippa Middleton katika harusi ya kifalme iliyofungwa Uingereza Aprili mwaka huu ambapo wasimamizi pamoja na mama yake Kardashian walivaa nguo za Disigner huyo.

Maceleb waliofika katika party hiyo ni pamoja na Eva Longoria, Lindsay Lohan na Melanie Brown, ambaye alikuwa na hofu ya ukubwa wa ujauzito wake kumkosesha siku hiyo kubwa.

Endelea kufatilia blog hii kwa picha kamili za siku hiyo kubwa kwa bibie Kim K.........

No comments:

Post a Comment